|
Na.185 Shawwal 1419, Januari 22 - 28, 1998 |
|
Salamu za Edd-El-Fitr kutoka DAMUSA
Ndugu Mhariri HIVI karibuni ubaguzi na dhuluma dhidi ya Waislamu unaofanywa na Serikali na taasisi zake umeonekana dhahiri pale ambapo wanafunzi walitakiwa kufanya mitihani ya kidato cha nne ndani ya sikukuu ya Idd-e-Fitr. Wizara ya Elimu inasema kuwa matokeo ya darasa la saba yalicheleweshwa kwa sababu vijana wa kikristo waweze kusherehekea vizuri Christmas Tunawashukuru wazee wetu kwa kulipigia kelele hili na hatimaye ratiba ikabadilishwa. Lakini hata hivyo tunapenda kuwakumbusha wazee wetu kuwa kazi iliyo mbele yetu ni kubwa. Karibuni tumesoma katika magazeti kwamba mlialikwa "FUTARI ZA NGUVU" kwa waheshimwa. Hatukufahamu kama mlipata fursa ya kuwakumbusha juu ya matibabu ya Chuki Athumani (nje ya nchi) aliyepigwa risasi na polisi, na haja ya wale waliofanya udhalimu huu na kuua kufikishwa kwenye vyombo vya sheria. Bado wanafunzi wa Kiislamu wanaendelea kunyanyaswa na wakuu wa shule wanazosoma katika masuala ya "HIJABU" na "SWALA YA IJUMAA". Wale wanaovaa "HIJABU" hudhihakiwa kwa kupachikwa majina kama vile Mujahidina n.k. Wale wanaotaka kuvaa hupata vitisho, na ipo mifano mingi ya shule za msingi, sekondari na vyuo. Pia, bado baadhi ya mashule na vyuo ufugaji wa nguruwe unaendelea. Kwa hiyo kwa kupitia salamu hizi tunawakumbusha Waislamu kwamba harakati za kuondosha madhila yanayotukabili hazijesha, kwa hiyo funga zetu hizi zinapaswa kuchochea harakati hizi. Tunawasihi wapenda amani wote wakemee dhulma hizi dhidi yavijana wa Kiislamu, na wale wenye kusimamia ukandamizaji huu pia waache kwa manufaa yawote kwa sababudhulma ikiendelea hakutakuwepo na njia nyingine bali kusimama kidete kupambana na dhulma hii; na mara zote dhalimu (mdhulumaji) hushindwa. Mwisho tunawasihi ndugu zetu wanaofanya mitihani, wafanye bidii wakizingatia mazingira wanayofanyia mitihani hii. Tunawatakia kila lakheri katika mitihani yao na Idd njema na Waislamu wote kwa ujumla. Wabillah Tawfiq,
Kuanzishwa kwa gazeti na radio, historia kujirudia? Ndugu Mhariri NIMEFARIJIKA niliposoma kwenye ANNUUR Na. 184 kuhusu BAKWATA kuwa na mpango wa kuanzisha gazeti lake (miezi michache ijayo) na Radio yenye kurusha masafa takriban maili 15. Mpango huo unadhihirisha kuwa kumbe BAKWATA ina wenye kufanya mambo makubwa ya kuendeleza Uislamu na Waislamu. Wito umetolewa kwa Waislamu au taasisi yoyote kuanzisha jarida au Radio na mambo mengine ya kuendeleza Uislamu katika nyanja ya kuelimisha umma unastahiki kuungwa mkono wa Waislamu wote. Lakini kama vyombo vya habari hivyo (Mass Media) vitatumika kinyume kama kuleta propaganda, kuvuruga maadili na kutangaza mambo ya laghawi (upuuzi) vitakuwa havina maana ya kuwepo. Historia ni jambo la kujirudia, isije kuwa kuanzishwa kwa jarida na Radio ikajirudia historia ya kuvunjwa kwa jumuiya ya Afrika Mashariki (EAMWS) mwaka 1968. EAMWS haikuvunjwa ila baada ya kuundwa jumuiya iliyo chukua nafasi. Wakati BAKWATA ina mpango wa kuanzisha gazeti na Radio, tayari kuna Waislamu wameanzisha na wanatarajia kufungua Radio Insha-Allah. Kwa kuwa Bakwata imetoa wito kwa Waislamu kuanzisha vyombo vya habari, naishauri iepuke dhana ya kila kitu kupa fikiria kwamba kwa muda mrefu sasa hakuna anayejali juu ya upotofu unaoenezwa na wale waliokwisha amua kuufanya upotofu ndio sera zao za manisha. Inaonyesha kana kwamba wote tumekubali kupotolewa na waharibifu hawa na kwamba wanavyofanya ni haki yao na ndio ndivyo. Hivi kweli muuza pombe ya "Chibuku" au "tiger beer" atangaze ulevi wake kwa kupitia mgongo wa sikukuu ya Idi Fitri, kwa kisingizio cha salamu za mkono wa Idi. Hivi tunahaja ya kusalimiwa na kutakiwa heri na walevi mafasiki na waharibifu hawa. Hakuna salama wala heri yoyote wanayotutakia sisi, isipokuwa balaa la ulevi na walevi katika jamii. Ni kashfa, na kejelii siyokifani kwa imani ya Kiislamu, ikatazayo ulevi na pombe zote, kwamba itumike sikukuu yetu kutangazia ufuska uharibifu na upotofu wa wauza pombe. Natoa ombi kwa jumuia zote za Kiislamu tusiikubali kashfa hii na tuipige vita ife mara moja. Lazima tuchukue hatua kali kukomesha uhuni na upuuzi huu. Ukitazama gazeti la Mtanzania toleo 925 la Jumatano, Januari 20, 1999 kuna matangazo ya pombe ya Chibuku na Tiger beer, wamediriki hata kuweka alama zetu za mwezi na nyota katika matangazo hayo. Kejeli isiyovumilika. Kama wapo akina Juma na Asumani walevi hao sio Waislamu. Hawi mtu Muislamu kwa sababu ya jina lake tu, Uislamu ni imani na matendo. Ninapendekeza kwamba kuanzia sasa yeyote atakaefanya kashfa na kejeli ya aina hii, ashtakiwe huyo mtangazaji na gazetil ililopokea tangazo hilo pamoja na redio na Station za TV zitangazazo pombe kwa kuinasibisha na sherehe za Waislamu. Hatua na za aina hii pia zichukuliwe kwa vikundi vya muziki wa dansi na taarabu. Watangaze, wasizihusishe na Uislamu. Hakuna Idi inayosherehekewa kwa ulevi, wala dansi,wala taarabu, wala ngoma.Wanaofanya hivyo ni mafasiki, wapotofu, waharibifu wasiojua Uislamu na sherehe na tafrija zake. Waislamu tushikamane juu ya hilo tusichezewe na Shetani na vikaragosi vyake. Tulinde dini yetu. Wabillahi Taufiki
Kilio cha Padri Luambano kujirudia 1999? Ndugu Mhariri TAKRIBAN mwaka mmoja tangu mheshimiwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Lutani Makamba kuitikia wito wa Padri Luambano. Aliyoyafanya Makamba hiyo Februari 1998 yameweka historia mpya ya maisha ya Waislamu Tanzania. Kwa mara ya kwanza wameuliwa kwa amri ya baadhi ya viongozi wa serikali yao. Katika gazeti la Mtanzania toleo la tarehe 13/01/1999 Bw. Abel Ngapenda amemtaka Mheshimiwa Makamba adhibiti vikundi vya dini vinavyohubiri katika viwanja vya wazi, ukiondoa viwanja vya Jangwani. Nionavyo mimi ni kwamba, uanajeshi wa Makamba ni mzuri sana, isipokuwa naiomba serikali na wapambe wote wanaohujumu kutangazwa kwa dini hii ya Kiislamu wawe na fikra za nini kitakachotokea. Hali ni mbaya. Kwa Waislamu, hizi kambi za hawa mabwana hazitakiwi kuachwa hivi hivi, lazima tuwe macho nazo, wenzetu wanasikilizwa tena mno. Waislamu sisi ni wapweke hatuna pa kusemea. Kwa wale wenye kufikiri, tukio la Mwembechai wataona kwamba; Waislamu wameamka kiasi fulani. Utakapoongelea masuala ya Uislamu hapa Tanzania basi sura kubwa itakayokujia ni ile ya Mwembechai. Waislamu wameshajua hasa msimamo wa nchi isiyo na dini wanavyoonewa, hawatendewi haki, hapana usawa na thaamani ya Muislamu ilivyoshushuwa na jingine zaidi wanafiki wameonekana. Namshukuru Mwenyezi Mungu, tunaona mshikamano madhubuti kabisa wa akina mama tena Tanzania nzima hongereni na Allah (s.w.) atawalipeni. Makongamano na mikusanyiko ya Kiislamu imeongezeka. Hatuna kingine zaidi ya mshikamano ili kuondoa hii dhuluma na hawa madhalimu, wanaosubiriwa kuzomewa ndio wajisahihishe. Mahubiri yaendelea sio Misikitini tu bali hata kwenye viwanja vya wazi mahubiri ya Kiislamu sio sawa na ya Kikristo na dini nyinginezo. "Sisi dini yetu nanyi dini yenu". Mama Hijari,
|
YALIYOMO
Tahariri
Waislamu wataka serikali iwajibike Serikali yakiri kupokea malalamiko ya Waislamu: Mkapa awataka Watanzania waepuke kubaguana Mtambani wasema kamwe hawakubali pumbao la kisiasa Maoni: Kweli ikisimama uongo hujitenga MARADHI YA KISAIKOLOJIA: TRANSVESTISM Risala ya Waislamu katika Baraza la Idd kwa Mgeni Rasmi Rais Benjamin Mkapa Wafanyakazi TANESCO waingiwa hofu ya wingu la udini Hotuba ya Rais Mkapa kwenye Baraza la Idd Diamond Jubilee Jan. 19, 1999 Makala: Hotuba ya Mkapa, Magazeti
ya Ruzuku na Waislamu
Kutoka magazeti ya zamani: Washitakiwa walipelelezwa Hivi siku ya ibada ni ipi?: Ijumaa,
Jumamosi au Jumapili?
'Msitarajie kupambana na adui kwa upanga wa Hamza' Sasa ni kulishwa nguruwe kwa nguvu Sayansi na Teknolojia
Chakula na lishe
|