|
Na. 052 Jumatano Juni 14 - 20, 2000 |
|
|
|
|
|
Na Mwandishi Wetu BAADA ya kupoteza kiti cha Uenyekiti wa mtaa wa Boma viongozi wa kata ya Boma wametoa malalamiko yao kupinga matokeo ya uchaguzi wa marudio ambao mgombea wa CUF Bw. Madadi Hassan Maringo aliibuka mshindi . Uchaguzi huo umerudiwa kwamara ya pili baada ya CCM kushindwa katika uchaguzi wa awali na hivyo kukata rufaa iliyokusudia na kupeleka uchaguzi huo kurudiwa ambapo CCM ilishindwa tena. Viongozi wanaohusika na chaguzi hizo akiwemo mwenyekiti wa kikao kilichojadili malalamiko ya chama tawala juu ya kiti hicho wiki iliyopita ( Juni 6,2000) kwenye ofisi ya kata , Afisa taaluma manispaa Bw. Mpessa na afisa utumishi manispaa Bw. Mhina wamekiri kupokea malalamiko ya CCM. Akiongea na gazeti hili afisa utumishi wa manispaa ya morogoro Bw. Mhina alisema " ni kweli tumepokea malalamiko hayo ambayo kisheria hutolewa baada ya siku tatu toka chaguzi husika na kujadiliwa wakati wowote tupatapo nafasi ndani ya siku 60 baada ya uchaguzi" Alipotakiwa na mwandishi wa habari hizi aeleze kwa kuwa na lalamiko la chama hicho Bw Mhina alisema kuwa taarifa kamili itatolewa na Mkurugenzi wa manispaa Bw Paul Baruti katika kipindi cha siku chache zijazo ." mimi si msemaji na pia ni vyema tukasubiri ripoti rasmi ya mkurugenzi" Gazeti hili lilimtafuta mwenyekiti wa muda wa uchaguzi unaolalamikiwa Bw kassim malumbo ambapo inadaiwa katika kikao hicho cha malalamiko aligoma kuzungumza lolote kwa kukitaka kikao kitoe vifungu vya sheria za uchaguzi zinazohalalisha kuwepo kwa kikao hicho. " nilipofika katika kikao hicho niliulizwa maswali mawili , kwanza juu ya muda wa kumaliza uchaguzi na pili sababu ya kijana mmoja (mtoto) Sharif Matengo kuzuiwa kupiga kura" alisema awali kwenye uchaguzi huo wa mtaa unaoelekea Ikulu ndogo na maarufu kama "MKUNAZINI" uchaguzi huo ulimalizika saa mbili usiku, ambapo wazazi wa mtoto huyo walishindwa kutoa uthibitisho wa vyeti vya kuzaliwa ili kuoanisha umri halisi wa mtoto huyo. Baada ya Bw. Kassim kutoa hoja hizo mbele ya kikao hicho kilichohudhuriwa na wajumbe kdhaa wa CCM chini ya ofisi ya taaluma ya manispaa , katibu mtendaji kata wa mji mkuu mama mlaki, makada wa CCM Bw Josephat Lugaimukamu, Issac manyama , Sudi Kiroboto, Bw Simba pamoja na mgombea wa chama hicho Hassan Mlapakolo, Mwenyekiti wa kikao hicho alikataa hoja ya Bw Kassim na kumtaka ajibu maswali aliyeulizwa ambapo Bw huyo hakufanya hivyo na kuamua kuondoka . Alipoulizwa na Nasaha juu ya uamuzi wake huo, Mwenyekiti huyo wa muda bw Kassim alisema asingeweza kwenda kikao asichofahamu uhalali wake kama taratibu za uchaguzi wa viongozi wa vijiji vitongoji na mitaa za mwaka 1999 na sheria ya serikali za mitaa namba nane ya 1988 ilivyoweka wazi. Bw. malumbo aliendelea kusema kwamba katika taratibu za uchaguzi GN. 255 / 199(9) kifungo cha 18 (1) kinasema malalamiko kuhusu uendeshaji wa uchaguzi yatapelekwa kwa Mkurugenzi na yatasikilizwa na kamati ya malalamiko iliyoundwa kwa mujibu wa taratibu ya 11 katika siku tatu tangu siku ya uchaguzi. Ameendelea kusema kuwa na kifungu cha 18 (12) kinasema : muda wa kusikiliza na kutoa uamuru kuhusu malalamiko ya uendeshaji wa uchaguzi hautozidi siku saba tangu siku ya uchaguzi "leo ni zaidi ya siku 29 tangu uchaguzi sasa waniita nikafanye nini? Na ninapohoji uhalali wa kikao najibiwa kuwa hiyo si kazi yako. Bali jibu yale utakayoulizwa " amehoji Bw malumbo. Gazeti hili halikuishia hapo bali lilimtafuta aliyekuwa mgombea wa CCM alieshindwa katika kinyang'anyiro hicho mara mbili Bw hassan Mlapokolo ambapo alikubali kuwa chama chake (CCM) kimelalamikia matokeo hata hivyo alikataa kuelezea malalamiko hayo kwa madai kwamba si msemaji wa chama hicho. " Nenda kamuone mama Fatma au mheshimiwa Shamte pale mji mkuu watakupatia maelezo kamili, mimi si msemaji wa chama" alisema Bw mlapakolo aliyekuwa mchezaji wa zamani wa timu ya soka ya simba ya jijini. Gazeti hili lilifika ofisi ya katibu kata CCM
mji mkuu ili kupata ufumbuzi zaidi wa suala hili ambapo ofisa wake mama
fatma alisema kwamba huu siyo wakati muafaka wa kuzungumzia suala hilo.
" ni mapema mno kulizungumzia jambo hili, wakati utakapofika tutalizungumzia
bayana na wala hakuna shaka alisema"
|
YALIYOMO
TAHARIRI
Mkapa, Karume wapewa tiketi za CCM kugombea urais Kufuatia
kukamatwa kwa Sheikh Mbukuzi na Ricco:
HABARI
Amiri Mbukuzi ahojiwa na polisi Wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi watajwa USHAURI NASAHA
MAKALA
MAKALA
MAKALA
MAKALA
HOJA BINAFSI
Makala maalum ya Maulid
MAKALA
Habari za Kimataifaza Kimataifa Lishe
RIWAYA
MICHEZO
|
|
|
|
|