|
Na. 052 Jumatano Juni 14 - 20, 2000 |
|
|
|
|
|
Kupiga vita udini zisiwe kauli za kuendeleza udini dhidi ya Waislam KATIKA mkutano mkuu maalum wa CCM uliomalizika hivi karibuni mjini Dodoma, pamoja na mambo mengine, Rais Ben Mkapa alisikika akikemea vikali hoja ya baadhi y awatu wanaotaka kuligawanya taifa letu kwa misingi ya dini. Katika mkutano huo ambao ulimchagua tena Mkapa kugombea urais kwa tiketi ya CCM, Rais alisisitiza kwamba atatumia nguvu na uwezo wake wote kuzuia mgawanyiko wa jamii ya Tanzania kwa misingi ya kidini. Mwandishi KONDO SEFU anaelezea zaidi. KWA dhati ya moyo, napenda kumpongeza Mhe. Mkapa kwa kauli yake hii ya msingi ambayo ameitoa wakati na mahali muafaka kabisa. Ni mahali muafaka kwa vile ameitoa kauli yake mbele ya viongozi wenzake wote. Na wale viongozi wasiokuwepo wamesikia kauli hii kupitia vyombo vya habari kama vile redio na runinga. Ni wakati muafaka pia kwa vile Rais ana ushahidi kwamba migawanyiko ya kidini imeanza kujitokeza.Hivyo basi, kama rais hana budi kukemea mgawanyiko huu kwa vile matokeo yake ni hatari na maangamizi ya jamii yetu ambayo tayari imeshajijengea heshima ya umoja na mshikamano. Pamoja na pongezi zangu napenda pia kutoa wasi wasi wangu juu ya utekelezaji wa kauli hii.Nasema hivyo kwa sababu mbili. Sababu ya kwanza ni kwamba kauli kama hii ya Mhe. Rais siyo ya kwanza. Kiasi kwamba imekuwa kama wimbo. Na sababu ya pili ni kwamba hali ilivyo nchini , udini umekuwa ukishamiri siku hadi siku. Jambo linalotisha zaidi udini unaonekana kuwepo ndani ya jumuia, taasisi, wizara na mashirika ya Serikali. Aidha, udini umekuwa ukijionesha katika mitazamo ya baadhi ya viongozi wa chama tawala. Labda nitoe mifano michache kuthibitisha wasi wasi wangu. Baadhi ya viongozi wengi wa chama tawala ni miongoni mwa wale walioanza kudai kwamba CUF ni chama cha kidini. Madai haya yamepokelewa nas ehemu kubwa yv vyombo ya habari ambavyo vimekuwa vikiyasambaza nchini kote. Madai hayo yamekuwa yakisem akwamba chama cha CUF ni chama cha Waislamu na hivyo ni chama cha kidini. Vigezo vikubwa vinavyotolewa ni kwamba katika mikutano ya CUF wanancji wengi wanaohudhuria mikutano hiyo huonekana wamevaa mavazi ya Kiislam kama vile kanzu na kofia kwa wanaume, nguo ndefu na mitandio (hijab) kwa wanawake. Ni dhahiri kwamba mtazamo huu wa CCM na Serikali yake ni mtazamo wa udini.Tena, udini dhidi ya Waislamu. Tanzania ni nchi yenye watu wa makabila na dini mbali mbali. Wengi ni wafuasi wa Uislamu naUkristo Mikutano ya kisiasa huwa haihutubii wala kuhubiri namna ya kumpeleka mwanchi peponi au mbinguni. Huwa inahutubia sera za chama cha siasa na yale yanayomuwajibikia mwanachama na mwananchi kuyatekeleza ili chama chao kipate kuingia madarakani. Lakini cha kushangaza viongozi hawa wa CCM wanapoitazama mikutano ya CUF inaelekea huwa hawana wanachokiona wala kukisikia isipokuwa huwatazama watu waliopo na kuzichambua dini zao. Na wanapofanya hivyo inaonesha kwamba nafsi zao huchukizwa wanapoona Waislamu wamehudhuria au kuhutubia mikutano hiyo. Hivi ndiyo baadhi ya viongoai hao wa CCM na serikali yake wanavyowadhihirishia Watazania chuki zao na udini walio nao dhidi ya Uislamu. Kwa sababu, ni vipi mtu aende mahali penye hadhara isiyokuwa ya kidini akawatazame watu kwa dini zao.Ni wazi kuwa huo ndiyo mtazamo wake. Mtazamo wa chuki dhidi ya Waislam. Anachukizwa kuonaWaislamu wamo katika siasa. Hataki kuona Waislamu wanashiriki katika siasa japo ni haki yao kama Watanzania. Mtazamo huu ni mtazamo wa kidhalimu.Ni mtazamo wa udini uliyolenga kuwadhulumu Waislamu kwa sababu tu ya dini yao. Mtazamo huu walio nao viongozi hao hauanzii na kuishia kwenye shughuli za kisiasa pekee. Upo pia katika idara na taasisi za serikali na mashirika ya umma.Huko nako vile vile wanachukizwa wanapowaonaWaislamu wanafanya kazi au kushika nafasi za madaraka. Chuki hizo za udini dhidi ya Waislam zimedhihiri vile vile katika utendaji wa vyombo mbali mbali vya dola. Mfano ulio wazi zaidi ni dhulma waliofanyiwa Waislamu kuhusu suala la Mwembechai. Katiba ya nchi inayompa Mtanzania haki yake ya msingi kama binadamu na sheria zilizopo nchini zilizotungwa na bunge zinasema wazi kwamba aliyeuliwa na aliyekufa mikonini mwa polisi sharti afanyiwe uchunguzi wa kimahakama ujulikanao kwa jina la INQUEST. Pamoja na kuwepo kwa haki hiyo viongozi wa serikali ya CCM iliyopo madarakani wamekataa kulitekeleza hilo. Kwa kuwa haki hizo zimekuwa zikitolewa na kutekelezwa pale ambapo masuala hayo yanapowagusa wasiyokuwa Waislam, ni wazi Waislam wamekataliwa haki hiyo kutokana na chuki za udini. Wailsam wamekwishatoa ushahidi mwingi na wa kutosha kuhusu jinsi wanavyodhulumiwa haki zao mbali mbali kama Watanzania; kwa sababutu ya wao kuwa Waislam. Ushahidi huo umekwishafikishwa na viongozi madhubuti wa Waislam kwa kauli na maandishi, mbele ya Rais wa nchi. Kushindikana kuondolewa dhuluma hizo dhidi ya Waislamu mpaka hivi leo tayari kumeanza kuleta athari kubwa nchini. Hivi sasa Waislam na wao pia wameambukizwa na mtazamo huo mbovu wa baadhi ya viongozi mabaya wa CCM Kutokana na kuambukizwa huko, Waislamu vile vile wamelazimika kuwatazama CCM kwa dini zao; hususan viongozi na mwenendo wao wa uongozi katika chama hicho na serikali yake. Wanasema kwamba, katika maeneo mengi ya vyeo vya juu ndani ya chama hicho na serikali yake wamejaa Wakristo. Vile vile wanasema Maaskofu wa Makanisa hasa ya Kikatoliki, wamekuwa wakisikilizwa na CCM na serikali yake katika kutoa maamuzi yanayowaathiri Waislam hapa nchini. Na hilo Waisamu wanalitaja kwa kuonesha ushahidi wa kimaandishi uliomo katika vitabu vya Jan Van Bergen na Dk. John Sivalon ambaye ni Padri wa Kikatoliki. Katika vitabu hivyo ipo ahadi iliyotolewa na uongozi wa juu wa Serikali ya Tanzania wa kulipa kanisa Katoliki upendeleo katika nyanja mbali mbali nchini. Upo ushahidi vile vile katika vitabu hivyo unaoonesha kauli ya Kanisa Katoloki ya juu wanavyoutazama Uislam kwa jicho la uaduia. Yapo pia maandishi yanayoonesha jinsi Kanisa hilo lilivyojenga mtandao wake wa kisiasa na viongozi wa chama na serikali. Imeoneshwa vile vile jinsi kanisa lilivyopenyeza waumini wake katika nafasi mbalimbali za juu serikalini na mashirika ya umma. Pamoja na udini huo, Waislam wanadai katika malalamiko yao kwamba hata hatua za kupunguzwa wafanyakazi viwandani kumewalenga Waislam wengi kuliko watu wa dini nyingine. Inadaiwa vile vile katika uuzaji wa mashirika ya umma wawekezaji wengi wanaouziwa mashirika hayo huwa kuna mtazamo wa kiudini na ushawishi kwa wawekezaji hao kuajiri Wakristo wengi kuliko Waislam. Kwa kuwa msingi ya utawala mbovu na ubadhilifu wa matumizi ya madaraka ya kuongoza nchi hutokana na viongozi katika chaguzi kama hizi zilizopo nchini mwetu chini ya mfumo wa nyama vingi, Waislam wanadai kuwa kuachia mfumo wa demokrasia wa uchaguzi huru na wa haki unaweza kutoa fursa kwa vyama vingine vyenye kutetea haki na usawa kwa wananchi wote, kupata fursa ya kuingia madarakani. Hivyo, udini wa baadhi ya viongozi hao wa CCM, na serikali yake dhidi ya Waislam katika nyanja ya siasa, una lengo la kuwazuia viongozi waadilifu watakaoleta utawala wa haki kwa watu wote, wasiingie madarakani, ili dhuluma hii wanavyofanyiwa Waislamu ipate kuendelea. Moja ya hoja zinazotolewa kuonyesha mfano wa madai hayo ya udini dhidi ya Waislam ni uteuzi wa wasimamizi wa uchaguzi ambao kwa zaidi ya asilimia 90 ni Wakristo. Inafaa ikumbukwe kwamba idadi kubwa ya Waislam ndiyo iliyoongoza chama cha TANU kwa hali na mali hadi kupatikana uhuru. Waislam hawakuwatazama wakoloni kwa rangi yao wala kwa dini yao ya Kikristo. Walipambana nao kama madhalimu waliokuwa wakiwanyima haki zao mbali mbali ikiwemo ya kuwatawala kwa mabavu. Waislam hawakuwa na udini, kwa jambo hilo hakuna shahidi mkubwa kama kauli ya Mwalimu Nyerere aliyekiri kwamba Waislam walimpokea na kukaa naye katika siasa kama mwenzao. Hivyo bila shaka sasa inajulikana nani mwenye udini katika nchi hii. Na nani anayedhulumiwa kwa misingi ya udini. Na nani vile vile aliyeanzisha udini. Na hivyo ni nani anayehatarisha usalama na amani ya nchi hii kwa udini wake. Katika kuzingatia yote hayo ningependa kurudia
maoni yangu niliyoyatanguliza hapo awali kwamba naunga mkono juhudi za
kupiga vita udini lakini kauli hizo za kupiga vita udini ziwe za kweli
na zisiwe hoja na visingizio vya kuwaandama zaidi Waislamu na kuwadhulumu
haki zao kwa misingi ya udini.
|
YALIYOMO
TAHARIRI
Mkapa, Karume wapewa tiketi za CCM kugombea urais Kufuatia
kukamatwa kwa Sheikh Mbukuzi na Ricco:
HABARI
Amiri Mbukuzi ahojiwa na polisi Wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi watajwa USHAURI NASAHA
MAKALA
MAKALA
MAKALA
MAKALA
HOJA BINAFSI
Makala maalum ya Maulid
MAKALA
Habari za Kimataifaza Kimataifa Lishe
RIWAYA
MICHEZO
|
|
|
|
|