NASAHA
Na. 052 Jumatano Juni 14 - 20, 2000
Ukurasa wa mwanzo
Islam Tanzania
Matoleo yaliyopita
HABARI 

Wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi watajwa 

  • Wengi wao ni Wakristo 


Na Mwandishi Wetu 

TUME ya Taifa ya Uchaguzi imetangaza majina ya wasimamizi wasidizi wakuu wa uchaguzi (Principal Assistant Returning Officers) kwa ajili ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, mwaka huu, ambapo Watanzania watapiga kura kuwachagua Rais wa Muungano, wabunge na madiwani.

Kwa mujibu wa taarifa iliyosambazwa na tume hiyo katika vyombo vya habari Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilifanya kikao chake Juni 9 mwaka huu na kuwateua watumishi kutoka serikali kuu na serikali za mitaa kuwa wasimamizi wasidizi wakuu wa uchaguzi huo utakaovishirikisha vyam vingi vya siasa. 

Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa zaidi ya asilimia 80 ya wasimamizi hao wa uchaguzi wana majina yenye kuashiria kuwa ni wafuasi wa dini ya Kikristo. 

Orodha ya kwanza ya wasimamizi wakuu wa uchaguzi (Principal Returning Officers) iliyotangazwa miezi michache iliyopita ililalamikiwa na Waislamu kwa madai kuwa zaidi ya asilimia 90 ya walioteuliwa walikuwa ni Wakristo. 

Hata hivyo si tume ya uchaguzi wala serikali iliyodiriki kujibu kadai hayo ya Waislamu. 

Aidha, mara kadhaa, Rais Benjamin William Mkapa amekuwa akikemea udini hapa nchini. Hivi karibuni, akizungumza katika Mkutano Mkuu Maalum wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Mkapa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho tawala, alisema serikali yake haitavumilia ubaguzi wa raia kwa misingi ya dini, kabila au jinsia. 

Huko nyuma Waislamu wamewahi kupeleka kwa Rais Mkapa madai yao yakiwemo ya kubaguliwa kwa msingi wa dini. Hata hivyo Waislamu nchini wanadai kwamba malalamiko yao yamepuuzwa na Mhe. Rais. 
 

Juu
 

YALIYOMO
 

TAHARIRI
NASAHA yatimiza mwaka mwaka mmoja

Mkapa, Karume wapewa tiketi za CCM kugombea urais

CCM walilia kiti cha CUF

Kufuatia kukamatwa kwa Sheikh Mbukuzi na Ricco:
Viongozi wa Serikali  watakiwa kuacha udini dhidi ya Waislamu

HABARI
Mauaji ya Mwembechai: Hatimae inquest yafunguliwa

DC aishukuru Finland

Amiri Mbukuzi ahojiwa na polisi

Wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi watajwa

USHAURI NASAHA
Mapambano dhidi ya dhuluma ni ya kudumu

MAKALA
Dini na siasa haviwezi kutenganishwa

MAKALA
Mchango wa taasisi ya Dhiynurayn

MAKALA
Sayyidat Fatma:Jumuia iliyosimama dhidi ya dhulma 

MAKALA
Kupiga vita udini zisiwe kauli za kuendeleza udini dhidi ya Waislam

HOJA BINAFSI
Kwa Rafiki yangu Mpendakula

Makala maalum ya Maulid
Kumpenda Mtume Muhammad (s.a.w.)

MAKALA
CCM  na sera za maendeleo

Habari za Kimataifaza Kimataifa

Lishe 
Vyakula vitupatiavyo vitamini C

BARUA

MASHAIRI

RIWAYA
Mapinduzi ya fikra - 4 

MICHEZO
Ongara, Salvatory, Nteze, Mwansasu waenda Ulaya
Mokake aikosoa Yanga


   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: nasaha1420@yahoo.com

Ukurasa wa mwanzo
Islam Tanzania
Matoleo yaliyopita