|
Na. 047 Jumatano Mei 10 - 16, 2000 |
|
|
|
|
|
Mapinduzi ya fikra MTUNZI: ABU FIRDAUS ......"Rahma! Rahma Mwanangu.: :Bee Mama:,
nakuja." Hiyo ilikuwa sauti iliyojaa mapenzi na huruma ya Mama kwa mtoto,
ilikuwa ni sauti yaMama Rahma akimwita mwanae kipenzi. Wito wa mama Rahma
ulifuatiwa na mwitiko uliojaa adabu na nidhamu ya hali ya juu kutoka kwa
Rahma. Rahma mtoto wa pili kuzaliwa akitanguliwa na kaka yake, Luqman na
kufuatiwa na wadogo zake wawili Omar na Lul, ni watoto waliolelewa kwa
maadili mema ndani ya nyumba ya marehemu baba yao Abubakar. "Waite nduguzo
mje wote hapa barazani muda wetu umewadia.
ALIAGIZA Mama Luqman baada ya kumaliza sala ya Ishaa nakula chakula chao cha usiku. Haikuchukua muda mrefu wote walikuwa wameketi ukumbini wakimkabili mama yao kipenzi iliwasikielile alilowaitia kwa usiku ule. "Ni kawaida yetu kukutana na kukumbushana yale yanayotupasa kuyafanya au kuyaacha katika muda wote wa maisha yetu hapa duniani. Lakini leo, hatatumia muda wetu kama tulivyozoea, baliningependa kuwafikishia usia wawangu tu. Kumbukeni kuwa baba yenu amefariki na kuwaacha ninyimkiwa bado wadogo. Hivyo hamkupata bahati ya kupata usia kutoka kwake ambao mngeweza kuuzingatia." "Mimi mama yenu uzee umenikabili, mbali na uzee maradhi pia yameniandama. Shinikizo la damu, madonda ya tumbo na kisukari ni miongoni mwa magonjwa yanayonikabili. Sina maana kwamba kuwa na maradhi haya basi ndio sababu ya kufikwa na kifo, la hasha. Kwani watu wazima huweza kutangulia kufa na huku wanawanawaacha wagonjwa mahtuti wakiwa hoi wamelezwa hospitalini. Lakini inatosha kuwa dalili ya kusogelea safari yangu. Ndio maana nikaona kwakuwa sasa mnafahamu na mnaweza kuzingatia yale mnayoambiwa ni bora nikuwausia." Huo ulikuwa ni utangulizi alioutoa mama Laqman kwa watoto wake wanne kabla hajaanza kutoa usia wake. Utangulizi ambao uliwafanya watoto Luqman na Rahma kububujikwa na machozi ya huzuni. Kwanisi tu walikumbushwa msiba wa baba yao mpendwa bali piawalihisi kama mama yao naye yuko safarini. Lulu na Omar wao hawakulia, hii inatokana na umri wao kuwa haujawa na uwezo wa kuyachambua maneno na kupata maana ya ndani. Luqman mwenye umri upatao miaka kumi na nane, wao waliathirika moja kwa moja kwa hotuba hiyo fupi ya utangulizi. "Enyi wanangu, Mtume (S.A.W.) alisema ametuachia vitu viwil, Qur-an na Suna na mwenye kushikamana navyo hivyo vitu viwili, hatopotea kamwe. Enyi wanangu ili kufikia lengo letu la kuumbwa, mimi nawausia ninyi nyote kwa pamojamuishi katika mapinduzi, mtafanikiwa. "Ina maana badotunahaja ya kumpata kiongozi kwa njia ya mapinduzi"? Alihoji haraka Lulu ambaye kimaumbile ni mtoto mdadisi, mwenyehamu ya kufahamu mambo mengi kadriitakayvowezekana. "Hapana mwanangu, sisi tulishuhudia mapinduzi yaliyofanywa Zanzibar miaka ya sitini. Wakati wa mtume na maswahaba zake, waliteka au kufanya mapinduzi katika miji mbalimbali. Lakini kabla hajaondoka alisema vita vya silaha vilikuwa vimekwisha na kutupa habari juu ya vita kubwa zaidi ambayto ni kupambana na nafsi na kuishinda ili kifanyiwe mapinduzi roho yako. Katika hali ya kawaida, roho za binadamu huamrisha maovu. Roho ambazo hazijafanyiwa mapinduzi hutamani mali zote za watu zingekuwa zao. Hata kama wanakazi nzuri mshahara wa kutosha lakini bado watapokea rushwa na kuwadhulumu wafanyakazi zao. Roho ambazo hazijafanyiwa mapinduzi zinatawaliwa na ujinga, umaskini, husda, kiburi na kupenda kila kilichoharamishwa. Zaidi ya yote roho ambayo haijafanyiwa mapinduzi huwa nzito kujitoa kushiriki katika harakati na mapambano ya kuutetea Uislam. Kwa sababu wanapenda sanamaisha na anasa za dunia kuliko akhera yao. Huogopa zaidi kifo, huweweseka na kujawa na hofu pindi wanapougua kwa kujua safari (kifo) imewadia. Hivyo wanangu wapendwa nakuhusieni muishi katika mapinduzi siku zote. Mapinduzi mnayopaswa kuwa nayo ninyi kama vijana wa Kiislamu si mapinduzi kama ya Zanzibar wala ya Burundi. Si mapinduzi ya kutumia mtutu wa bunduki bali mapinduzi ya kifikra. Mkifanikiwa kufanya mapinduzi haya, mtaupindua ujinga na kuweka elimu, mtapindua chuki na husuda na nafasi yake kichukuliwa na mapenzi na huruma. Mtawaonea huruma watu na viumbe wengine. Mtatamani kutengeneza akhera yenu kuliko dunia kwani dunia ni yenye kupita mtakuwa ni watetezi wazuri wa wanyonge na wapingaji wa dhulma. Kimsingi njia pekee itakayowasaidia kufikia mapinduzi hayo ya fikra ni kuhoji uhalali wa kuwepo halifulani badala ya hali nyingine. Hii itawafanyaakili zenu zifanye mambo yaliyobora naya kimapinduzi. Alipumzika kidogo kupata tathmini juu ya somo lake kama linaeleweka vema. "Mnanielewa vemawanangu?" aliuliza mama Luqman "Tunakuelewa mama" walijibu kwa pamoja. Lakini jee tutayapimaje maamuzi yetu baada ya kuhoji uhalali huo? Aliuliza Rahma baada ya kuitika pamoja na wenzake kuwa wanamuelewa mama yao." Umeuliza swali zuri Rahma, watu wengi wanadhani wanaweza kufikia mapinduzi ya kweli au kupata ushindi katika harakati au maisha yao bila kufuata muongozo wa aliyewaumba. Hawaamini kabisa kuwa Mola wao anafaa kuwapangia taratibu za maisha. Ndio maana hutunga miongozo yao ya maisha (katiba) na kujiwekea sheria za kibinadamu. Ndio kusema kwanadhaniwanajifahamu zaidi kuliko yule aliyewaumba. Wanasahau kuwa akili za wanaadamu zinaudhaifu, zinatabia ya kupenda vitu japo vina madhara kwao na kuchukia vitu japo vina faida kwao. Kwa sababu hiyo, ema kwa makusudi au bahati mbaya akili huweza kuamua mambo kinyake vyake. Hivyo wanangu ili kuyapima maamuzi yenu kuwa ni boira au laa, ndio maanaMtume akasema ametuachia vitu viwili, kitabu cha MwenyeziMungu na mwenendo wake Mtume mwenyewe. Akasema mwenyekushikamana na vitu hivyo viwili hatopotea kamwe. Ndio kusemamaamuzi yenu myapime na sheria za aliyewaumba na Mtume wake. "Sijui umenielewa vizuri Rahma!" aliuliza mama \rahma. Nimekuelewa mama. Enyi wanangu muwe na subira juu ya yale yatakayokufikeni katika kuishi kwa kufuata muongozo na utaratibu wa maisha unaokubalika. Kwani jamii kwa sasa imeharibiwa kiasi cha kutisha. Ulevi unahamasishwa kana kwamba pombe imekuwa maziwa ambayo watu wakinywa huwajengea kinga mwilini. Kamari inazidi kuboreshwa na kuitwa bahati nasibu, kompyuta zimetengenezwa ziwasaidie kucheza kamari. Nyumba maalumzimejengwa ili kutoa fursa kwa wazinifu wafanye uchafu huo humo. Nyumba hizo zimeitwa kasino na zingine zikapambwa kwa kuitwa nyumbaza kulala wageni. Mtu anaishi Magomeni anaenda kulala nyumba ya wageni iliyopo Kinondoni au Mburahati! Ushirikina unahamasishwa kupitia vyombo vya habari na kupewa jina la "utabiri wa nyota." Uvutaji bangi, madawa ya kulevya na wasichana kujitoa utu wao kwa kutembea uchi. Muziki usio na mazingatia. Ndio kusema kwa kuhoji kwenu sababu ya kila jambo kutawafanya mpendwe sana na Mola wenu lakini mtachukiwa na kitu mtu muovu. Atadai ema unamwingilia katika maisha yake, mmepitwa nawakati, ilimradi tu mtajikuta mnatofautiana na jamii iliyoharibika. Enyi wanangu, muwe waadilifu katika kuwatendea haki watu. Mtumie shura katikakufikia maamuzi yenu. Shura yenu itegemee muongozo wa Molawenu. Je mmenielewa? Aliuliza mama Luqman huku akizunguusha macho kuwaangaliawanae. Wote waliinua vichwa kuashiria wameelewa. Kunamwenye swali kati yenu? Aliuliza tena Mama Luqman watoto wote walikaa kimya kitambo kisha kila mmoja akajibu hatuna kwa nyakati tofauti. "|Ewe Molawangu, shuhudia kuwa nimewausia watoto wangu kheri katika uhai wangu", alimaliza Mama Luqman. Waliomba dua kwa pamoja iliyoongozwa na Luqman kisha waliogubikwa na maswali na huzuni kwa watoto wa Abubakar. "Nini makusudia na mama yetu kutupa usia huu? Vipi tutakuwa pindi mama yetu kipenziatakapotangulia mbele ya haki? Maskini marehemu baba yetu, angetuhusianini endapo angekuwa hai? Hayo yalikuwa ni miongoni mwa maswali yaliyowakabili vijana hawa. Iliwachukuwa muda mrefu kupata usingizi fiku ile. ***** **** **** Baada ya miezi takriban saba, wakati huo Luqman akiwa anasoma katika chuo cha ufundi Dar es Salaamna Rahma akiwa mwanafunzi wa kitato cha nne, Mama yao kipenzi alilazwa katika hospitali ya Rufaa Muhimbiliakikabiliwa shinikizo ladamu. Baada yasiku tatu tatizo lasukari nalo liliingilia kati na hivyo kumfanya mama yao kuwa na hali mbaya zaidi. Katika muda wkote huu, Rahma na Luqman walishindwa kujisomea vizuri kutokana na hali ya mama yao kuwa mbaya. Baada ya mwezi mmoja na siku tatu, mama yao aliruhusiwa kutoka hospitalini na kurejea nyumbani. Hata hivyo ilimchukuwa siku takriban kumi na nanetu, hali ilirudi kuwa mbaya kwa matatizo yaleyale. Walimchukuwa jioni moja ndani yagari kumpelekea hospitalini. Rahma alikaa upnade wa kulia, pembeni ya mama yake. Upande wa kushoto mwa mgonjwa alikaa Mama Lueiman, jirani na rafiki kipenzi cha Mama Luqman. Wakiwa wmefika Jangwaniwakielekea hospitali Muhimbili, Mama Lu qman alipepesa macho kulia na kushoto kisha alitoa shahada "Ash-hadu an Ilah ilaha illah ila wa ash-hadu anna Muhammad Rasurullah". Klisha alishusha pumzi kwa nguvu na kukata roho.Rahma alishtushwa na kutulia kwa mama yake, alijaribu kusikiliza mapigo ya moyo yaliyokuwa yakienda kasi, moyo ulikuwa umetulia huku joto lamwili likitoweka taratibu. Alimkumbatia marehemu mama yake katutangulia, alilalama kwa uchungu. MamaSuleiman alimfunika marehemu Mama Luqman alimuasa Rahma aache kulia kwa sauti kwani si katika maadili mema na wala kulia kisingemsaidia kitu. Alimuombadereva asimamishe gari, na kubadili muelekeo wa safari kurejea na maiti nyumbani yapata saa mbili kasoro walikuwa tayari wamefika nyumbani. Waliteremsha maiti na kuiingiza ndani. Mama Suleiman aliwakusanya watoto wa marehemu na kukaa nao pamoja huku akiwanasih juu ya nini kinawapasa kufanya katika wakati ule mgumu. Asubuhi na mapema, majirani, ndugu na jamaa walianza kushughulikia mipango ya mazishi. Baada ya mazishi watu waliendelea kuifariji familia ya marehemu. Kwa upande wa Luqman, Rahma, Omari na Lulu, walikuwa na wakati mgumu zaidi. Wakifikria kifo cha baba yao marehemu mama yao na usia aliowaachia, wanajikuta wakikumbwa na wimbikubwa la mawazo hasa ukizingatia ukiwa waliokuwa nao kutokana na kukosa ndugu wa karibu. Baada ya muda wa maombolezo kumalizika, watoto wote walichukuliwa na Mama Suleiman. Mnjomba wao ambaye anaishi mkoani Tabora aliahidi kuja kuwaona pindi atakapopata uwezo kwani hali ya maisha ni ngumu. Na hata kama angewachukua ingekuwa vigumu kwake kuwagharimia kielimu. Waliendelea na masomo chini ya ungalizi wa Mama Suleiman. Kutokana na tukio hilo kutokea karibu na mitihani ya Kidato cha nne na mitihani ya mchundo kwa vyo, Rahma hakufanya vizuri katika mtihani wake wa mwisho Lugqman alifaulu, lakini si kwa kiwango ambacho kingemuwezesha kuchagualiwa endapo angetuma maombi katika chuo kingine ili ajiendeleze.Omar ambaye sasa alikuwa kidatocha pili na Lulu ambaye alikuwa darasa la saba waliendelea kujisomea. *** *** *** Luqman na Rahma waliendelea kuishi pale nyumbnani kwa Mama Suleiman huku........... |
YALIYOMO
TAHARIRI
Wananchi washutumu vyombo vya habari Lipumba awaambia wananchi wasibabaishwe na walioko madarakani Wasomi SUA walaani ‘rushwa’ ya kisiasa Polisi kataeni kutumiwa - Lipumba Maelfu ya tani za matunda yanaoza Tanga Habari za ndani
MPASHO NASAHA
HABARI
Ushauri Nasaha
Makala
MAKALA
MAKALA
Kalamu ya Mwandish
MAKALA
RIWAYA
Lishe
|
|
|
|
|