|
Na.185 Shawwal 1419, Januari 22 - 28, 1998 |
| Mtambani
wasema kamwe hawakubali pumbao la kisiasa
FFU watinga na kuondoka patupu MAPEMA wiki hii historia ya nchi hii nusura igubikwe na doa jingine sawa na lile la Mwembechai, kufuatia jaribio la s zilipandisha mori na hisia kwa waumini hao ambapo imamu aliyesalisha Swala ya laasiri aliwataka waichukulie swala hiyo kuwa ni ya mwisho kabla ya mapambano kuanza ambayo yangeamua hali yao ya baadaye. "Ilikuwa kama majogoo yanayoangaliana kwa hasira na kisasi kabla ya kurukiana, mimi nilishangaa kama polisi wangelivamia basi ama ningekutwa gerezani, mochuari au hospitali", amedai kijana mmoja aliyetokea maeneo ya Mwananyamala. Kadri muda ulivyozidi kusonga mbele ndivyo waumini walivyozidi kumiminika mahali hapo. Katika hatua za awali za kutaka kuzuia Baraza hilo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Alfred Gewe inasemekana alifika Msikitini hapo na kutaka kuongea na Imamu. Hata hivyo, ilibidi aondoke kuepusha shari baada ya kujibiwa kwamba Mtambani hakuna Imamu kwani Imamu wake Mzee Chatta alishauliwa. Baadae aliwasili mkuu wa upelelezi wa mkoa (RSO) akiwa amevalia kanzu na kofia ambapo baada ya mazungumzo na Alhaj Hanzuruni Mungula, aliwaamuru polisi waondoke. AN-NUUR ilishuhudia mabasi madogo aina ya DCM yapatayo sita yakiwasili na kuteremsha waumini waliobeba mabango yanayoonyesha mahali wanapotokea. Akiwa katika harakati za kufuatilia kila tukio lililotokea mahali hapo, mwandishi alivamiwa na vijana watatu huku mmoja wapo uso ukiwa umezibwa na kitambaa cheupe kilichoachia sehemu ya macho tu. Vijana hao walimshuku mwandishi kuwa huenda ni mmoja wa "watafuta habari wa serikali.". Walimuamuru atulie mahali pamoja vinginevyo wangelimchukulia hatua. Hata hivyo jitihada za kujitambulisha zilifanikiwa kuwashawishi vijana hao ambao walionekana wako tayari kwa lolote. Kila aliyefika eneo hilo na kusimama kando alifuatiliwa na vijana hao kwa siri au kwa uwazi. Makachero waliofika mahali hapo walikuwa na wakati mgumu kimajukumu kutokana na ulinzi wa "para military" hao. Wakati wa onesho la mkanda wa Mauaji ya Mwembechai ulipowadia watu wote waliokuwa eneo hilo ikiwa ni pamoja na wakazi walio nyumba za jirani na msikiti huo walishonana mahali hapo kiasi cha kukanyagana. Waumini wengine walijazana juu ya jengo la msikiti linaloendelea kujengwa. Mkanda huo ulionekana kuvuta hisia za wengi hasa pale mmoja wa mapolisi walikuwa katika operesheni hiyo alipokuwa amelala chini akimlenga kijana mmoja ambaye baadaye alimfyatulia risasi na kumuua papo hapo. Sehemu nyingine iliyoamsha masikitiko ni pale polisi mmoja alipoamrisha "piga yule, mwongeze tena." Viongozi wa kamati iliyoandaa baraza hilo walifanya kazi ya ziada kuwanasihi waumini waliokuwa wakiangalia onesho hilo ili kuwatuliza kutokana na yale waliyokuwa wakiyashuhudia katika onesho hilo. "Haya ni yale yale ya Soweto wakati wa ubaguzi wa rangi Afrika kusini, alisema muumini mmoja aliyeonekana kujawa na hasira baada ya kuangalia mkanda huo. Hadi mwandishi anaondoka eneo hilo hapakuwa na tukio lolote lililoashiria kuvurugika kwa amani ukiondoa vitisho vya magari sita yaliyokuwa yakiranda eneo hilo kabla ya shughuli hiyo kuanza. |
YALIYOMO
Tahariri
Waislamu wataka serikali iwajibike Serikali yakiri kupokea malalamiko ya Waislamu: Mkapa awataka Watanzania waepuke kubaguana Mtambani wasema kamwe hawakubali pumbao la kisiasa Maoni: Kweli ikisimama uongo hujitenga MARADHI YA KISAIKOLOJIA: TRANSVESTISM Risala ya Waislamu katika Baraza la Idd kwa Mgeni Rasmi Rais Benjamin Mkapa Wafanyakazi TANESCO waingiwa hofu ya wingu la udini Hotuba ya Rais Mkapa kwenye Baraza la Idd Diamond Jubilee Jan. 19, 1999 Makala: Hotuba ya Mkapa, Magazeti
ya Ruzuku na Waislamu
Kutoka magazeti ya zamani: Washitakiwa walipelelezwa Hivi siku ya ibada ni ipi?: Ijumaa,
Jumamosi au Jumapili?
'Msitarajie kupambana na adui kwa upanga wa Hamza' Sasa ni kulishwa nguruwe kwa nguvu Sayansi na Teknolojia
Chakula na lishe
|