|
Na.185 Shawwal 1419, Januari 22 - 28, 1998 |
|
Washitakiwa walipelelezwa
Joe Masanilo na Stepheni Mganga
MIKUTANO yote iliyokuwa ikifanyika kati ya shahidi mkuu wa kesi ya uhaini Bw. Potlako Kitchener Leballo pamoja na washitakiwa saba wa kesi hii ilikuwa ikichunguzwa na maafisa wa uchunguzi, Mkurugenzi wa Idara ya uchunguzi aliieleza Mahakama Kuu mjini Dar es Salaam jana wakati alipokuwa akiendelea kutoa ushahidi wake. Alipoulizwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bw. Mark Bomani kwamba alijuaje kuwa Leballo kweli alikutana na washitakiwa wakati alipokuwa akihitajika kufanya vile, Mkurugenzi huyo alijibu: "Wakati kila nikijua kwamba kutakuwa na mkutano kati ya Leballo na mmojawapo au baadhi ya washitakiwa hao, nilikuwa nikiwatuma maafisa fulani wa uchunguzi kwenda kuchunguza habari za mkutano huo bila ya washitakiwa kufahamu. Shahidi huyo alisema kwamba, Leballo aliwahi kumwarifu juu ya safari yake ya kwenda Nairobi mnamo tarehe 25.3.69 ambapo alikwenda na kurejea tarehe 1.4.69. Leballo alimwambia Mkurugenzi huyo kwamba madhumuni ya safari yake ya Nairobi ilikuwa kukutana na mshitakiwa wa kwanza Gray Likungu Mattaka, ili apate kuhakikishiwa zaidi na Mattaka juu ya mpango wa kupindua serikali kama alivyokwisha elezwa na mshitakiwa huyo hapo awali. "Nilijua kwamba Chipaka na Leballo walikuwa wamekwisha kutana na kwamba Leballo alikwisha tambulishwa kwa Prisca na Titi Mohamed. Mkutano huu ulifanyika katika Hoteli ya Twiga. Bwana Leballo pia alikutana na Titi katika ukumbi wa Chuo cha Kiislamu huko Chang’ombe ambako walizungumza na Titi jinsi Rais Nyerere pamoja na maafisa wengine wakubwa wa serikali wangeuawa, shahidi huyo alisema. Mkurugenzi huyo aliendelea kwamba mnamo tarehe 24.3.69 Leballo alimjia na kumweleza juu ya mkutano wake na Chipaka huko katika hoteli ya Twiga. Alipoulizwa na Mwanasheria Mkuu, Bwana Bomani, kwamba alijuaje kuwa Leballo na Chipaka walikuta kweli, shahidi alisema kwamba aliwahi kuwatuma maafisa wa uchunguzi kwenda kuchunguza wakati mkutano huo ulipokuwa ukifanyika. Mkurugenzi alisema kwamba siku iliyofuatia tarehe 25.3.69 Bwana Leballo aliondoka kwenda Nairobi "na niliwapeleka maafisa fulani kwenda kumsindikiza," alisema. Mkurugenzi huyo aliendelea kuieleza Mahakama kuwa katika mwezi wa Aprili mwaka 1969 alikuwa amesafiri kwenda ng’ambo. Alisema "nilikutana tena na Leballo tarehe 2.5.69 na akanieleza kwamba mpango wa kuipindua serikali ya Tanzania kwa njia zisizo za halali kama alivyoelezwa na Grey Likungu Mattaka mjini Nairobi, ulipokelewa na kukubaliwa kwa shangwe na Chipaka. Kamaliza na Titi na kwamba Mattaka mwenyewe alikwishaweka ahadi ya kuagiza fedha kutoka kwa Kambona." Alisema mbele ya mahakama pia kwamba Leballo alitoa barua iliyotoka kwa Mattaka kwenda kwa Prisca ambayo yeye Mattaka aliinakili na kumpa Leballo nakala moja. Bwana Bomani: Unaweza kuitambua nakala hiyo kama ukiiona? Mkurugenzi: Ndiyo, ninaweza. Bwana Bomani: Utaitambuaje barua hii? Mkurugenzi: Ninaweza kuitambua kwa jina la Chaima. Bwana Leballo: aliniambia kwamba baada ya kukutana kwa mara ya kwanza na Mattaka, mshtakiwa huyo alibadili jina lake na kujipa jina la bandia Chaima. Jaji Mkuu: Je barua hiyho ilitafsiriwa? Mkurugenzi: Mara nakala hiyho ilipokwisha tengenezwa ilitafsiriwa ili niweze kuelewa imeandikwa nini. Bwana Bomani: Ulijua kuwa barua ililetwa? Mkurugenzi: Niliarifiwa kuwa inaletwa. Mkurugenzi alisema kwamba ku tokana na taarifa ya Leballo, Chipaka, Titi, Leballo na Prisca walikuwa wakutane na kujadilimambo watakayofanya huku wakati wakisubiri fedha kutoka kwa Kambona. Mapema Wakili anayemtetea Chipaka, Bwana Raithatha, alikataa Mkurugenzi wa uchunguzi asitumie maandishi yake aliyoandika kuhusu taarifa ya Leballo, kwa sababu, alisema, hakuna ruhusa ya kisheria kwa shahidi kutumia kumbukumbu za maandishi yake. "Maandishi yaliyotayarishwa na shahidi kutokana na taarifa ya Leballo yanadhihirisha kwamba yanaweza kumpa kumbukumbu za kutosha,"alisema. Bwana Verji, Wakili wa Kamaliza, alikataa vikali Mkurugenzi asitumie
maandishi hayokwa sababu maandishi ya kwanza yaliyoandikwa kwamkono yaliharibiwa
makusudi.
|
YALIYOMO
Tahariri
Waislamu wataka serikali iwajibike Serikali yakiri kupokea malalamiko ya Waislamu: Mkapa awataka Watanzania waepuke kubaguana Mtambani wasema kamwe hawakubali pumbao la kisiasa Maoni: Kweli ikisimama uongo hujitenga MARADHI YA KISAIKOLOJIA: TRANSVESTISM Risala ya Waislamu katika Baraza la Idd kwa Mgeni Rasmi Rais Benjamin Mkapa Wafanyakazi TANESCO waingiwa hofu ya wingu la udini Hotuba ya Rais Mkapa kwenye Baraza la Idd Diamond Jubilee Jan. 19, 1999 Makala: Hotuba ya Mkapa, Magazeti
ya Ruzuku na Waislamu
Kutoka magazeti ya zamani: Washitakiwa walipelelezwa Hivi siku ya ibada ni ipi?: Ijumaa,
Jumamosi au Jumapili?
'Msitarajie kupambana na adui kwa upanga wa Hamza' Sasa ni kulishwa nguruwe kwa nguvu Sayansi na Teknolojia
Chakula na lishe
|