AN-NUUR
Na.185 Shawwal 1419, Januari 22 - 28, 1998
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
MARADHI YA KISAIKOLOJIA:

TRANSVESTISM


WIKI iliyopita tuliyachambua maradhi yaitwayo Transsexualism, yaani kichaa cha mtu kupenda kuwa na silka au umbile la mtu wa jinsia tofauti na yeye, kwa mfano mwanaume kuwa na shauku ya kupata silka au umbile la kike, au mwanamke kuwa na shauku ya kupata silka au umbo la kiume.

Leo tuangalie maradhi mengine yaitwayo Transvestism. Haya ni maradhi au kichaa cha mtu kupendelea mavazi au mapambo ya watu wa jinsia nyingine. Maradhi haya hurandana sana na yale ya Transsexualism, lakini wengi pia hupenda kujipamba kwa vipambo vya watu wa jinsia nyingine bila ya wao kuwa na silka za watu hao. Haya ni maradhi ya mwanaume kupenda kuvaa nguo au mapambo ya kike, au mwanamke kupenda kuvaa nguo za kiume. Mwenye maradhi haya huitwa Transvestite. (Husomwa Transevestait) 

Wenye maradhi haya walio wengi ni wanawake, hawa wale tuliowaelezea katika toleo lililopita kuwa wameielewa vibaya dhana ya "usawa". Ni nadra kumkuta mwanaume amevaa sketi na blauzi, lakini siku hizi tunawaona wanaume waliotoboa masikio na kuvaa hereni, na wengine huacha vifua wazi ili mikufu yao ya dhahabu ionekane. 

Wagonjwa wengi wenye maradhi haya wako kule Ulaya na Marekani. Wagonjwa walio huku kwetu mara nyingi huambukizwa maradhi haya kwa kupitia Mavazi mapachiko (Programmed Mind) kwamba chochote wanachokifanya watu wa Ulaya na Marekani ndiyo maendeleo, kwa hiyo vijana huiga yanayoonekana kwenye televisheni hata kama yanafanywa na wanaume mashoga. Hivyo, Trasvestite wengi wa humu kwetu huwa na maradhi mengine yanayoitwa Copycatism, ugonjwa wa kuiga bila ya kuelewa maana ya kinachoigwa. 

Wagonjwa wa kike wa maradhi haya mara nyingi huwa na michanganyiko ya maradhi. Mwanamke anayevaa nguo za kiume, hasa makaptula au suruali na shati, mara nyingi huwa na maradhi ya Sexual Sadium, kwa kupenda wanaume wahemkwe kwa umbile lake popote anapopita, kwa vile huziacha wazi sehemu zake za mvuto. Pili, mgonjwa huyu wa kike pia yawezekana kuwa ameathirika na wazo mpachiko la kuwa "sawa" na wanaume, kwa hiyo labda yeye ni Transsexual, na tatu inawezekana kuwa ni miongoni mwa malimbukeni ambao wako ndani ya hali ya kuchanganyikiwa kiasi cha kutojielewa afuate mila gani (Identity Crisis) na ndipo wanaishia kuwa Copycats kila siku wanaangalia Mzungu kavaaje ili na yeye avae hivyo. Kwa hiyo siku Mzungu akivaa gunia basi na yeye unaweza kumkuta mitaa ya Tandale akichagua magunia matupu akashone vazi aliloliona kwenye kabati la picha (tv). Wagonjwa wengine hurithishwa tabia ya kuvaa kiume tangu wadogo, hivyo wazazi malimbukeni huchangia sana katika kutengeneza jamii ya ma-Transvetite. Mara nyingi watoto wa kike tu ndio huzoeshwa kuvaa mavazi ya kiume, lakini sijapata kuona watoto wa kiume(waliofikia umri wa kukimbia) wakivalishwa vigauni au wakatogwa masikio. 

Wanaoshangaza zaidi ni wale wagonjwa wa kiume wanaotoga masikio na kuvaa hereni na vidani. Hawa nao huenda ni Transsexuals, wana shauku ya kuwa wanawake, ila tu kwa bahati mbaya huku kwetu hakuna hospitali za kufanyia operesheni, pengine wangependa kubadilishwa viungo vyao vya mwili vinavyowafanya wanaume. Kama sio madume jike (transsexuals) basi ni malimbukeni waliopapia miji. Au wako kwenye vurugu la mawazo ua kujitambua (identity crisis). Au pengine labda ameona wanawake wamependelewa kwa kuachiwa wapendeze peke yao, kwa hiyo na yeye anataka apendeze kama dada zake, au mabinti wa jirani. Cha kumuuliza ni: Unataka upendeze kama akina dada ili iweje? Halafu ukishapendeza watu wakikupenda, wafanyeje? Labda walete posa! 

Uislamu umechukua zaidi tahadhari kwa wanawake Waislamu wasije wakawaiga majahili katika kujipamba, kwa kuwaambia: 

"... Wala msijipambe kujipamba kwa majahili waliopita (yaani msiwaige majahili)" (33:33). 

Huyu Transvestite wa kiume sijaipata aya yake, nadhani haipo kwa sababu, labda haitegemewi kabisa mwanaume kujifananisha na mke au kuvaa kike. Lakini Abu Hurairah amesema kwamba Mtume Muhammad (s.a.w.) amewalaani wanaume wanaovaa mavazi ya kike na wanawake wanaovaa mavazi ya kiume. (Abu Daud).
 

Juu
 

YALIYOMO
 

Tahariri
Fundisho toka Mtambani

Waislamu wataka serikali iwajibike

Serikali yakiri kupokea malalamiko ya Waislamu: Mkapa awataka Watanzania waepuke kubaguana

Mtambani wasema kamwe hawakubali pumbao la kisiasa

Maoni: Kweli ikisimama uongo hujitenga

MARADHI YA KISAIKOLOJIA:  TRANSVESTISM

Mjue Usama bin Ladin

Risala ya Waislamu katika Baraza la Idd  kwa Mgeni Rasmi Rais  Benjamin Mkapa

Wafanyakazi TANESCO waingiwa hofu ya wingu la udini

Hotuba ya Rais Mkapa kwenye Baraza la Idd Diamond Jubilee Jan. 19, 1999

Makala: Hotuba ya Mkapa, Magazeti ya Ruzuku na Waislamu
Na J. Hussein

Kutoka magazeti ya zamani: Washitakiwa walipelelezwa

Hivi siku ya ibada ni ipi?: Ijumaa, Jumamosi au Jumapili?
Na Mwinjilisti Bunga E. Dettu

'Msitarajie kupambana na adui kwa upanga wa Hamza'

Sasa ni kulishwa nguruwe kwa nguvu

Sayansi na Teknolojia
[KUPELEKA  FAX NCHI ZA NG'AMBO BURE!]

Masomo ya Dini ya Kiislamu

Barua za Wasomaji

Mashairi

Chakula na lishe
[Faida na  hasara za kupika chakula]
  


Bonyeza hapa
kushriki mjadala au kutoa maoni juu ya habari hizi na masuala mengineyo ya Kiislamu kwenye Baraza ya Wasomaji

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtanzania.org

 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita