AN-NUUR
Na.185 Shawwal 1419, Januari 22 - 28, 1998
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
Faida na hasara za kupika chakula
 

Na Mujahid Mwinyimvua

Sanaa ya kupika chakula kwa matumizi ya binadamu ni dhana kongwe katika historia ya mwanadamu. Sanaa hii inafaida na vile vile ina hasara. Ni makusudio ya makala hii kuziweka wazi faida na hasara hizo, na hatimae kutoa mapendekezo ya namna ya kupunguza hasara hizo.

Tukianza na faida; sanaa ya kupika chakula inafaida kadhaa, baadhi yake ni hizi.

Kwanza, kupika chakula kunasaidia kuua vijidudu vinavyoweza kuambukiza maradhi. Kwa kawaida, vyakula vibichi huwa na vijududu ambavyo vinaweza kuambukiza maradhi. Mfano wa vijidudu hivyo ni kama vile: Salmonella typhi, ambavyo husababisha ugonjwa wa homa ya matumbo (Typhoid fever); na Vibrio cholerae ambavyo husababisha ugonjwa wa kipindupindu (Cholera).

Ni vyema pia hapa tukakumbuka kuwa, chakula kilichopikwa na kupoa kinaweza kuingiwa na vijidudu vyenye kuambukiza magonjwa. Kwa hiyo, chakula kilichopoa lazima kipashwe moto tena kabla ya kuliwa.

Pili, kupika chakula kunasaidia chakula kuwa laini na kuweza kusagwa kwaurahisi tumboni.

Tatu, kupika chakula kunasaidia kuongeza utamu (radha) wa chakula. Kwa hiyo, mtuanaweza kula chakula cha kutosha.

Nne, kwa vile kupika chakula kunaua vijidudu na vimengenyo (enzymes), chakula kilichopikwa kinaweza kukaa kwa siku kadhaa bila ya kuharibika.

Tano, kupika kunapunguza kiasi cha sumu inayoweza kuiwemo katika chakula hicho. Kwa kawaida baadhi ya vyakula huwa na sumu. Kwa mfano, mihogo ambayo ni michungu huwa na sumu inayoitwa cyanide. Sumu hiyo, hasa kwenye kisamvu (majani ya mti wa mu hogo) hupungua kama kisamvu kitapikwa kwamuda wa kutosha.

Hata hivyo, ikumbukwe kuwa sumu nyingine hazipungui kwa kupikwa.Jambo lakufanyakwa nyumbani ni kuacha chakula hicho.

Licha ya faida hizo; sanaa ya kupika chakula inahasara zake. Hapa tutatazama hasara mbili.

Hasara ya kwanza, kupika chakula kunaweza kusababisha upotevu wa virutubisho, hasa vitamini.

Hasara ya pili, baadhi ya vyakula kama vile mafuta (fats/oils) yanayotumika kupika vyakula kwanjia ya kukaanga (flying) yanaweza kuunguana ku toa vitu ambavyo ni sumu.

Baada ya kuona baadhi ya faida hasara za kupika chakula, vyema sasa nikamilishe makala hii kwa kutoa ushauri ufuatao:

Sanaa ya kupika vyakula ina faida nyingi kuliko hasara zake. Kwa hiyo lazima tupike vyakula vyetu. hata hivyo, vyakula hasa vyenye vitamini kama vile mboga mboga tusivipike kwa mudamrefu. Vile vile, vyombo (Sifuria) vya shaba zisitumike kupikia mboga mbonga namatunda. Pia vyombo vya kupikia lazima vifunikwe; na maji yaliyotumika kupikia ni vyema ya katumika kama supu na wala yasimwagwe. Zaidi ya hayo, mafuta yaliyofunika kukaangia (flying) vya kula yasitumike tena.
 

Juu
 

YALIYOMO
 

Tahariri
Fundisho toka Mtambani

Waislamu wataka serikali iwajibike

Serikali yakiri kupokea malalamiko ya Waislamu: Mkapa awataka Watanzania waepuke kubaguana

Mtambani wasema kamwe hawakubali pumbao la kisiasa

Maoni: Kweli ikisimama uongo hujitenga

MARADHI YA KISAIKOLOJIA:  TRANSVESTISM

Mjue Usama bin Ladin

Risala ya Waislamu katika Baraza la Idd  kwa Mgeni Rasmi Rais  Benjamin Mkapa

Wafanyakazi TANESCO waingiwa hofu ya wingu la udini

Hotuba ya Rais Mkapa kwenye Baraza la Idd Diamond Jubilee Jan. 19, 1999

Makala: Hotuba ya Mkapa, Magazeti ya Ruzuku na Waislamu
Na J. Hussein

Kutoka magazeti ya zamani: Washitakiwa walipelelezwa

Hivi siku ya ibada ni ipi?: Ijumaa, Jumamosi au Jumapili?
Na Mwinjilisti Bunga E. Dettu

'Msitarajie kupambana na adui kwa upanga wa Hamza'

Sasa ni kulishwa nguruwe kwa nguvu

Sayansi na Teknolojia
[KUPELEKA  FAX NCHI ZA NG'AMBO BURE!]

Masomo ya Dini ya Kiislamu

Barua za Wasomaji

Mashairi

Chakula na lishe
[Faida na  hasara za kupika chakula]
  


Bonyeza hapa
kushriki mjadala au kutoa maoni juu ya habari hizi na masuala mengineyo ya Kiislamu kwenye Baraza ya Wasomaji

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtanzania.org

 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita