|
MASHAIRI
CUF ni chama cheupe
Leo nimeshika bango, wazi kuwatangazia,
Kuwashushua waongo, CUF wanopakazia,
Mashushu visebengo, CUF tiki kwa jalia,
CUF ni chama cheupe, HAKI kimejijengea.
Karibuni wote ndani, CUF ndani kuingia,
KunaHAKI na AMANI, karibu Watanzania,
CUF huru si utani, haki tupu chapigia,
CUF ni chama cheupe, HAKI kimejijengea.
Kinao wa zote fani, wasomi walotimia,
Kwa uchachemfanoni, wachumi na inginia,
Walimu walo makini, HAKI wanopigania,
CUF ni chama cheupe, HAKI kimejijengea.
Jama kinginesioni, bora kilichosalia,
CUF pekenambawani, USAWA chapigania,
Kututoadhulmani, na hakini kuingia,
CUF ni chama cheupe, HAKI kimejijengea.
Mwajua niaye nini? “CUF ilojipangia,
Kfuta umasikini, ukubwa dhuluma pia,
Mama zetu kiungeni, rahani tuje ingia,
CUF ni chama cheupe, HAKI kimejijengea.
Cheupe sio cha dini, upemba na ukabila,
Cheupe kipo hakini, dhulma ya chembe bila,
CUF ni chama makini, zingine ni zao hila,
CUF ni chama cheupe, HAKI kimejijengea.
Sio chama kibaguzi, sifa kilo jiwekea,
Walasio kichochezi, haki kimejijengea,
Wakweli wamageuzi, mkija chawapokea,
CUF ni chama cheupe, HAKIkimejijengea.
Ona wakeviongozi,dini zote watimia,
Lengo kufikishadozi, kwa pamoja kuchangia,
Leo vipiwajembuzi, FITINA kukitilia,
CUF ni chama cheupe, HAKI kimejijengea.
Wacha niwajulisheni, kebeni muweze jua,
Alofuzu uchumini, huyo wa kwanza kujua,
LIPUMBAalo makini, Mwenyekiti CUF jua,
CUF ni chama cheupe, HAKI kimejijengea.
Wengine ni JULIASI, bwana SAMBAMBA mwane,
Na mama alomwepesi mugishi mwiba kinae,
Atiki katia nyusi, kusanga tumbo, kinae,
CUF ni chama cheupe, HAKI kimejijengea.
Kamanda wake SHAIBU, ngangari mwarobaini,
Kamanda aso aibu, hasa awapo hakinini,
Hongera kama Shaibu, wafuasitu nyumbani,
CUF ni chama cheupe, HAKI kimejijengea.
Kina mama upandeni, kwa waka moto Bungeni,
MAGIMBI kimewapeni, kuwaongoza Bungeni,
Mama ninamuamini, FATUMA moto hakini,
CUF ni chama cheupe, HAKI kimejijengea.
Kiuchache toshekeni, CUF ilivyo jueni,
Vijana nguvu wapeni, kwao umoja ungeni,
Mimi mwisho shairini, naasa CUF dumuni,
CUF ni chama cheupe, HAKI kimejijengea.
Almasi H.Shemdoe,
“Tund ala Matumaini”,
Dar es Salaam.
Rais mtarajiwa
Lipumba ndiwe kinga, Bwana wa kuteuliwa,
Kila ovu walipinga, Tusije kuonelewa,
Hakuna la kukutinga, shida za watu wajuwa,
Rais mtarajiwa, Tanzania wangojewa.
Ulipokee shairi, moyoni kufurahiwa,
Ulisome kwa fahari, kila baya kuelewa,
Uelewe ya hatari, wananchi twatendewa,
Rais mtarajiwa, Tanzania wangojewa.
Leo ndiyo siku yako, kilio unatetewa,
Na hatujuwi twendako, jinsi tunavyochukiwa,
Kilio kifike kwako, Rais mtarajiwa.
Rais mtarajiwa, Tanzania wangojewa
Inatutia machungu,nchini kubaguliwa,
Yakaliwa kwa majungu, wenyeji twadhulumiwa,
Kubaguliwa kuchungu, kama mtoto na ziwa,
Rais mtarajiwa, nchini kote wangojewa.
Ufukara kutufika, si bure twakamatiwa,
Kila tukitutumuka, twazidi kushindiliwa,
Hatuwezi kunyanyuka, hawa wasipotolewa,
Rais mtarajiwa, Tanzania wangojewa.
Subira yavuta heri, cha mbali karibu huwa,
Lakini mbona hatari, tunazidi kutesewa,
Tunateshwa kama NGIRI, mikuki kupigiliwa,
Rais mtarajiwa,Tanzania wangojewa.
We! Lipumba msifika, mtenda yaliyo sawa,
Kila siku watajika, mfano maji ya kunywa,
Tanzania watajika, kwa busarayo na pawa,
Rais mtarajiwa, Tanzania wangojewa.
Ututoe wasiwasi, ya nchi kufanikiwa,
Twazidi fanywa mafisi, mifupa tu kutupiwa,
Na Mola katuumba, tupeane haki sawa,
Rais mtarajiwa, Tanzania wangojewa.
Elimu yako adimu, wachache waliopewa,
Kila kilicho muhimu, tunaomba kuambiwa,
Na usiache hatamu, tusije kuparamiwa,
Rias mtarajiwa, Tanzania wangojewa.
Mola ulokamilika, mjalie mtarajiwa,
Mjaze yalo baraka, “Lipu” wetu, mridhiwa,
Haki zetu kuzisaka, za wanyonge na wakiwa,
Rais mtarajiwa,Tanzania wangojewa.
Nahodha mwenye elimu, shika sukani mashuwa,
Shabani ndiye makamu,nyota inayo ng’ariwa,
“Furahini wanakafu, shangilio la ubingwa,”
Rais Mtarajiwa,Tanzania wangojewa.
Said M.Buweta,
S.L.P. 33626,
Dar es Salaam.
Dhuluma si njema
Ya ilahi yakarima, nakuomba l-wahabu,
Niwezeshe ya Rahima, niyaseme bila tabu,
Niuelezee umma, yale yanayotusibu,
Tuiepuke dhuluma, tusije tukaharibu.
Tusije tukaharibu, ikatufika laana,
Laana iso sababu, kuepa yawezekana,
Dawa yake mujarabu, kujiweka mbali sana,
Hatutofikwa na tabu, adhabu zikatubana.
Kumengia kashikashi, hapana pa kuegama,
Watu mekuwa shawishi, kusimamia dhuluma,
Umewashika utashi, kuleta ya uhasama,
Wanaufanya ubishi, hawaitaki salama.
Dhuluma imeenea, haina mfano wake,
Kila pembe zungukia, watu mejaa makeke,
Dhuluma waogelea, hata khofu siwashike,
Mbizi wanaizamia, hawajali njia zake.
Hawajali njia zake, zile wanazopitia,
Mradi yao ya wake, ya wenzao kupotea,
Haki za watu zishuke, zao juu kupepea,
Furaha wafuarahike, wangine wanaumia.
Haki imewekwa kando, watu meshika batili,
Wanahusudu vishindo, wenzao kuwakatili,
Wanafuata mkondo,walofanya majahili,
Wanaona ndio mwendo, mzuri wa kukabili.
Wamesahau wengine, waangalia ya kwao,
Wanahusudu unene, unawatia pumbao,
Hata wengi wasonone, hawana habari nao,
Bali ya kwao yafane, hilo ndilo tarajio.
Hakika ya watu hao, dhuluma wamebobea,
Kudhulumu vya wenzao, yao kuwanyookea,
Kutwa wako mbiombio, haki wanazikwapua,
Wanazifanya za kwao, haya wameziondoa.
Wanadhulumu bayana, mbele ya kadamuasi,
Uongo kwao kunena, hawaoni wasiwasi,
Zimewajaa khiyana, tabia za kibilisi,
Vya watu kuvitafuna,ili wapate ukwasi.
Hawana hata kificho, sasa wanatanafasi,
Watenda kimachomacho, kugombania fulusi,
Wakipate watakacho, hata kama kwa uasi,
Ili mradi kwa hicho, yao yanaenda kasi.
Dhuluma imeenea, wachache wafaidika,
Wengi wanaangamia, hawanapo pa kushika,
Vilio vingi walia, haki zao kuzitaka,
Lakini vinaishia, hawana pa kupeleka.
Wale wategemeao,roho zao mechafuka,
Huwa ni furaha kwao, wenzao wakiteseka,
Mesinyaa nyoyo zao, ukatili mezisika,
Waendekeza ya kwao, wanyonge wanyanyasika.
Lakini na waelewe, kudhulumu si hazina,
Dhuluma ina mwishowe, itakuja kuwabana,
Kamasi hapa wajue,kesho mbele ya Rabana,
Wasijepiga mayowe, mateso wakiyaona.
Freshi wataipata, wakome udhulumati,
Watabakia kujutia, umeshapita wakati,
Dunia wataiita, imefikia tamati,
Wasiwe pa kukamata, itabaki ati ati.
Dhuluma katu si njema, ndugu zangu nawambia,
Inakimbiza neema, mbali zikatokomea,
Na maisha ya salama, hayakawi kukimbia,
Utabaki uhasama, uhasidi na umbea.
Sihaba,
Dar es Salaam.
|
YALIYOMO
TAHARIRI
NASAHA yatimiza mwaka mwaka
mmoja
Mkapa,
Karume wapewa tiketi za CCM kugombea urais
CCM walilia
kiti cha CUF
Kufuatia
kukamatwa kwa Sheikh Mbukuzi na Ricco:
Viongozi
wa Serikali watakiwa kuacha udini dhidi ya Waislamu
HABARI
Mauaji
ya Mwembechai: Hatimae inquest yafunguliwa
DC aishukuru
Finland
Amiri
Mbukuzi ahojiwa na polisi
Wasimamizi
wasaidizi wa Uchaguzi watajwa
USHAURI NASAHA
Mapambano
dhidi ya dhuluma ni ya kudumu
MAKALA
Dini na
siasa haviwezi kutenganishwa
MAKALA
Mchango
wa taasisi ya Dhiynurayn
MAKALA
Sayyidat
Fatma:Jumuia iliyosimama dhidi ya dhulma
MAKALA
Kupiga
vita udini zisiwe kauli za kuendeleza udini dhidi ya Waislam
HOJA BINAFSI
Kwa Rafiki
yangu Mpendakula
Makala maalum ya Maulid
Kumpenda
Mtume Muhammad (s.a.w.)
MAKALA
CCM
na sera za maendeleo
Habari
za Kimataifaza Kimataifa
Lishe
Vyakula
vitupatiavyo vitamini C
BARUA
MASHAIRI
RIWAYA
Mapinduzi
ya fikra - 4
MICHEZO
Ongara, Salvatory, Nteze, Mwansasu
waenda Ulaya
Mokake aikosoa Yanga |