NASAHA
Na. 052 Jumatano Juni 14 - 20, 2000
Ukurasa wa mwanzo
Islam Tanzania
Matoleo yaliyopita
TAHARIRI
S.L.P. 72045, Dar es Salaam

NASAHA yatimiza mwaka mwaka mmoja

WIKI hii gazeti la NASAHA linatimiza mwaka mmoja tangu kuasisiwa na kuanza kutoka ambalo hutoka mara moja kwa wiki.

Toleo la kwanza la gazeti hili lilitoka Juni 15, 1999.

Awali ya yote tunamshukuru Mwenyezi Mungu kutujaalia fikra njema, ari na moyo kuweza kutoa nasaha kwa lengo la kujenga jamii ya waungwana badala ya mabaradhuli, jamii ya waadilifu badala ya wafujaji.

Aidha, tunawashukuru wasomaji wetu kwa ujumla wao kwamba michango yao - makala, barua, maoni n.k.- imesaidia kulifanya gazeti hili kuwa mahiri katika umri mdogo.

Katika kipindi hiki cha mwaka mmoja NASAHA haikuvuka kwa 'wasaa', bali ilikumbwa na misukosuko kadhaa. Hata hivyo hatusikitiki wala kujuta kwa misuksuko hiyo kwa vile imesaidia sana kutujenga na pia kutupa fundisho moja kubwa kwamba dawa ya misukosuko si kuikimbia bali ni kuikabili, na kwamba palipo na nia ya dhati watu wanaweza kuleta mabadilko waliyoyakusudia.

Tunaona fahari na muhimu kuufikisha uzoefu wetu huu kwa Watanzania wote hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu ambao unaweza kuleta mabadilko katika hali za wananchi.

Tulipoingia katika fani hii tuliahidi tutaifanya kazi ya kupasha habari, kuelimisha na kuburudisha kwa misingi ya taaluma hii lakini kikubwa bila kumchelea mtu fulani au kulichelea kundi la watu lenye nembo ya siasa, dini au vinginevyo.

Katika kipindi hiki cha mwaka mmoja tumejitahidi kuienzi ahadi yetu hiyo na leo tunairejea: tutaifanya kazi hii bila kujali hofu au vitisho vya yeyote bali kwa mujibu wa sheria zinazoitawala fani hii.

Hata hivyo, tutakuwa ni watu wenye kibri iwapo tutajiaminisha kuwa hatukufanya kosa lolote katika kipndi hiki cha majuma 52. Kukosea ni sehemu ya ubinadamu na kuomba radhi ni wajibu. Hivyo kwa yeyote ambaye tulimkosea, ama kwa kujua au hata bia ya sisi wenyewe kufahamu, tunaomba radhi.

Aidha, tunaahidi kuliboresha gazeti hili kuweza kukidhi mahitaji ya Watanzania kama wanadamu na, katika kutimiza azma hiyo, tunakiri kwamba michango ya wasomaji wetu inahitajika.
 

Juu
 

YALIYOMO
 

TAHARIRI
NASAHA yatimiza mwaka mwaka mmoja

Mkapa, Karume wapewa tiketi za CCM kugombea urais

CCM walilia kiti cha CUF

Kufuatia kukamatwa kwa Sheikh Mbukuzi na Ricco:
Viongozi wa Serikali  watakiwa kuacha udini dhidi ya Waislamu

HABARI
Mauaji ya Mwembechai: Hatimae inquest yafunguliwa

DC aishukuru Finland

Amiri Mbukuzi ahojiwa na polisi

Wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi watajwa

USHAURI NASAHA
Mapambano dhidi ya dhuluma ni ya kudumu

MAKALA
Dini na siasa haviwezi kutenganishwa

MAKALA
Mchango wa taasisi ya Dhiynurayn

MAKALA
Sayyidat Fatma:Jumuia iliyosimama dhidi ya dhulma 

MAKALA
Kupiga vita udini zisiwe kauli za kuendeleza udini dhidi ya Waislam

HOJA BINAFSI
Kwa Rafiki yangu Mpendakula

Makala maalum ya Maulid
Kumpenda Mtume Muhammad (s.a.w.)

MAKALA
CCM  na sera za maendeleo

Habari za Kimataifaza Kimataifa

Lishe 
Vyakula vitupatiavyo vitamini C

BARUA

MASHAIRI

RIWAYA
Mapinduzi ya fikra - 4 

MICHEZO
Ongara, Salvatory, Nteze, Mwansasu waenda Ulaya
Mokake aikosoa Yanga


   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: nasaha1420@yahoo.com

Ukurasa wa mwanzo
Islam Tanzania
Matoleo yaliyopita