|
Na. 052 Jumatano Juni 14 - 20, 2000 |
|
|
|
|
|
Siku nne kabla ya kuanza ligi
kuu:
WACHEZAJI wa kutumainiwa wa timu ya Kajumulo, Kalimangonga Mtoro Ongara, Salvatory Edward Augustino, Nteze John Lungu na John Jacob Mwansasu wameondoka jana nchini wakielekea barani Ulaya kujaribu kucheza soka ya kulipwa. Akithibitisha jana jijini, Katibu Mkuu wa Kajumulo Juma Simba alisema kwamba wachezaji hao waliooondoka kwa ndege ya Swiss Air na British Airways watakuwepo huko kwa mwezi mmoja. Simba ameitaja Uswiss kama nchi ambayo kina Kally watajaribu bahati yao chini ya uangalizi wa Mkurugenzi Alex Kajumulo wa Kajumulo World Soccer ambaye tayari alikwisha wasili huko. Kally na Nteze ni washambuliaji, Salvatory ni kiungo wa kati na Mwansasu ni mlinzi ambao bila shaka watauwa wameacha uwazi mkubwa katika timu yao inayoshiriki ligi kuu Tanzania bara itakayoanza Jumamosi wiki hii kwa kupambana na Yanga. Akizungumzia mapengo hayo Simba amesema kocha Mkuu wa Klabu hiyo Jamhuri Kihwelo "Julio" kwa karibu wiki tatu sasa amekuwa akiwafuata vilivo wachezaji wanaotarajiwa kuziba mianya hiyo. Kwa mujibu wa Simba wachezaji hao ni Ali Shah
atakayechukua nafasi ya Kally , Ali Mohammed atakayecheza kama Salvatory
na Kipese ataziba pengo la Nteze wakati mbadala wa Mwansasu bado anasakwa.
Mokake aikosoa Yanga Na Mwandishi Wetu ERNEST Mokake, Kocha wa Timu za Vijana nchini chini ya umri wa miaka 17 na 20 amekosoa uchezaji wa wachezaji wa timu ya Yanga ambao amediani wa kukaribisha mashambulizi golini kwao. Makake ameyasema hayo wiki hii jijini baada ya kufuatilia mechi kadhaa ambazo Yanga imekuwa ikicheza Uwanja wa Taifa kama njia ya kujipima nguvu. Amesema kuwa tatizo la Yanga lipo katika sehemu ya ulinzi ambapo wachezaji wakepasiana pasiana bila sababu za msingi na kuwafanya washambuliaji wa timu pinzani kujazana langoni kwao. Katika kukazia hoja yake Makake ambaye ni raia wa Nigeria alisema - hata goli ambalo Yanga walifungwa na Bandari ya Mtwara lilitokana na makosa hayo". Katika mchezo huo wa mwishoni mwa wiki Yanga ilishinda mabao 4-1. Katika hatua nyingine washabiki wa baadhi ya wananchama wa Klabu ya Simba ya Mkoani Dar es Salaam Jumapili iliyopita nusura wawashambulie wachezaji watimu ya Bandari-Mtwara kwa kukubali kufungwa magoli 4-1 na Yanga huku wakiwa wamevaa 'uzi' mwekundu chini mpaka juu. Bila kificho washabiki hao wakawataka Bandari Mtwara kukoma kuvaa jezi zenye rangi nyekundu na nyeupe kwa kuwa hawana uwezo wa kutetea hadhi yake na hivyo kuifedhehesha klabu ya Simba ambayo inadaiwa kuwa na asili hizo. |
YALIYOMO
TAHARIRI
Mkapa, Karume wapewa tiketi za CCM kugombea urais Kufuatia
kukamatwa kwa Sheikh Mbukuzi na Ricco:
HABARI
Amiri Mbukuzi ahojiwa na polisi Wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi watajwa USHAURI NASAHA
MAKALA
MAKALA
MAKALA
MAKALA
HOJA BINAFSI
Makala maalum ya Maulid
MAKALA
Habari za Kimataifaza Kimataifa Lishe
RIWAYA
MICHEZO
|
|
|
|
|