AN-NUUR
Na.185 Shawwal 1419, Januari 22 - 28, 1998
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
Historia: Form IV


Upinzani dhidi ya Serikali ya Kiislamu wakati wa Khalifa wa Tatu Uthman bin Affan

Watu wa Madina wanasema, nina pembe laini kwa ajili ya ndugu zangu na ninawafanya wema (ninawapendelea ndugu zangu). Lakini kuwapenda kwangu hakuathiri haki ya mtu yeyote. Ninawapa wanachostahili kutokana na mali yangu. Sijafikiria kujihalalisha maliya serikali kwa ajili yangu au mtu mwingine yeyote. Wakati wa Mtume, Abubakr na Umar nilitoa mali nyingi ingawa nilikuwa naipenda na bakhili. Hivi sasa niko ukingoni mwa uhai wangu na nimewaachia watoto na ukoo wangu, makafiriwanaeneza madai ya uzushi dhidi yangu. Hakuna mji uliotozwa kodi kwa ajili ya kufuja mali, bali kwa manufaa ya wananchi, Nina hisa ya moja ya tano, lakini sichukui kitu chochote kwa ajili yangu, inatumiwa na Waislamu wanaostahili. Katika mali ya Mwenyezi Mungu hakuna kinachoibwa wala sichukui kitu. Ninaishi kwa kutegemea kipato changu. 76

Shutuma nyingine aliyotupiwa Khalifa Uthman ni kuchoma moto Qur’an. Dai hili pia sio la kweli. Ukweli ni kuwa Uthman alituma nakala za Qur’an inayotokana na ule msahafu na kuamuru nakala nyingine zote zichomwe moto. alichukua hatua hii kwa sababu zilikuwepo naksi za Qur’an zisizokuwa na mpangilio wa Mtume kwa mujibu wa aya na sura kama Jibrilu alivyomuelekeza Mtume. Baadhi ya nakala zilizokuwa nje ya Madina zilikuwa hazikukamilika. Hali kadhalika miandiko tofauti ilileta tofauti.77 Tofauti nyingine ilikuwa ile ya usomaji. Hivyo ni dhahiri misahafu haikuchomwa na dai hili kama mengine ni la uongo kwani kwa kazi hii Uthman amepewa jina la Jami-ul-Quran (mkusanyaji wa Qur’an).78

Hata kazi ya kupanua eneo la Kaaba, na msikiti wa Madina ililaumiwa. Kazi ya upanuzi wa eneo la Kaaba ilianzwa na umar na uthman aliiendeleza, wenye nyumba za karibu zilizovunjwa walikataa kuchukua fidiya, na kuanza kulalamika. Baadhi ya maswahaba walipinga kutumia fedha za serikali kupanulia msikiti wa Madina na uwanja wa Kaaba. Hata hivyo mnamo mwaka 29 A.H. Uthman aliamua kupanua msikiti wa Madina kwa pesa zake79 magogo ya miti yaliondolewa na kuta zikajengwa kwa matofali. Hebu ona kama sio unafiki na ukafiri kazi ya kurekebisha msikiti na upanuzi wa uwanja wa Kaaba ni vya kulalamikiwa? Tena kwa gharama ya Khalifa mwenyewe. 

Lawama nyingine ambayo ni kuhusu mjomba wa Uthman Hakam Ibn Al-Aas ambae alikuwa akiwatendea vibaya jirani zake na kumcheza shere Mtume. Alihamishwa Madina. Baada ya miaka michache Uthman alimuombea kwa Mtume na baada ya kuombwa mara nyingi Mtume aliahidi kulitazama upya suala hilo. Mtume alipokufa jambo hili lilikuwa halijapatiwa ufumbuzi. Uthman aliwaomba Abubakr na Umar wamrejeshe katika ukhalifa wao, hawakuruhusu. Katika ukhalifa wa uthman alimrudisha mjomba wake baada ya miaka 17 ya kuishi uhamishoni. Hili nalo limefanya la Khalifa kulaumiwa.. 

Haditihi zikavumishwa kuwa khalifa amewanyanyasa baadhi ya maswahaba mfano unaotolewa ni wa Abu Dharr Ghifari, Swahaba huyu alikuwa mchamungu kama maswahaba wengine ila yeye alichukua muelekeo wa kisufi. Kwa imani yake hii alilaumu waliokuwa wanaishi maisha ya kujiweza hasa baada ya watu kupata utajiri kutokana na ngawira. Hali kadhalika alitaka Baitul Mal, pasiwe na salio. Fedha au mali igawiwe na itumike kadiri inavyokuja. alianza kueneza imani yake hii Syria. Gavana wa jimbo la Syria Amir Muawiya alimuandikia Khalifa kumfahamisha juu ya shughuli za Abu Dharr Ghifari. Kahlifa Uthman alimwita Abu Dharr Madina. Abdallah bin Sabaa alijaribu kumuombea alipokuwa syria lakini Gavana Muawiya alimwambia imani anayofundisha ni mpya katika Uislamu na nia yake nikuleta mtafaruku miongoni mwa Waislamu. Abu Zarr (Abu Dharr) alipofika Madina alijadiliana na Khalifa. Khalifa alimuuliza Abu Zarr watu wakishatekeleza wajibu wao mimi nina mamlaka gani ya kuwataka watoe zaidi? Abu Zarr alipoona hakuweza kumbadili Khalifa alikwenda kuishi kijiji cha Rabdhah karibu na Madina na alifia hapo. Wanafik waligeuza maneno na kusema kuwa Abu Zarr alitakiwa aishi kijijini hapo kwa amri ya serikali hivyo alinyanyaswa. Ni dhahiri Khalifa hata kama alifanya hivyo alikuwa sahihi kwa vile ni kweli imani ya Abu Dharr haikuwa ya Kiislamu. Inasemekana pia kuwa maswahaba aliwanyanyasa ni pamoja na Ammar bin Yasir na Abdullah bin Masud. Dai hili ni la uongo kama tulivyoonyesha. Lakini linathibitika zaidi wakati Abu Ammar alipoteuliwa kuwa miongoni mwa wajumbe wa kwenda mikoani kuchunguza matatizo ya magavana. 

Khalifa Uthman anatoka ukoo wa Banu Umayyah wa makureish. Kabla ya kuzaliwa Mtume kulikuwa na kutoelewana baina ya ukoo wa Banu Ummayah na ukoo wa Banu Hashim anaotoka Mtume ambao nao ni wa Kikureish. Wasabai waliwashawishi ukoo wa Hashim kuwa Khalifa anapendelea ukoo wa Banu Ummaya kwa kuwapa nafasi za juu na kuwaondoa madarakani ukoo wa Hashim. 

Dai lingine ambalo halina msingi kama mengine linahusu mashamba ya Serikali ya kuchungia wanyama. Mtume (s.a.w.) alianzisha mashamba ya serikali ya kuchungia wanyama. umar aliongeza mawili. Wakati wa Uthman Farasi na ngamia wa serikali waliongezeka. Kwa sababu hii Khalifa aliongezea mashamba ya kuchungia wanyama ya serikali. Uzushi ukawa Khalifa ameruhusu ukoo wake wa Banu Ummaya uchungie wanyama wao katika shamba la serikali. 

Wingi wa vita ulilazimisha matumizi makubwa ya fedha kwa kuimarisha jeshi kwa kununua zana na vifaa vya jeshi la majini. Pamoja na ngawira iliyokuwa inatumika kwa kuimarisha jeshi. uthman alitumia Zaka na Sadaka kuimarisha ulinzi. Wapinzani wake wakashutumu kuwa, Zaka na Sadaqa zina matumizi yaliyotajwa kwenye Qur’an hivyo haikuwa sahihi kutumia kwa kuimarisha jeshi. Hiki ni kichekesho kwani moja ya matumizi ya Zaka na Sadaqa ni kuimarisha Dini ya Allah. Ulinzi nao huimarisha dini ya Allah. Hata hivyo Khalifa alieleza kuwa alitumia fungu kwa kuliazima na atalirudisha. 

Juu
 

YALIYOMO
  

Tahariri
Fundisho toka Mtambani

Waislamu wataka serikali iwajibike

Serikali yakiri kupokea malalamiko ya Waislamu: Mkapa awataka Watanzania waepuke kubaguana

Mtambani wasema kamwe hawakubali pumbao la kisiasa

Maoni: Kweli ikisimama uongo hujitenga

MARADHI YA KISAIKOLOJIA:  TRANSVESTISM

Mjue Usama bin Ladin

Risala ya Waislamu katika Baraza la Idd  kwa Mgeni Rasmi Rais  Benjamin Mkapa

Wafanyakazi TANESCO waingiwa hofu ya wingu la udini

Hotuba ya Rais Mkapa kwenye Baraza la Idd Diamond Jubilee Jan. 19, 1999

Makala: Hotuba ya Mkapa, Magazeti ya Ruzuku na Waislamu
Na J. Hussein

Kutoka magazeti ya zamani: Washitakiwa walipelelezwa

Hivi siku ya ibada ni ipi?: Ijumaa, Jumamosi au Jumapili?
Na Mwinjilisti Bunga E. Dettu

'Msitarajie kupambana na adui kwa upanga wa Hamza'

Sasa ni kulishwa nguruwe kwa nguvu

Sayansi na Teknolojia
[KUPELEKA  FAX NCHI ZA NG'AMBO BURE!]

Masomo ya Dini ya Kiislamu

Barua za Wasomaji

Mashairi

Chakula na lishe
[Faida na  hasara za kupika chakula]
 


Bonyeza hapa
kushriki mjadala au kutoa maoni juu ya habari hizi na masuala mengineyo ya Kiislamu kwenye Baraza ya Wasomaji

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtanzania.org

 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita