|
Na. 052 Jumatano Juni 14 - 20, 2000 |
|
|
|
|
|
Dunia ndivyo ilivyo - 2 Mtunzi: Marcussy G. Mzee MZEE Kidazu na mkewe wanapata mwaliko wa harusi hivyo wanafunga safari kuelekea kwenye sherehe hizo zilizofanyika nyumbani kwa Mzee Haule ambaye mtoto wake Lucy alikuwa anafunga ndoa na kijana John. Idd anatumia mwanya huo wa kutokuwepo kwa wazazi wake kwa kumtaka kumwingilia kinguvu Mariam. Alionasiku hiyo ndio nzuri baada yakutofanikiwa kwa muda mrefu. Mariam alikuwa hana hili wala lile akitokea bafuni kukoga akiwa amejifunga upande mmoja wa Khanga, hakuwa na nguo yoyote ya ndani,alikuwa amerudisha mlango wa chumbani kwake akijifuta maji maji. Idd bila aibu anaingia chumbani humo ghafla na kumsukumiza Mariam kitandani na kumaliza haja yake bila ridhaa ya Mariam, kutokana na kuingiliwa kinguvu alipata maumivu makali sana, sababu ilikuwa ndio mara yake yakwanza kufanyiwa unyama ule, siku hiyo Mariam alilia sana. Idd alifokewa sana na Baba yake na kutishiwa kuuawa iwapo atarudia tena upumbavu wake kama huo. Kutokana na onyo hilo Idd hakuthubutu tena kumchezea hata kumtania Mariam, waliheshimiana kwa kupeana salam tu,huku maisha yao yakiendelea vizuri pasipo matatizo. Raha ya maisha ya nyumba ile vilimfanya Mariam azidi kunawili, akapendeza, kanenepa vizuri akawa na sifa zote atakiwazo kuwa nazo mtoto wa kike, kwa kifupi alizidi kuvutia. Hali hii ya afya njema ya Mariam ilimtia kiwewe hata Mzee Kidazu. Wavulana wengi pale mtaani walijaribu bahati zao za kumtaka urafiki bila mafanikio, kwani alikumbuka sana kauli ya Baba yake alipewa majina mengi ya ajabu pale mtaani na baadhi ya vijana, lakini msimamo wake ulikuwa ni ule ule hakutaka kuchezewa na mvulana yoyote, alizingatia zaidi kazi iliyompeleka pale mjini. Mkewe Mzee Kidazu anapata likizo ya uzazi toka kwa mwajiri wake kama ilivyo sheria kwa akina mama wafanyakazi pindi wanapokuwa katika haliya namna ile, na muda wa kujifungua ulipokaribia Mzee Kidazu anachukua jukumu la kumpeleka nyumbani kwao kijijini Doma -Malaka. Kuondoka kwa mkewe, kulimfanya Mzee Kidazu aanze kubadili tabia yake, alianza kurudi nyumbani mapema sana kuliko hapo mwanzoni, alikuwa akiingia chumbani kwa Mariam bila ya hodi na kumwambia amtayarishie chakula kisha ampelekee chumbani kwake. Msichana Mariam hakujua nia mbaya aliyokuwa nayo Mzee Kidazu au "mjomba" kama alivyozea kumwita, alitekeleza kama alivyoambiwa, aliandaa chakula na vinywaji vyepesi, alipokuwa akipeleka chakula kwa "mjomba" kwa bahati mbaya aliteleza akaanguka, chupa ya soda ikamkata sehemu ya mguuni, alikaa chini kwa maumivu huku damu zikimtiririka. Mjomba wakeakaenda kumnyanyua, Mariam alishangaa sana kuona mikono ya "mjomba" wake ikishika kiuno chake, lakini Mariam hakuhisi jambo baya lolote, alijua ni katika hali ya kumfariji. Idd mtoto wa kwanza wa Mzee Kidazu anapewa pesa za matumizi ili kuzipeleka kijijini kwa mama yake kwa ajili ya matumizi, hali hii inampa nafasi Mzee Kidazu na utu uzima wake kumtaka kinguvu Mariam, Mh, ama kweli wazee wengine ovyo, kwani Mariam angeweza kuwa sawa kabisa na mtoto wake, aliporudi toka matembezini alimwambia Mariam ampelekee chakula chumbani alimpomaliza kula Mariam alikwenda kwa nia ya kuondoa vyombo, lakini "mjomba" wake akamkataza, akiwa na sura iliyojaa uchu wa "kubaka" akamrukia Mariam, akamnyanyua Mariamu juu juu na kumlaza kitandani, Mariam alistushwa na hali hiyo, huku mikono ya Mzee Kidazu ikiwa kifuani kwa Mariam ikiyaminya matiti yake madogo "mjomba, mjomb aniache, sitaki", alilalamika sana Mariamu huku akitoa mikono ya mjomba wake huku akikataa kutimiza lile lililokusudiwa na mjombe wake. Mariam alifanikiwa kukurupuka mbio mpaka chumbani kwake. Akafunga mlango na kujilaza kitandani. Mzee Kidazu kama kawaida baada ya mihangaiko ya hapa na pale, akarudi nyumbani kwake kama kawaida, akamwita Mariam chumbani kwake na kumwambia amtayarishie chakula kisha amletee chumbani, Mh! Ama kweli. Mariam akatekeleza kama kawaida alipokujakutaka kutoa vyombo, mjomba wakea kamkataza, akamwambia "Mariam keti hapo kwenye kiti", Mariam akaketi kwa kutii amri, akapewa "safari lager" ili anywe, lakini alikataa,kwa sababu katika umri wake hajawahi kutumia ulevi wa aina yoyote ile, kinywaji alichokifahamu yeye ni soda na maji baridi tu, ndipo bila aibu mjomba "Mzee Kidazu" akuchuku avidongo vya usingizi akaweka kwenye soda kisha akampa Mariam. Usingizi mzito ukamchukua, Mzee Kidazu akamnyanyua Mariam mpaka kitandani na kutimiza azama yake. AH! Mtu mzima akafanya jambo la aibu tupu. Mariam akastuka ghafla toka usingizini akajukuta yupo kama alivyozaliwa, "mjomba kwa nini umenifanyia hivi, huu si unyama"? Alilalamika Mariam kwa tendo alilofanyiwa. Mzee Kidazu alimbembeleza Mariam na kumuahidi zawadi kemkem pamoja na pesa nyingi na kusihi asimwambie mtu yeyote. Mariam alirudi chumbani kwake huku akilia kichwani akiwa na mawazo tele, akajitupa kitandani usingizi mzito ukampitia, alipostuka tayari ilikuwa asubuhi kumekucha, amechoka hoi! Mariam alizidi kunawili kutokana na huduma zote alizokuwa akipewa na kumzidishia tamaa mjomba wake, hali iliyopelekea kukiuka maadili ya dini, shetani akamtawala ndani ya moyo wake na kuiteka akili yake yote, pasipo kukumbuka tendo analofanya ipo siku litaleta aibu siku moja. Miezi kadhaa ilishapita tangu mjomba Mzee Kidazu afanye tendo la "kubaka" akazidi kuisaliti ndoa yake wakati mkewe hayupo, Mariam naye akanogewa na mambo ya mjomba wake, akajisahau, udhaifu wa tamaa na dhiki ya pesa alizokuwa akipewa na kuzipeleka kijijini kwa wazazi wake vilizidi kumpumbaza na kumuingiza mtegoni Mariam. Mama Idd, mkewe na Mzee Kidazu anarejea toka kijijini akiwa amejifungua mtoto wa kike aliyempa jina la Jamila, alimkuta Mariam akiwa na afya nzuri na kumsifia kwamba hali ya hewa ya Morogoro inampenda, Mh! Masikini mama Idd hakuelewa kilihchokuwa kinaendelea. Miezi minne ilikatika Mariam hakupata kuziona siku zake, huku akiona hali ya mabadiliko katika mwili wake, hali ya uchovu, kichefuchefu na kizunguzungu ndio viliutawala mwili wa Mariam, ama kweli ulikuwa ni usiku wa giza! Mariam hakujijua alishanasa ujauzito ukachukua nafasi yake, hofu ikamjaa, iwapo mama Idd angegundua kitu,hivyo aliendelea kufanya kazi za pale ndani kivivu vivu, kutwa nzima alikuwa mtu wa kulala lala tu. "Wewe Mariam kwanini siku hizi umekuwa mvivu namna hiyo, kazi hufanyi unalala tu ondoka basi usinitie kichefuchefu hapa ngoja Baba Idd aje nimwambie", alifoka mama Idd. Mzee Kidazu akarudi toka kazini, baada ya salama za kujuliana hali, mama Idd akamueleza lililomkifu moyoni mwake "hivi una tabia ya huyu Mariam kwa jinsi alivyobadilika siku hizi", alisema kwa sauti iliyojaa hasira. Baada ya kupata mashtaka hayo, Mzee Kidazu anamwita "Housegirl" wake kisha kumuuliza "Mariam kwanini siku hizi umekuwa mvivu wa kazi, hukuja kulala lala hapa sawa"? Mariam kwa macho yaliyo jaa ukarimu alimwangalia mjomba wake, kisha akaangalia chini akatamka "Mjomba mimi kwa kweli kazi nafanya kwa bidii isipokuwa kwa sasa ninaumwa, hivyo sijisikii vizuri", alijitetea Mariam kwa sauti iliyojaa mtetemo wa woga. Kutokana na maelezo hayo, Mzee Kidazu akamwambia Mariam, "sasa kama unaumwa kwa nini usimwambie mama akupeleke Hospitalini?" Mariam mapigo ya moyo yakapanda, akatulia kwa sekunde kadhaa, huku akijua wazi ule muda wa kusema ukweli umefika, sasa ukweli ambao hatima yake unaweza kuzua mtafaruku kati ya Mzee Kidazu na mke wake. Mariam akalipua bomu, Mhe! Msema kweli ni kipenzi cha Mungu. "Mimi siumwi ugonjwa wa kwenda hospitali jamani isipo......" kabla hajaendelea Mzee Kidazu akafoka "sasa ni kitu gani kinachokusumbua? "Nina mzigo wako" Mariam alijibu. "Mzigo wangu" toka wapi? Alijifanya kushangaa, "sio mzigo wa kutoka sehemu, mimi ni mja mzito na wewe ndio mwenye mzigo huu "mjomba:, alimaliza kutoboa siri huku machozi yakimtoka. "Mwana wa haram wee! Mtoto hauna adabu hata kidogo, mimi ndio nimekupa hiyo hiyo ....nasema koma kabisa na uondoke hapa nyumbani kwangu, mimi mtu mzima na heshima zangu unasema nimekupa mimba, toka hapa nenda huko huko ulikoitoa sio kusema uongo hapa" alikuja juu bila aibu huku akijua wazi dhambi ile ni yake, anadai yeye ni mtu mzima, akasahau kuwa anaweza kuwa mtu mzima lakini wa ovyo, kisha akaendelea kufoka, "Siwezi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mtoto mdogo. Hujui hata kuoga, kwanza hata harufu ya maziwa haijakutoka, nasema usiniletee balaa lako hapa. "AAAH-leo unanikana, unaniona mtoto mdogo sijui hata kuoga?" Kumbuka ulivyonifanyia umnyama wako, uliniwekea dawa za usingizi kwenye soda kisha "ukanibaka"na uliendelea na mchezo wako huku ukinilaghai kwa pesa, mimi sisemi zaidi kama leo unanikana Mungu yupo atanilipia na ipo siku utaona aibu juu ya hii dunia kwani malipo ya dhambi ni mauti bali kalama ya Mungu ni uzima wa milele".Alilalama Mariam huku akitoa machozi. Mzee Tandara na mkewe Bi. Fatuma walikuwa wakiendelea vizuri na biashara yao ya kuuza vitumbua katika baraza ndogo ya nyumba yao ya nyasi, hukuwakiendelea kuweka pesa katika Benki ya Maendeleo vijijini, wakamshukuru Mungu huku wakikubaliana na ule msemo usemao "Mungu hamtupi mja wake",lakini ya Mungu vile vile ni mengi msichana Mariam alikuwa katika Tafrani nzito huko mjini bila wazazi kujua kinachoendelea kati yaMariam na mwajiri wake. Mkewe Mzee Kidazu alikuja juu kama moto wa kifuu baada ya kusikia habari ile nzito toka kwa Mariam, ulizuku ugomvi mkubwa, huku mkewe akimimina matusi na kashfa nzito kwa Mzee Kidazu huku akidai apewe Talaka yake aondoke ili amwache aishi na "house-girl" wake. Juu ya Mzee Kidazu kujaribu kujitetea mbele ya mkewe bado hakumsaidia kitu. Mariam akawa anafungasha nguo zake katika mfuko wake wa Rambo uliochakaa tayari kwa safari ya kurejea kijijini, alisindikizwa hatua chache kwa macho, kisha akageuka, akamtazamaMzee Kidazu kwa jicho la kisasi, kwa sauti ya huzuni akatamka "Mjomba! Kama kwangu limetota, kwa uwezo wa Mungu kwako litazama". Kweli dunia ndivyo ilivyo! Mariam akavuta hatua kuelekea stendi ya "Bus" tayari kurejea kijijini kwa wazazi wake. Hukum nyuma akiacha mzozo mkubwa kati ya Mzee Kidazu na mkewe kutokana na kitendo cha kishenzi alichokifanya kwa "House-girl" wao, lakini mzozo huo ukamalizwa kifamilia, mambo yakaisha kwa usalama maisha yao ya ndoa yakaendelea kama zamani. Mariam alipokelewa kwa furaha na wazazi wake wawili, lakini Mariam hakuwa na furaha yoyote aliyoionyesha kwa wazazi wake, alikuwa ni mnyonge aliyegubikwa na mawazo tele kicheani lakini hali hii haikuwapa mstuko wazazi wake, kwani walijua vile ni uchovu wa safari. Baada ya salamu na maamkizi ndipo ilipodhihirika kwanini Mariam kwa muda ule yupo pale kijijini, Babana Mama yake Mariam walisikitika sana kufuatia habari ile iliyomuhusuMariam. Pesa zilizokuwa zikiwekwa Benki zilimfanya Mariam asiyaonemaisha ya pale kijijini magumu kama alivyo yaacha mwanzoni, akawa anashirikiana na mama yake kupika vitumbua, siku mojaMariam alikaa chini ya mtiwa mpapai huku amejiinamiaakifikliria juu ya ule ujauzito, "wewe! Vipi unaumwa"? Alistuliwa na sauti ya mama yake "Hapana mama nimepumzika tu", "usifikirie sana mwanangu dunia ndivyo ilivyo". Hivyo ndivyo ilivyojihili hali iliyopelekea Mariam kurudi tena katika himaya na maisha ya kijijini, kisichoridhiki hakiliki kutokana na mwendo mzuri wa biashara ya vitumbua wanakijiji wengi wakaanzisha biashara hiyo nakufanya kipato kwa upande wa kina Mariam kishuke sana. Hivyo hali yamaisha yao ikarudi tena katika taabu kwani hata ile akiba yaBenki nayo ilikuwa ikipungua siku hadi siku. Muda ukafikia, Mariamakajifungua mtoto wa kiume mwenye afya njema. Mh! Hapo ndipo ilipodhihirika kwamba kila panapo ukweli uongo hujitenga! Mariam alitoa machozi kilaalipomwangalia mtoto wake mzuri wa kiume ambaye amefanana sana na Mzee Kidazu mwishoe akajisemea "Inshaalah Mungu yupo". Mzee Tandara akarudia tena biashara ya kuuza kuni. Alitembea kilometa kadhaa kutafuta kuni, maisha yakawaelemea tena, huku Mariamakiendelea kumhudumia mtoto wake kwa taabu na mashaka matupu, akampa jina la Masumbuko. Juu ya matunzo duni aliyokuwa anayapata lakini aliendelea kukua vizuri, Masumbuko akafikia umriwa kwenda shule, akaanza shule, juhudi zake katika masomozilileta mafanikio katika matokeo ya mtihaniwakewa mwisho kwa kufaulu vizuri. "Sawa mwanngu juu yakufaulu kwako nasikitika sana tenanina uchungu mkubwa moyoni sina uwezo wa kugharamiamasomo yasekondari, wewe mwenyewe unaona hali ya maisha yetu ilivyo,nitafanya nini mwanangu?" Maneno haya yalimchomasana Masumbuko na kumfanya ajiinamie, kisha akamtazama mamayake, akamuuliza "Mama! Hivi Baba yuko wapi?" Swali hili likampa hudhuni sana mamayake, kwa macho yaliyojaa huruma akamjibu kwa kumpa mkasa wote uliomkuta mpaka kuzaliwa kwake na kuwepo katika hali ile.... Kutokana na mambo yaliyomkuta mama yake, Masumbuko roho ilimuuma na akapata uchungu mkubwa, kweli duniani kunawatu wenye tabia mbaya tena wengine ni watu wakubwa wenye umri wa kutosha kutofanyaupuuzi kama aliofanyiwa Mariam, mama. Hivyo Masu akaamua kumuaga mama yake kwenda mjini kutafuta kazi lakini kabla hajaondokaakapewa wosia na mama yake... Nyumbani kwa Mzee Kidazu maisha yaliendelea huku mtoto waoJamila akiendelea na masomo ya sekondari, Jamila alikuwa Jamila haswa ameumbika vizuri akamvutia kila mtu, lakini hakutaka kupotezewa muda na mtu yeyote hasa walewenye tamaa za mapenzi, lakini Waswahili husema "Ndege mjanja..... Jamila hakutaka kabisa kupotezea mudawa walewenye uchu wa mapenzi kwa watoto wa shule. Mzee Kidazu na mkewe wanaafikiana kutafuta tena mtu wa kufanya kazi ndogo ndogo pale nyumbani, lakini safari hii linatolewa sharti na mkewe, kwambamfanyakaziwa sasa asiwe msichana bali mvulana, kwa ajili ya kazi ndogo dngo isipokuwa kupika. Masumbuko anatelemkatokandani yaBus la"Yo Transport" katika stendi yaMa-Bus Msamv,akashika njia inayoelekea katikati ya Mji wa Morogoro, alipokuwa katika maeneo ya jirani na kiwanda cha kutengeneza sabuni cha KOMOA huku akishangaa shangaa baadhi ya majengo, anastuliwa na honi ya gari kwa nyuma, alipotakakugeuka tayari dereva alishafunga breki jirani kabisa namiguu yake, alipoangalia ndani ya gari akakutana macho kwa macho na mzee wa Makamo kiasi, na macho yao yalipokutana yalizungumza kitu fulani. Mzee Kidazu akafungua mlango wa gari, akamwita Masumbuko kwa sautiya utaratibu "Wee kijana hebu njoo"! Masumbuko hakukawia akatii wito akamsogelea, na ikamtokasalam iliyo jaa hofu "Shikamoo!" Naye Mzee Kidazu akaitikia"Marahaba mtoto mzuri, je unaitwa nani,unatoka wapi?" "Mimi naitwa Masumbuko, natokea Mikese nimekuja hapa kutafuta kazi" alijibu hukuakimuangalia usoni, kwa kweli walifanana, lakini hawakujuwana kwamba pale ni mtu na Baba yake, mambo hayo,akamchukua kwenye gari mpaka nyumbani. Juhudi za kufanya kazi pasipo uvivu kulimfurahisha sana mamaIdd.Kwani hakupoteza hata sekunde moja bila kujishughulisha na kazi. Wakawa nauelewano mzuri sana na Jamila. Kutokana na Jamila kupenda kumtania kila mara wakati mwingine kusaidia baadhi ya kazi, lakini panapofuka moshi.....,Masualijitahidi sana kuvikwepavishawishi vya Jamila,ambaye alikuwa akifanya vituko vya kila aina hasa wanapokuwa wapowawilitu pale nyumbani. Jamila alivutiwa sanauzuri wa jambo aliokuwa nao Masu, hali yaupole, unyenyekevu na tabasam lake vilimfanya Jamila aingie kichwa kichwa, lakini Masu aliogopaasijefukuzwa kazi bure. Ilifikia siku ya siku Masuakiwa chumbani kwake akibadilisha nguo kwani alitoka kukoga, akastukia Jamila ameingia ghafla na upande mmoja wa khanga, akafunga mlango kwa ndani hali aliyokuwa nayo ilimfanya Masu atetemekeakafumba macho kwa viganja vya mikono yake, katika vuta nikuvute wote wakajikuta kitandani, puu! Jamila akatoka huku moyo wakeumeridhika lakini Masu akabaki kitandani amejiinamiaakijutiatendo lile, akajiuliza maswali mengi iwapo Mzee Kidazu atagundua, Mh! Masikini bila kujijua kumbe ni mtunadadayake, aibu! Tabia ikajengeka ikaota mizizi, Masumbuko naye Aah! Kamchezo kakaendelea, lakini ilililo na mwanzo halikosi mwisho, tahamaki Jamila akanasa, ujauzito, Juhudi za kutaka kuitoa nzikashindikana, siku zilivyozidi kwenda na mimba nayo ikaanza kujitokeza,hakupewa barua yakufukuzwa shule. Mzee Kidazu alipopata habari ya kufukuzwa shule nusra apoteze maisha kwa "Pressure" akamwita Masumbuko, kilichofuatia hapo nikipigo kikali. Huku akitoa matusi mazito mazito. Mh! Mkuki kwa nguruwe....., Masu akatimuliwa kwa kutupiwa vitunguo zakechache zilizokuwemo kwenye kifukochaRambo, akashika njia nakuondoka huku akiwa na mawazo tele kichwani "Nitaenda wapi?" Wakati huu mji siuelewi vizuri, iwapo nitaishi bila kazi matokeo yakehayatakuwa mazuri nifanye nini mie?" Mwishoe akakata shauri kurudi kijijini kujisghughulisha na kilimo. Majira ya mchana wa jua kali sana kijana Masu akawasili kijijini kwao, akapokelewa kwa furaha na mama yake pamoja na Babu na Bibi yake, Masumbuko hakuficha kile kilichomsibu mpakakufikia kurudi tena katika maisha ambayo alishaanza kuyasahau mama yake machozi yakamtoka, kwanitukio lile lilifanana na lililomkuta yeye, kisha akajiinamia kwa sekunde kadhaa mwishoe Masu akamwita mama yake "Mama! Usilie ukilia utaniliza na mimi,dunia ndivyo ilivyo ina mambo mengi yaliyopangwa naSub-ana Mungu yupo na atatusaidia kwa haya yaliyotokea", kauli ya Masu inamtoa mamayake katika majonzi. Wakaanza kilimo kilicho leta faraja kwao. Nyumbani kwa Mzee Kidazu hali ya masimango na kejeli vilimuandama Jamila, hali iliyopelekea akose Raha, hali ya afya yake ikadhoofika sana, akamkumbuka sana Masu, akajiinamiahuku machozi yakimtiririka, kuondoka kwa Masu ilikuwa ni hudhuni tupu kwake, akakaa, akawaza sana mwishoe akafikia uamuzi wa kunywa sumu ili aepukanane naadha toka kwa Baba yake. Akajifungilia ndani akachukua glassi ya maji akamimina sumu kali ya panya, akainyanyua glassi. Lakini kabla hajainywa nafsi ikamsuta na ikamuonya "Olewaowalewanaozurumu nafsi za roho zao na kuua, hawa wote siku ya kiyama Mungu hatowauliza kitu atatia moja kwa moja katika shimo la moto wa Jehanamu". Sauti hii ilimpomjia, akairudisha glassi juu uya meza,msichanaJamila akaona ni afadahali apande "Bus" amfuate kipenzi chake Masu huko klijijini, kwani alikuwa tayari kwenda kuishi maisha ya aina yoyote. Ilikuwa ni safari iliyoashiria huzuni, na kwenda kuishi maisha ya dhidiki ambayohajayazoea, lakini alijipa imani yaushindi, akapnda "Bus laYob-Transport tayarikwa safari ya kijijini Mikese, safari pevu ilikuwa mbele yake - kuishi mbali na familia yake baba na mama, kitu alichohisi kitakuwa kigumu sana kwake, lakini mambo yameharibika: mawazo yalimsumbua katika muda wote wa safari ile. Masumbuko na mama yake, wakiwa wameshika majembe mkononi wamechoka jua kali sana wanatoka shamba, ghafla Masu alistuka "Aaah! Jamila" akamkimbilia kwa furaha, akampokea mizigo, mabegi mawili yaliyojaa nguo, wakaongozana mpaka nyumbani, wakala chakula kwa pamoja, ndipo Masu akamfahamisha mama yake kuhusu Jamila, wakafurahiwakamkaribisha sana pale kijijini. Baadaya mapumziko mafupi, Jamila akaelezea hali halisi iliyomkuta, Masu na mama yake walisikitika sana, lakini mama Masu ndio lilimchomazaidi, maisha yakaendelea vizurihuku Jamilaakiizoea hali ya maisha ya pale kijijini. Nyumbani kwa Mzee Kidazu amani ikatoweka kwani mkewe amekuja juu anataka ajue ni wapi alipokimbilia Jamila, lakini Mzee Kidazu akamtamkia mke wake "kama unamtaka mwanao nenda mfuate huko alipo." Kluanzia sasa sitaki kusikia upuuzi wako wa kumuuliza Jamila." Muda wa mavuna ulipofika, familia ya Mzee Tandara ilifanikiwa kupata mavuno mazuri sana walipata magunikaribu hamsini ya mahindi na hususan ya mpungu kutokana na kilimo cha hek kumi za mpunga, kumiza mahindi, wakatenga kiasi kwa ajili ya chakula na kiasi kilichobakia walipeleka Morogoro kwa mauzo, wakapata pesa nyingi za kutosha. Mazumboko akajenga nyumba nzuri sana pale kijijini akafungua duka kubwa. Mzee Tandala akamwita Masu ili amueleze jambo la busara lenyehekima "Mjukuu wangu nilichokuitia hapa ni kimoja, fanya mpango ili tupeleke barua ya posa ili ufunge ndoa na huyu bint, sababu si vizuri kidini kukaa katika hali hii",baada ya maelezo hayo Masu alipata furaha moyoni, ikaandikwa barua akatumwa mshenga, akapnda bus kuelekea Morogoro. Maelezo aliyopewa yalimfikisha nyumbani kwa Mzee Kidazu bila wasiwasi. Mzee Kidazu kwa kutotaka kuiona tena sura ya Jamila pale nyumbani akaipokea barua ile ya uchumba kisha akatoa majibu harakasana ya kulikubali ombi lile. Mshenga akaipokea barua ya majibu akafunga safari kurudi kijijini. Mipango na michango ya harusi ikapangwa haraka haraka nyumbani kwa Mzee Tandara pia nyumbanbi kwa Mzee Kidazu. Jamila akapanda Bus kuelekea Morogoro, huku tumbo likiwa tayari limeshajitokeza zaidi, akapokelewa vizuri na mama yake, siku mbili baadaye akapelekwa saloon kuandaliwa zaidi..... Masumbuko na nduguze Bibi, babu na mama yake wakajumuika na baadhi ya jamaa kuelekea Morogoro kumfuata mchumba wake, tayari kwa kufunga ndoa. Watu walikuwa wengi kwelikweli, nyimbo za kila aina ziliimbwa,masheikh wakatayarishwa kukamilisha lile lililokuwa likisubiriwa, lakini kabla hakuajatendeka lolote, Umati wote wa wale ulistushwa na sauti kali ya mwana mama aliyesimama kuipinga ndoa ile, "Nduguwaalikwa, nasikitika sana kwa kuivunjaau kuisitishandoa hii, kwani hao wanaotaka kufunga ndoa ni mtu na dadayake wa kuzaliwa kwa baba mmoja, hivyo sipingani nasheria ya dini,kamasheria inaruhusu watu hao waoane sawa", alisema mamaMasu hukuakilia kwa sauti,umati wote ukapatwa namshangao mkubwa. Mama Masu akaelezea mkasa mzima kuanzia yeye mwenyewe alivyopewa ujauzito na Mzee Kidazu kisha akatimuliwa ndipo akazaliwa Masu, ambapo Masu naye akapata kazi ya ndani kKidazu ibilisi akawaingia akatembea na Jamila mtoto wa Mzee bila kujua kuwa ni dada yake. Kilifuata kiliokwa Masu naJamila ambaye alibakiza muda jmchache kujifungua: "Mh! Yaani nazaa na kaka yangu?" Alijiuliza. Sheikh Mkuu Yahaya Omari Bawazir akachukua kipaza sauti na kuwaasa watu kwa kifupi, "Ndugu waalikwa bila shaka mmesikia kisa kizito kilicho pelekea ndoa isifungwe, hivyo hili liwe fundisho kwa wazeewengine wenye tabia mbaya kama alivyofanya Mzee Kidazu, tamaayake ya kutembea na "House-girl" wake leo imeleta aibu hapa, jamani angalieni misihadaike na mambo ya dunia, naomba hili lisirudiwe tena hii ni fedheha kubwa kwa mzee mwenzetu, tabia hii ilaaniwe kabisa. Iwe fundisho kwa wenginewenye tabia mbaya mimi naishia hpa na Mwenyezi Mungu ayafikishe katika nyoyo zetu na tuyafuate, tusikengeuke. MWISHO. |
YALIYOMO
TAHARIRI
Mkapa, Karume wapewa tiketi za CCM kugombea urais Kufuatia
kukamatwa kwa Sheikh Mbukuzi na Ricco:
HABARI
Amiri Mbukuzi ahojiwa na polisi Wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi watajwa USHAURI NASAHA
MAKALA
MAKALA
MAKALA
MAKALA
HOJA BINAFSI
Makala maalum ya Maulid
MAKALA
Habari za Kimataifaza Kimataifa Lishe
RIWAYA
MICHEZO
|
|
|
|
|