NASAHA
Na. 052 Jumatano Juni 14 - 20, 2000
Ukurasa wa mwanzo
Islam Tanzania
Matoleo yaliyopita
USHAURI NASAHA 

Mapambano dhidi ya dhuluma ni ya kudumu

JAMII ya binadamu imejengwa juu ya msingi wa mapambano. Mapambano haya huwa ni dhidi ya mazingira ili kupata maisha bora zaidi na pia dhidi ya kikundi kinachowadhulumu wenzao katika mgao unaotokana na matunda ya ushindi wa binadamu dhidi ya mazingira.

Mwandishi KHADIJA IDDI anaelezea zaidi.

HAPA Tanzania aina hizi zote za mapambano zipo na zinaendelea. Kama binadamu Watanzania wamepambana na mazingira yao na matunda ya mapambano hayo japo haba lakini yamepatikana. Mapambano haya yamemwondoa mkoloni na hatimaye kuondoa ukiritimba wa CCM katika siasa. 

Aina hii ya mapambano kwa kuwa ni ya kudumu bado inaendelea. Kwa bahati mbaya lipo kundi dogo la watu ambalo wanadhani huwa wana haki zaidi na uhuru uliopatikana kwa jasho la wengi na kuwa japo sasa ipo demokrasia ya vyama vingi lakini wao wana haki zaidi katika mfumo huo kuliko wenzao. 

Kuwepo kwa dhana hii ya kikundi fulani kidogo cha watu kudhani kuwa lina haki zaidi kuliko wengine hapa nchini ndicho kinachozaa aina hii ya pili ya mapambano. Mapambano dhidi ya wanaokandamiza wenzao ambayo huendeshwa na kugharimiwa na wale wanaokandamizwa. 

Yapo matukio kadhaa yanayodhihirisha kuwepo kwa mapambano hayo hapa nchini. Mfano wa haya ni kauli za viongozi wa dini ya Uislamu dhidi ya serikali kuwa inawabagua Waislamu. Maandiko mbalimbali ya Maskofu ya kuikosoa serikali na kauli za viongozi wa serikali za kukanusha shutuma dhidi yao. 

Kwa sasa mapambano haya yana sura ya kisiasa. Tayari Waislamu nchini kama kundi la waathirika wanatangaza hadharani kuinyima kura CCM chama kinachonasibishwa na shutuma za kuendesha sera zisizo rasmi za kuwabagua,kuwatenga na kuwadhulumu Waislamu. Pia kuna ishara kuwa baadhi ya mikoa na makabila nchini wananasibisha kuwa kwao duni kielimu, uchumi na huduma za jamii na sera za CCM. Kwa ujumla katika mapambano haya yenye sura ya kisiasa waathirika ama kwa dini, kabila au mikoa yao wanachukuwa hatua mbalimbali ikiwa ni pamoja na kujiunga na vyama vya upinzani. 

Mapandano ya aina hii ni mazuri kwani ni ya wazi na kamwe hayafanyiki kwa siri. Yanampatia fursa anayetuhumiwa kujirekebisha na anayeonekana huenda atakuwa afadhali anapewa fursa ya kujituma kutokana na yale yaliyomfanya mwezake kukosa imani ya wananchi. 

Jambo linalofaa kufahamika hapa na hivyo basi kupasa ushauri hasa kwa wale wanaodai kuwepo katika harakati za ukombozi ni kuwa kipimo cha mafanikio siyo matokeo ya kura zinazopigwa kila baada ya miaka mitano. Kipimo hasa cha mafanikio ya mapambano dhidi ya dhalimu ni pale anapoondoka dhalimu. Jambo hili halipangiwi muda wala gharama zake si rahisi kukadirika. 

Wanaopambana ni lazima wafahamu na kuzingatia lengo la kumwondoa dhalimu kuwa ni kuleta uadilifu. Wenye nia ya kumuondoa yule anayewebagua ili wao washike nafasi hizo wapate kuwabagua wengine watambue wazi kuwa nao pia wataitwa madhalimu na wananchi hawatakawia kuwatambua na kuwatangazia vita. 

Pili, lazima wanaopambana kuondoa udhalimu na kuleta uadilifu utakaosimamia fursa sawa kwa wote wakubali kuwa watapambana hadi udhalimu utokomee. Endapo wataishia katikati basi wajue wamepoteza nguvu zao bure na kuwa dhalimu atawadhulumu zaidi kuliko hapo awali. 

Hii ni kwa sababu tabia ya dhalimu ni kuwapenda wale ambao wanadhulumiwa bila kujitambua na huku wanaendelea kumpenda, kumchekea na kushirikiana naye. Yeyote kutoka katika kundi la wale wanaodhuulumiwa akitokea kujitambua na akatangaza kuwa ametambua dhuluma dhidi yake siku hiyo hiyo hutangazwa adui wa dhalimu hata kama katika maisha yake ya awali aliwahi kuwa rafiki na mfadhili wa dhalimu. 

Ni wazi basi wale wanaoendesha mapambano dhidi ya kikundi kidogo kinacho wadhulumu wanahitaji sana subira. Hawatasita baada ya uchaguzi kwani lengo lao si kufanyika uchaguzi bali ni kuondoa dhuluma. Endapo uchaguzi utasaidia kuondoka kwa dhuluma na kueneza haki sawa kwa wote basi mapambano yataahirishwa. 
 

Juu
 

YALIYOMO
 

TAHARIRI
NASAHA yatimiza mwaka mwaka mmoja

Mkapa, Karume wapewa tiketi za CCM kugombea urais

CCM walilia kiti cha CUF

Kufuatia kukamatwa kwa Sheikh Mbukuzi na Ricco:
Viongozi wa Serikali  watakiwa kuacha udini dhidi ya Waislamu

HABARI
Mauaji ya Mwembechai: Hatimae inquest yafunguliwa

DC aishukuru Finland

Amiri Mbukuzi ahojiwa na polisi

Wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi watajwa

USHAURI NASAHA
Mapambano dhidi ya dhuluma ni ya kudumu

MAKALA
Dini na siasa haviwezi kutenganishwa

MAKALA
Mchango wa taasisi ya Dhiynurayn

MAKALA
Sayyidat Fatma:Jumuia iliyosimama dhidi ya dhulma 

MAKALA
Kupiga vita udini zisiwe kauli za kuendeleza udini dhidi ya Waislam

HOJA BINAFSI
Kwa Rafiki yangu Mpendakula

Makala maalum ya Maulid
Kumpenda Mtume Muhammad (s.a.w.)

MAKALA
CCM  na sera za maendeleo

Habari za Kimataifaza Kimataifa

Lishe 
Vyakula vitupatiavyo vitamini C

BARUA

MASHAIRI

RIWAYA
Mapinduzi ya fikra - 4 

MICHEZO
Ongara, Salvatory, Nteze, Mwansasu waenda Ulaya
Mokake aikosoa Yanga


   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: nasaha1420@yahoo.com

Ukurasa wa mwanzo
Islam Tanzania
Matoleo yaliyopita