AN-NUUR
Na.185 Shawwal 1419, Januari 22 - 28, 1998
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
Tahariri
Fundisho toka Mtambani


Wakati Bakwata; Taasisi mbalimbali na madhehebu kadhaa zikiandaa Baraza la Eid el Fitr lililokuja kufanyika katika ukumbi wa Diamond Jubelee, Waislamu kupitia kamati yao ya kupigania haki zao ilikuwa ikiandaa Baraza kama hilo katika Msikiti wa Mtambani.

Tofauti na lile la Diamond Jubilee, Baraza la Mtambani lilikabiliwa na vikwazo pamoja na vitisho; ikiwa ni juhudi za kuzuia lisiwepo. Katika juhudi hizi baadhi ya Masheikh na wazee walitumia, vyombo vya habari na hatimaye vyombo vya Dola.

Baadhi ya vyombo vya habari vilitumia ufundi wao kulipaka Baraza la Eid la Mtambani sura ya vurugu na shari hivyo, lisilostahiki kuwepo, kwa upande wake vyombo vya dola vilionyesha makucha yake kwa kutoa kauli ya kupiga marufuku. Lakini kubwa zaidi siku yenyewe ya siku Magari yaliyosheheni askari walikuwa tayari tayari kwa lolote yalitanda eneo la Mtambani ikiwa ni juhudi za mwisho kuzuia Baraza hilo.

Mwenye macho haambiwi tazama. Wenye kazi zao bila shaka washafikisha Salaam:

Katika baraza hilo la Eid wakati Mh.Rais huko Diamond Jubilee, anakariri Waislamu kwamba Suala la Mwembechai halijaisha. Mtambani Waislamu walikuwa wakinoa hisia zao kwa kuleta kumbukizi ya ule unyama waliofanyiwa wa kulengwa risasi kama Swala. "Piga yule" "na yule" "Bado mwongeze". Yote haya yalifanyika kwa amani, ila tu ikachukuliwa ahadi madhubuti ya kusonga mbele katika kupigania na kudai Haki zao.

Kwa mwenye akili iliyofunga na asiyeongozwa kwa chuki atakuwa amejifunza mambo makubwa manne kutokana Baraza hili la Eid la Mtambani.

Kwanza; si vyema kuwachokoza wananchi walioamua kufanya jambo lao kwa amani. Pili, Muislamu akishaushika ukweli na akaweka nia na kuchukua ahadi hakuna wa kumtoa katika ahadi yake hiyo mpaka ije hukumu ya Allah. 

Tatu, kama serikali na kama nchi ni vyema tujiepushe na hatua zinazo vuruga amani kwa kisingizio cha kulinda amani. Ule umati uliokusanyika Mtambani ulishatia nia kwamba swala ile ya Laasiri waliyo swali ndiyo ya Mwisho na ikaombwa dua ndefu kuzikabidhi roho zao kwa Mola wao. Katika hali hiyo Polisi wangewagusa hapana shaka habari yake ingekuwa nzito.

Nane kuwapelekea jeshi watu waliokutana kuzungumzia madhila waliyofanyiwa na polisi ni sawa na kuwakaribisha katika mapambano kwa kuamsha hisia na kumbukumbu zao.

Ilikuwepo haja ya kutumia hekima katika mahali pale ambapo Imamu wake Mzee Chatta bila ya kosa lolote aliwekwa ndani na kuteswa, akatoka akiwa mgonjwa dhaifu na hatimaye kufa muda mfupi tu. Hapa si mahali pa kwenda bila ya hekma. Tushukuru Mungu Salama imepatikana.

Baraza la Eid el Fitr la Mtambani hapana shaka limekuwa la kihistoria. Limedhihirisha kwamba Waislamu ni watu wa amani na wanaweza kulinda amani wasipochokozwa. Na hili liwe fundisho kwa polisi. 

Juu
 

YALIYOMO
 

Tahariri
Fundisho toka Mtambani

Waislamu wataka serikali iwajibike

Serikali yakiri kupokea malalamiko ya Waislamu: Mkapa awataka Watanzania waepuke kubaguana

Mtambani wasema kamwe hawakubali pumbao la kisiasa

Maoni: Kweli ikisimama uongo hujitenga

MARADHI YA KISAIKOLOJIA:  TRANSVESTISM

Mjue Usama bin Ladin

Risala ya Waislamu katika Baraza la Idd  kwa Mgeni Rasmi Rais  Benjamin Mkapa

Wafanyakazi TANESCO waingiwa hofu ya wingu la udini

Hotuba ya Rais Mkapa kwenye Baraza la Idd Diamond Jubilee Jan. 19, 1999

Makala: Hotuba ya Mkapa, Magazeti ya Ruzuku na Waislamu
Na J. Hussein

Kutoka magazeti ya zamani: Washitakiwa walipelelezwa

Hivi siku ya ibada ni ipi?: Ijumaa, Jumamosi au Jumapili?
Na Mwinjilisti Bunga E. Dettu

'Msitarajie kupambana na adui kwa upanga wa Hamza'

Sasa ni kulishwa nguruwe kwa nguvu

Sayansi na Teknolojia
[KUPELEKA  FAX NCHI ZA NG'AMBO BURE!]

Masomo ya Dini ya Kiislamu

Barua za Wasomaji

Mashairi

Chakula na lishe
[Faida na  hasara za kupika chakula]
 


Bonyeza hapa
kushriki mjadala au kutoa maoni juu ya habari hizi na masuala mengineyo ya Kiislamu kwenye Baraza ya Wasomaji

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtanzania.org

 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita