NASAHA
Na. 052 Jumatano Juni 14 - 20, 2000
Ukurasa wa mwanzo
Islam Tanzania
Matoleo yaliyopita
HABARI ZA KIMATAIFA
 
 

Rais Assad wa Syria azikwa

  • Msimamo dhidi ya Israel kuendelea 


DAMASCUS,Syria.

Aliyekuwa Rais wa Syria marehemu Hafezal-Assad amezikwa jana baada ya kufariki Jumamosi iliyopita.

Bw. Assad ambaye alitawala kwa kipindi cha miaka 30 alijulikana kama simba wa Syria. 

Kabla ya mazishi maiti alizungushwa katika baadhi ya mitaa ya Damascus hadi kwenye kasri la wananchi kwa ajili ya viongozi mbalimbali kutoa heshima zao na kuaga. 

Huku maelfu ya wananchi wa Syria wakisindikiza jeneza, wengine wakipaza sauti za kilio watu kadhaa WALIPATWA NAMSHTUKO WA MOYO. 

Rais huyo atakumbukwa kwa sera zake dhidi ya dhuluma ya Israel huko mashariki ya Kati. 

Kabla ya umauti Assad ameshuhudia ushindi wa kikundi cha wapiganaji wa Kiislamu -Hizbullah kwa kuwaondoa Israel katika ardhi waliyoikalia kwa mabavu ya Lebanon. 

Kiongozi mtarajiwa atakayerithi wadhifa huo wa Urais akiongea na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Bibi Madelaine Albright amesisitiza kuwa sera ya Syria dhidi ya Israel itaendelea hadi milima ya Golan irudishwe kwa Syria. 

Israel iliiteka milima ya Golan katika vita kati yake na Syria mnamo mwaka 1967. 

Wakuu wa nchi mbalimbali kutoka nchi za Kiarabu na Afrika walihudhuria mazishi hayo isipokuwa mataifa ya Magharibi yalituma wawakilishi. 

Rais Assad aliyekuwa mtu muhimu katika suala la Amani Mashariki ya Kati,aliwahi kumwambia Rais Bill Clinton wa Marekani kuwa yeye si Rais Sadat au Yasir Arafat wa Palestina ambao aliwataja kuwa walifanya tabasamu na Israel katika kudai haki zao. 

Syria inayochukuliwa kuwa ni mlinzi wa Lebanon ina vikosi vya kijeshi huko vyenye idadi ya askari 35,000. 

Nchi hiyo yenye mchanganyiko wa raia wenye imani za dini ya Kiislamu, Kikristu na Kiyahudi ina idadi ya Waislamu asilimia tisini na nane. 

Viongozi waliohudhuria mazishi pia walichukua fursa ya kutambuana na mtoto wa Rais Assad Bashar ambaye ndiye anatarajiwa kuwa mrithi wa kiti hicho. 

Kamati ya mazishi ikitangaza taratibu za mazishi ilieleza kuwa maziko yatafanyika kijijini alikozaliwa Rais huyo kiasi cha kilomita 320 kutoka mji mkuu wa nchi hiyo Damascus. 

"Baada ya swala ya kumswalia maiti kwa majibu wa dini ya Kiislamu maziko yatakuwa kijijini kwake",ilisema taarifa hiyo. 

Mwili huo ulibebwa katika gari maalum laki jeshi katika safari yake ya mwisho kabla ya kutiwa ndani ya ndege kwenda Latakia kwa maziko. 

Baada ya mwili huo kufika Latakia ulibebwa katika gari la kivita hadi kijijini kwake Assad katika milima ya Alawite. Assad amezaliwa katika kijiji cha Qardaha. 

Swala za kumuombea maiti zilifanywa katika msikiti wa Naisa ambao ulipewa jina la Mama yake. 

Bwana Assad amezikwa katika makaburi ya kifamilia. 


Korea zafungua ukurasa mpya 



PIYONG YANG, Korea kaskazini.

Viongozi wa nchi za Korea ya Kaskazini na Korea ya Kusini wameazimia kufungua ukurasa mpya katika safari ndefu ya kuziunganisha nchi hizo baada ya kusambaratika mnamo mwaka 1948.

Hii inafuatia ziara ya Rais Kim Il Sung wa Korea ya Kusini kuwasili Korea ya Kaskazini mapema wiki hii katikaziara fupi. 

Kuhasimiana kwa nchi hizi kulifikia kilele mnamo 1948 zilipotengana kutoka Korea moja, na zaidi ukakasi wa chuki ulishika kasi na kufikia kupigana Vita mnamo mwaka 1950 na kumalizika 1953. 

Baada ya kuwasili mjini Piyong-Yang, Rais Kim Il Sung wa kusini alilakiwa na mwenyeji wake wa Kaskazini Bwana Kim Yong Il kisha kukumbatiana. 

China imeipokea ziara hiyo kwafuraha na kusema kuwa "tunaunga mkono hatua zote za maendeleo. 

Viongozi hao wa Korea katika mazungumzo yao ya awali wamesema kuwa wameazimia kufungua ukurasa mpya wa amani ya kudumu ili kuwaepusha Wakorea na vita. 

Korea ya Kaskazini ambayo kwa muda mrefu imetengwa na ulimwengu wa Magharibi ukiongozwa na Marekani kutokana na msimamo ya siasa za Kikomunisti zilizo asisiwa na Urusi iliyo sambaratika mwanzoni mwa miaka ya tisini na siasa zake za kikomunisti. 

Korea ya Kaskazini imekuwa ikipinga kuwepo kwa vikosi vya kijeshi vya Marekani huko Korea ya kusini, kwa madai kuwa inahujumiwa kwa mgongo wa ndugu na jirani yake. 

Nayo Korea ya Kusini inataraji kuwa huu ni mwanzo wa vikao vingine katika kuleta amani ya kudumu kwa uhakika zaidi katika safari ndefu ya kuungana. 

Korea ya Kusini imekuwa ikifuata sera za uchumi wa kibepari. 

Viongozi hao wametangaza kufungua njia za anga, maji na biashara. 

Nchi hizo ziko mbioni kufuata nyayo za Ujerumani ambayo iliwahi kuwa mataifa mawili yenye itikadi mbili tofauti, zile za kikomonisti na kibepari. 

Wachunguzi wa mambo ya kisiasa wanaeleza kuwa ukurasa huu mpya wa kuelekea Korea moja hauzifurahishi nchi za Magharibi hususan Marekani kwa kuhofia mustakabali wa maslahi yake huko kwa Wakorea wanaoelekea kuamka. 

Katika mkutano huo wa kihistoria, viongozi wa Korea hizo mbili wamezungumzia hatua mbali mbali za kuboresha uhusiano wao. 

Kwa miaka mingi, Korea ya Kaskazini na ile ya Kusini,zimekuwa na uhasama mkubwa, hivyo kukutana kwao kunaonekana kuwa ni hatua nzuri ya kuelekea kwenye uhusiano mzuri. 


Serikali hoi kwa Waislamu

MANILA, Philippines. 

Serikali ya Philippines ikiongozwa na Rais Joseph Estrada imefikwa na maji shingoni baada ya kuahirisha tena mazungumzo na wapiganaji wa Kiislamu wa kikundi cha Abu-Sayyaf. 

Wapiganaji hao wa Kiislamu wametoa masharti kwa serikali, masharti ambayo serikali ya Philippines imesema ni magumu na yanayohitaji kuangaliwa kwanza. 

Rais Estrada amewataka wapiganaji hao kuachana na dai lao la kutaka kuwepo kwa serikali ya Kiislamu Kusini mwa kisiwa hicho. 

Katiba ya Philippines ilianza kutambua rasmi sharia ya Kiislamu mnamo mwaka 1990. 

Kuanzia kipindi hicho Waislamu wa Philippines wamekuwa wakitekeleza sharia ya Kiislamu hususan zile za kijamii. 

Na hivi karibuni wameazimia kuutekeleza Uislamu katika kila nyanja ya maisha. 

Waislamu hao wa Philippines katika maelezo yao ya awali wameeleza kuwa Uislamu ni mfumo kamili wa maisha, hivyo ni budi utekelezaji ufanyike na si Uislamu wa nadharia. 

Mnamo miaka ya tisini kumekuwepo na vuguvugu ambalo limepambamoto kwa Waislamu sehemu mbali za ulimwengu kutaka kutekeleza sharia ya Kiislamu, yaani Qur'an na mwongozo wa Mtume Muhamad kuwa ndio katiba ya maisha yao. 
 

Juu
 

YALIYOMO
 

TAHARIRI
NASAHA yatimiza mwaka mwaka mmoja

Mkapa, Karume wapewa tiketi za CCM kugombea urais

CCM walilia kiti cha CUF

Kufuatia kukamatwa kwa Sheikh Mbukuzi na Ricco:
Viongozi wa Serikali  watakiwa kuacha udini dhidi ya Waislamu

HABARI
Mauaji ya Mwembechai: Hatimae inquest yafunguliwa

DC aishukuru Finland

Amiri Mbukuzi ahojiwa na polisi

Wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi watajwa

USHAURI NASAHA
Mapambano dhidi ya dhuluma ni ya kudumu

MAKALA
Dini na siasa haviwezi kutenganishwa

MAKALA
Mchango wa taasisi ya Dhiynurayn

MAKALA
Sayyidat Fatma:Jumuia iliyosimama dhidi ya dhulma 

MAKALA
Kupiga vita udini zisiwe kauli za kuendeleza udini dhidi ya Waislam

HOJA BINAFSI
Kwa Rafiki yangu Mpendakula

Makala maalum ya Maulid
Kumpenda Mtume Muhammad (s.a.w.)

MAKALA
CCM  na sera za maendeleo

Habari za Kimataifaza Kimataifa

Lishe 
Vyakula vitupatiavyo vitamini C

BARUA

MASHAIRI

RIWAYA
Mapinduzi ya fikra - 4 

MICHEZO
Ongara, Salvatory, Nteze, Mwansasu waenda Ulaya
Mokake aikosoa Yanga


   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: nasaha1420@yahoo.com

Ukurasa wa mwanzo
Islam Tanzania
Matoleo yaliyopita