AN-NUUR
Na.185 Shawwal 1419, Januari 22 - 28, 1998
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
Mjue Usama bin Ladin

Wiki hii, alhamdulillah, tunakuleteeni mahojiano yaliyofanywa kwa mwanaharakati wa Kiislamu ambaye anadaiwa kuwa ni gaidi hatari sana na ambaye kwa muda mrefu sasa amekuwa ‘akimchezesha kwata’ polisi wa ulimwengu aliyejilimbikizia nguvu za kijeshi na za kiuchumi - Marekani. Mahojiano haya yalichapishwa katika gazeti la Nida’ul Islam Toleo la 15, Oktoba - Novemba 1996. (http://www.islam.org.au) 

Jina: Usama Bin Mohammad Bin Ladin.

Historia yake kwa Ufupi

Amezaliwa katika mji wa Riyadh, Saud Arabia, mwaka wa Kiislam 1377AH, sawa na mwaka 1957. Amekulia katikia miji ya Al Madina Al Munawwara na Hijaz, na alianza kupata elimu katika shule za Jeddah, na kisha alijiunga na Chuo Kikuu cha King Abdul Aziz huko huko Jeddah ambapo alisomea Uongozi na Uchumi. Ameoa na ana watoto. 

Bw. Usama ni mtu anayejitahidi sana kufuata Sunna kwa ujumla wake na kwa vipengele vyake kama zilivyosimuliwa na wapokezi mashuhuri [wa Hadithi za Mtume Muhammad (s.a.w.)]. 

Kutokana na jitihada yake hii ya kufuata Sunna ametokea kuiona haja ya kuwepo kwa Da’awah -kuwafikishia watu wote ujumbe mwanzo wa Jihad nchini Afghanistan. Mwanzoni mwa miaka ya 1980 alishiriki na Mujahidina kupigana dhidi ya Chama cha Kikomunisti nchini Yemen ya Kusini, na akashiriki kwa mara nyingine tena katika miaka ya 1990 hadi chama hicho kiliposhidwa. 

Bw. Usama, kwa kusaidiana na Sheikh Dk. Abdullah Azzam - Mwenyezi Mungu amrehemu - alianzisha ofisi ya huduma kwa Mujahidina katika mji wa Peshawar; pia kwa kusaidiana na Sheikh Azzam, alianzisha Kambi ya Sidda ili kutoa mafunzo kwa Mujahidina wa Kiarabu walioingia Afghanistan kupigana Jihad. 

Safari yake ya kwanza kwenda kuwasidia Mujahidina wa Afghanistan ilikuwa ni siku chache tu baada ya Warusi kujiingiza Afghanistan, mwaka 1399AH (1979). Alianzisha "Ma’sadat AlAnsar" ambayo ilkuwa ni kambi [ya kijeshi] ya Mujahidina wa Kiarabu huko Afghanistan. 

Bw. Usama alihama toka Peninsula Arabuni tarehe 16 Shawwal 1414AH (1991). Baadaye alitakiwa na serikali ya Saudia arejee nyumbani, hata hivyo alikataa na serikali hiyo ikaufuta uraia wa Bw. Usama [katika nchi hiyo], ikaifuta pasi yake ya kusafiria (passport), ikazizuia mali zake na baada ya yote hayo serikali ya Kifalme ya Saudia ilianza kampeni ya kumtangaza vibaya - ndani na nje ya nchi hiyo. 

Hivi sasa Bw. Usama anaishi [uhamishoni] nchini Afghanistan na ametoa wito kwa Waislamu ulimwenguni kote kutangaza Jihad dhidi ya ushirika wa Wayahudi na Wakristu ambao kwa nguvu unaikalia ardhi takatifu ya Palesina na Peninsula Arabuni. 

Mahojiano

Swali: 

[Unadahani] Ni sera ipi inafaa kufuatwa na wanaharakati wa Kiislamu kuhusiana na wanazuoni ambao wanautetea, ima kwa kukusudia au la, utawala wa [Kifalme wa] Saudia?

Jibu:

Ni ukweli usiofichika kuwa tawala katika nchi za kiarabu zinategemea taasisi kadhaa ili kujilinda. Miongoni mwa taasisi hizi ni idara ya usalama wa taifa. Tawala hizi hutumia fedha nyingi kwa ajili ya idara hii, na shughuli yake kuu ni kuwapeleleza watu wa nchi husika ili kumlinda mtawala hata kama kufanya hivyo kutapelekea kuvunja haki za raia na [kuhatarisha] usalama wao. Aidha lipo jeshi ambalo huwa limetayarishwa kuwashambulia raia ikiwa raia hao wataonyesha kuupinga uonevu huo na kutaka kuondoa ukandamizaji na [ili] kusimamisha haki. 

Sekta ya vyombo vya habari [nayo] ipo katika kundi hilo hilo [la kuwalinda watawala] kwa vile [vyombo hivyo] hufanya kazi ya kuwapamba watawala kwa sifa nzuri nzuri; kuipumbaza jamii, na kusaidia kufanikisha mipango (njama) za maadui kwa kuwashughulisha raia [wasikilizaji, wasomaji na watazanmaji wa TV] na mambo madogo madogo [yasiyo ya msingi] na pia kutibua hamasa, jazba na matamanio ya wananchi hao kiasi kuwezesha mambo maovu kuenea miongoni mwa waumini. 

Pia ipo taasisi nyingine ambayo imepata kipaumbele mongoni mwa viongozi wa nchi za kiarabu, na hutumika kuwapotosha watu na hivyo kuvirahisihia vyombo vya usalama kutekeleza majukumu yake niliyotangulia kuyataja. Taasisi hii ni kundi la wanazuoni ambao wapo chini ya Watawala, na kazi yake ndiyo ya hatari kuliko taasisi zote katika nchi za Kiarabu. Historia inatuonyesha ushahidi mzuri zaidi juu ya ukweli huu. 

Wakati ambapo watawala hawa wanajiingiza katika mambo ya ukafiri mkubwa [kumuasi Mwenyezi Mungu waziwazi] na tena mbele ya watu wote, bado utakuta taasisi ya kidini inatoa Fatwa [kuonyesha kuwa watawala hao wapo sawa sawa]. Kazi ya taasisi ya kidini katika nchi hii [Saudia] yenye misikiti miwili mitakatifu ndiyo kazi mbaya zaidi. Bila kujali kuwa taasisi hiyo inafanya hivyo kwa kukusudia au la, madhara yatokanayo na kazi yake hiyo hayana tofauti na yale yatokayo kwa adui mkubwa wa taifa hili. 

Utawala huu katika ardhi iliyo na misikiti miwili mitakatifu imetoa nafasi [mamlaka ] kubwa kwa taasisi hii [ ya wanazuoni], na imeweza kuikweza mbele ya watu kiasi cha kufanywa kitu cha kuabudiwa mbali na Mwenyezi Mungu miongoni mwa watu wa kawaida, na pia bila ridhaa ya waliomo katika taasisi hii. 

Hata hivyo, kumeendelea kuwepo katika ardhi hii ya misikiti miwili mitakatifu - tunamshukuru Mwenyezi Mungu- idadi nzuri ya wanazuoni na wanafunzi waaminifu [wacha-Mungu] ambao hufanya kazi zao kwa mujibu wa mafundisho, na wale ambao wameonyesha msimamo thabiti dhidi ya vitendo vya kikafiri ambavyo vinaendelezwa na serikali. Serikali imekuwa ikifanya kila namna kuwazuilia wanazuoni hawa [waadilifu] wasiwe huru kwa wananchi. Aliyetangulia kwa wanazuoni [waadilifu] alikuwa Sheikh Abdullah bin Hamid - tunamuomba Mwenyezi Mungu amrehemu - ambaye alikuwa ni Mufti wa Peninsula ya Arabuni, na ambaye aliliongoza Baraza Kuu la Majaji. Hata hivyo, serikali ilimbana sana na kumtia misukosuko mpala akalazimika kujiuzulu. Sheikh huyu alipata kuandika maandiko mengi na yalipata umaarufu kuhusiana na sheria ambazo ni kinyume cha maamrisho ya Allah ambazo serikali ilizipitisha badala ya sheria ya Allah, na katika hizi ni "treatise" (mikataba) inayoshughulika masuala ya kazi na wafanyakazi ambapo sheria nyingi ndani yake zinapingana na sheria ya Allah (s.w.t). 

Wakati huo huo serikali ikawapandisha vyeo wanazuoni ambao kielimu [wao] ni chini ya Sheikh Ibn Hamid - Mwenyezi Mungu amrehemu na ambao wameonekana kuwa ni dhaifu na laini, hivyo wakawaweka mbele katika mpango wa "cunning" ambao ulianza zaidi ya miaka 20 iliyopita. Wakati wa miongo miwili hiyo iliyopita serikali iliyatanua majukumu ya Bin Baz (Mufti Mkuu) kwa vile serikali ilikuwa ikimjua udhaifu wake [Bin Baz] na urahisi wa kumshawishi na kumyumbisha kwa njia mbalimbali ambazo Wizara ya mambo ya ndani imekuwa ikizitumia kumpa habari za uongo. Hivyo kizazi kipya kikawa kinalelewa kikiamini kuwa mtu mcha-Mungu na mwenye elimu kuliko wote ni Bin Baz. Hii ilikuwa ni matokeo ya kampeni maalumu za vyombo vya habari kumpamba Bin Baz [kampeni] ambayo imefanyika kwa zaidi ya miaka ishirini. 

Baada ya hili, serikali ilianza kuyatumia mafundisho ya Bin Baz kupinga (kuzuia) kila mpango ulioletwa na wanazuoni waadilifu kurekebisha pale palipoharibika. Zaidi ya hapo serikali ikatoa Fatwa ya kuikabidhi Palestina kwa Wayahudi, na kabla ya hili, [ikatoa Fatwa] kuruhusu waendeshaji wa vita vya msalaba wa siku hizi (modern crusaders) kuingia katika nchi yenye misikiti miwili mitakatifu kwa kusingizio cha ‘kufanya hivyo ni jambo la lazima’. Aidha, kwa kuzingatia barua iliyotoka kwake [Bin Baz] kwenda kwa Waziri wa mabo ya ndani ya nchi, serikali iliwatia vifungoni wanazuoni waadilifu. 

Imani ya wananchi na vijana kwa Bin Baz ililegalega na hilo halikuwa jambo dogo kwa serikali [kwa vile] imani ya wananchi [hao hao] kwa wanazauoni waadilifu hasa wale waliokuwa magerezani ilikuwa imeongezeka. 

[Hivyo basi nikijibu swali lako ni kwamba] sera ya kikundi cha Ushauri na Marekebisho juu ya hawa wanazuoni ni kuendelea kuwapa ushauri waziwazi na pia kwa siri [pale inapobidi ili kuepuka bughudha ya sheria za nchi]. Ushauri na marekebisho hutolewa hasa kwa yale masuala ambayo wanazuoni hao wameyatolea [hoja na] maamuzi hadharani, na kisha ni kuleta hoja na maamuzi ya wanazuoni [waadilifu] waliyoyatoa kupinga (kuweka sawa) yale yaliyosemwa na wanazuoni waliotangulia ili kuwafanya wananchi waelewe hoja na hukumu sahihi juu ya mambo haya. Aidha sera inahusika na kuwaendeleza wanazuoni waadilifu na kuwataja mbele za watu kwa yale wanayostahiki ili kuzidi kujenga imani ya watu kwao. 

Unatathmini vipi siasa ya mambo ya nchi za nje ya serikali ya Saudia juu ya ulimwengu wa Kiislamu katika miaka iliyopita?

Siasa ya nchi za nje ya utawala wa Saudia kuhusiana na masuala ya Kiislamu ilikuwa ni aina ya siasa yenye mtazamo wa serikali ya kiingereza toka kuundwa kwa taifa la Saudi Arabia mpaka mwaka 1364AH (19945). Kisha siasa hizo zilichukua mtazamo wa kimarekani baada ya Marekani kuibuka kama taifa kubwa ulimwenguni baada ya Vita ya Pili ya Dunia. 

Inafahamika vizuri kuwa siasa za nchi mbili hizi [Uingereza na Marekani] zina uadui mkubwa ndani yake dhidi ya ulimwengu wa Kiislamu. 

Hata hivyo utawala huo mara kadhaa huyapigia kelele hadharani masuala yenye kuwagusa Wailslamu 

[lakini] bila kufanya juhudi ya kweli ili kulinda maslahi ya umma wa Waislamu mbali na jitihada ndogo [tu] ambayo hukusudia kuwakanganya watu [juu ya yale yanayowasibu Waislamu] na kuwatupia vumbi machoni mwao. 

Mapambano kati ya harakati za Kiislamu na utawala kibaraka wa Saudia yameweka katika historia mageuzi makubwa kufuatia mashambulizi ya hivi karibuni [1996] dhidi ya vituo [vya kijeshi] vya Marekani, [ambaye ni] mvamizi. Je, [katika Saudia] mashambulizi haya yalitoa picha gani juu ya msuguano wa ndani ya nchi yenyewe, na ni vipi [mashambulizi haya] yaliathiri uhusiano kati ya Saudia na Marekani?

[Naam] Kulikuwa na athari kubwa kufuatia ile milipuko miwili iliyotokea Riyadh, [na zilikuwa ni] athari za ndani na za nje ya nchi. Muhimu zaidi katika athari hizo ni vile wananchi kupata kujua taathira ya uvamizi wa Mareakani katika nchi yenye misikiti miwili mitakatifu na pia [kumbe] kauli za serikali [ya Saudia] si chochote bali ni matashi ya wavamizi wa Kimarekani. 

Hivyo wananchi wakawa hadhari kuwa matatizo yao makubwa yanasababishwa na wavamizi wa kimarekani na vibaraka wao katika serikali ya Saudia, iwe ni kwa mrengo wa kidini au kwa mrengo wa kidunia (katika maisha yao ya kila siku). Huruma na mshikamano wa wananchi kwa wanazuoni waadilifu waliofungwa magerezani pia viliongezeka. Kwa vile ufahamu wao juu ya ushauri na mwongozo [toka kwa wanazuoni hao waadilifu] viliwapelekea wananchi kuunga mkono harakati za kurekebisha mambo zinazoongozwa na wanazuoni hao na wale wenye kuwalingania watu katika Uislamu. Harakati hizi - kwa baraka za Allah - zinazidi kupata nguvu na watu zaidi wanaziunga mkono siku hadi siku. Watu wengi, raia na hata katika majeshi, wameonyesha kukubaliana na wanazuoni waadilifu, na pia ummah wa Waislamu ulimwenguni unazidisha upinzani dhidi ya Marekani. 

Ama juu ya uhusiano kati ya utawala huu [wa Saudia] na hao wavamizi wa Marekani, operesheni hizi [ulipuaji mabomu vituo vya kijeshi vya Marekani huko Riyadh] zimezivuruga pande zote mbili na zimepelekea [pande hizo] kushutumiana. 

Mareakni imedai kuwa sababu za milipuko hiyo ni matokeo ya siasa mbovu za utawala [wa Saudia] na pia mwenendo mbaya wa watu wa familia [ya kifalme] inayoitawala [Saud Arabia]. Serikali ya Saudia [nayo kwa upande wake ] inaishutumu Mareakni kwamba inautumia uhusiano uliopo [kwa manufaa yake] kwa kuilazimisha serikali ya Saudia kuingia katika mikataba ya kiraia na ya kijeshi ambayo ni nje ya uwezo wake [Saudia]. Mikataba hiyo imepelekea kutetereka kukubwa kwa uchumi na hivyo kuwaathiri wananchi. Zaidi ya hili ni ile tabia ya ukaidi na kiburi ya Marekani dhidi ya jeshi la Saudia na mwenendo wake usioridhisha kwa raia, na pia yale marupurupu ambayo wamarekani huyafaidi tofauti na majeshi ya Saudia. 

Mashambulizi haya pia yamepelekea kuibuka kwa upinzani wa wazi toka miongoni mwa wanafamilia ya kifalme [ambayo ndiyo watawala] na pia ndani ya majeshi ya ulinzi; kwa kweli tunaweza kusema kuwa nchi nyingine za Ghuba zimeamshwa kwa kiasi hicho hicho, na kwamba upinzani dhidi ya uvamizi huo wa Marekani umeweza kusikika katika familia tawala [za kifalme] na katika serikali za Baraza la Ushirika la Nchi za Ghuba (The Cooperative Council of Gulf countries). Tofauti katika mitazamo kati ya Mareakani na mataifa ya Ghuba zimeonekana kwa mara ya kwanza toka vita ya pili ya Ghuba. Hii ilikuwa ni wakati wa mkutano wa mawaziri wa mambo ya nchi za nje wa wa nchi wanachama wa Baraza la Ushirika la Nchi za Ghuba uliofanyika mjini Riyadh ili kujadili hatua ya Marekani kuivamia na kuipiga makombora Iraq. Tofauti hizi si chochote zaidi ya kuwa ni dalili ya mvutano ambao hatimaye umetokea ndani ya uhusiano uliopo kati ya Marekani na nchi za eneo hili [Ghuba] na hii ni matokeo ya hatua za awali za Jihad dhidi ya Marekani kujiingiza Riyadh na pia ni matokeo ya hofu [iliyozikumba] tawala hizi zikichelea nchi zao nazo kukumbwa na Jihad kama hiyo. 

Ilifahamika kuwa maafisa wa Marekani na wale wa Saudia walijaribu kuyahusisha mashambulizi haya na nchi fulani za nje. Je kuna msingi wowote katika madai haya?

Kutokana na kuongezeka kwa upinzani toka kwa raia dhidi ya Marekani kujiingiza Saudia na kuongezeka kwa ari ya wananchi kuunga mkono harakati za Jihad hii dhidi ya Wamarekani, imefikia sasa Marekani na Saudia wanaeneza propaganda za uongo ili kuvunja ari ya wananchi. Hii inajibainisha katika taarifa zao kuwa nchi fulani katika eneo hili zilisaidia mashambulizi yale yaliyofanywa ndani ya nchi yenye misikiti miwili mitakatifu. Hata hivyo watu wanajua kuwa hizi ni harakati za Kiislamu ndani ya nchi yenyewe dhidi ya uvamizi wa Marekani ambao umejionyesha katika picha ya wazi kabisa baada ya mauaji ya "machampioni" wanne walioendesha ile operesheni ya Riyadh, na ambao kwao, tunamuomba Allah awapokee kuwa ni miongoni mwa waliokufa shahidi. 

Imekuwa ni kawaida kwa nchi yenye kukumbwa na mgogoro wa ndani kusingizia nchi nyingine. Kabla ya ukibaraka wa nchi za kiarabu kwa Marekani kuonekana bayana, idara za usalama hazikusita kukishutumu kikundi chochote cha harakati za Kiislamu kuwa ni kibaraka wa Marekani na Israel. 

[Unadhani] utawala wa Saudia utafanya nini kuhusiana na kuibuka kwa wimbi hili la upinzani toka kwa vikundi vya Kiislamu, na ni nini matarajio yako?

Zipo hatua mbalimbali ambazo utawala wa Saudia unaweza kuchukua kukabiliana na hali hii, mojawapo ni kuleta suluhu kati yake na vikundi vyote vya wananchi vinavyoipinga serikali hiyo. Suluhu hii inajumuisha kuwaachia huru wanazuoni walio kifungoni, na pia kuleta mabadiliko muhimu katika utawala, ambapo badiliko muhimu kuliko yote ni kurejesha utawala wa Sharia ya Kiislamu, na kuendesha serikali kwa Shura ya kweli (kushauriana kabla ya kuamua jambo). 

Utawala wa Saudia unaweza kulazimika kuchukua hatua hii baada ya kujikuta kuwa wenyewe unatumika tu kwa manufaa ya Marekani. Leo hii wananchi wamebaini kuwa Wamarekani wamechupa mipaka - kisiasa na kiuchumi [katika mahusainao yao na Saudia]- na utawala unatambua kuwa wananchi sasa wanajua kuwa kumbe serikali yao imeingia ubia na Marekani kuongoza Saudia! Jambo hili lilijitokeza wazi hivi karibuni katika taarifa ya Marekani kwa vyombo vya habari ambayo ilitoa uhalali kwa Marekani kuikalia Saudia, na Wamarekani hawafanyi lolote zaidi ya kupora utajiri wa Wasaudia na kuineemesha Marekani. Hatua hii inategemea maafikiano ya watu ambao ndio wenye ufumbuzi wa kuanzisha mabadilko, na walio mbele katika hili [si wengine bali] ni wanazuoni waadilifu. 

Ama hatua nyingine ambayo utawala wa Saudia unaweza kuchukua, lakini hii ni hatua ngumu na ya hatari sana kwa utawala wenyewe, ni kuzidisha mapambano kati ya Waislamu na wavamizi Marekani, na hii itapelekea Saudia kukabiliwa na hali ngumu ya uchumi. Lengo kuu la hatua hii ni kuundoa madarakani utawala wa sasa, kwa radhi za Allah. 

Inaendelea wiki ijayo, Insha’Allah.
 

Juu
 

YALIYOMO
  

Tahariri
Fundisho toka Mtambani

Waislamu wataka serikali iwajibike

Serikali yakiri kupokea malalamiko ya Waislamu: Mkapa awataka Watanzania waepuke kubaguana

Mtambani wasema kamwe hawakubali pumbao la kisiasa

Maoni: Kweli ikisimama uongo hujitenga

MARADHI YA KISAIKOLOJIA:  TRANSVESTISM

Mjue Usama bin Ladin

Risala ya Waislamu katika Baraza la Idd  kwa Mgeni Rasmi Rais  Benjamin Mkapa

Wafanyakazi TANESCO waingiwa hofu ya wingu la udini

Hotuba ya Rais Mkapa kwenye Baraza la Idd Diamond Jubilee Jan. 19, 1999

Makala: Hotuba ya Mkapa, Magazeti ya Ruzuku na Waislamu
Na J. Hussein

Kutoka magazeti ya zamani: Washitakiwa walipelelezwa

Hivi siku ya ibada ni ipi?: Ijumaa, Jumamosi au Jumapili?
Na Mwinjilisti Bunga E. Dettu

'Msitarajie kupambana na adui kwa upanga wa Hamza'

Sasa ni kulishwa nguruwe kwa nguvu

Sayansi na Teknolojia
[KUPELEKA  FAX NCHI ZA NG'AMBO BURE!]

Masomo ya Dini ya Kiislamu

Barua za Wasomaji

Mashairi

Chakula na lishe
[Faida na  hasara za kupika chakula]
 


Bonyeza hapa
kushriki mjadala au kutoa maoni juu ya habari hizi na masuala mengineyo ya Kiislamu kwenye Baraza ya Wasomaji

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtanzania.org

 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita