|
Na. 047 Jumatano Mei 10 - 16, 2000 |
|
|
|
|
|
Jukumu la wazazi, walimu kwa wanafunzi wanaomaliza masomo NA KHADIJA IDD SI jambo geni kwa watu waliopitia shule za
sekondari kuwa na matatizo, wasiwasi au hata kugombana wakati wanapokaribia
kumaliza au wanapomaliza masomo yao. Ugomvi au matatizo haya yanatokana
na kukosekana kwa msaada unaohitajika na unaofaa wakati mwanafunzi husika
anapohitimu masomo yake; au kutokana na kulazimishwa na mzazi au mlezi
kusoma masomo ambayo mwanafunzi huyo hayapendi. Ni wanafunzi wachache wanaopata
wasaa wa kukaa na walimu au wazazi wao kujadili kwa mapana juu ya kile
mwanafunzi huyo anachohitaji au kinachomfaa kuhusu maisha yake ya baadaye.
KATIKA kipindi hiki ambacho kidato cha sita wanafanya mitihani yao ya mwisho, wazazi au walezi wana jukumu kubwa sana la kuwasaidia watoto na wanafunzi wao. Kuwatakia wanafunzi mitihani myema na kuwahongera wanapomaliza mitihani na kufaulu haitoshi. Lakini waangalie kwanza wamewasaidia vipi kuelewa na kuchagua kozi na kazi watazochukua baada ya matokeo ya mitihani hiyo kutoka. Pamoja na kwamba muda mwingi wa watoto wao unapita wakiwa shule na wakati mwingine "tution", wazazi wana jukumu la kuzungumza na watoto wao na kuwashauri kwa wakati huo huo mdogo uliopo. Wanaweza kuwauliza maoni yao juu ya masomo yao na juu ya yale wanayoyapendelea na kujadili iwapo yanafaa kulingana na hali halisi ya maisha au la. Wazazi wanaweza kuchukua fursa hii kuchambua masomo au kozi zilizochaguliwa na watoto wao na kuangalia kazi wanazoweza kufanya kutokana na masomo hayo. Iwapo mzazi hana ujuzi juu ya masomo anayosoma mtoto wake au hajui kabisa juu ya mambo yanayohusu shule bado wana nafasi ya kumsaidia mtoto. Mzazi anaweza kuzungumza na walimu wa mtoto wake ili waweze kumsaidia kama wako karibu. Iwapo pia mtoto huyo anasoma shule ambayo iko mbali na nyumbani ya bweni, mzazi anaweza kukuwasiliana nao kwa simu au barua. Anaweza pia kumtafuta mtaalam wa masomo yake aliye karibu. Magazeti na majarida yanaweza kumsaidia kupata taarifa juu ya vyuo mbalimbali na mahitaji yake. Radio na Televisheni pia zitampa taarifa muhimu anazohitaji kupitia matangazo ya vyuo na kozi mbalimbali na namna ya kuwasiliana nao. Baada ya kupata taarifa hizi unaweza kuwasiliana na vyuo hivyo wewe mwenyewe na ukapata taarifa unazohitaji kufahamu kama vile masomo yanayofundishwa, muda, vyeti vinavyotolewa, mahal ichuo au shule ilipo n.k. Cha msingi hapa ni kushirikiana na mtoto wako ili aweze kupita vizuri katika kipindi hiki kigumu vile vile asipitie katika ugumu ambao wazazi na ndugu zake walipitia. Mzazi amsaidie mtoto wake afahamu baada ya masomo ya kidato cha nne atasoma nini, au baada ya kidato cha sita atasomea kozi gani na wapi na kwa muda gani. Hili litamfanya mtoto wako asome kwa malengo sio tu kwa vile alifaulu darasa la saba na amepitia sekondari. Lakini pia mzazi atasaidiana na walimu katika kuwasaidia wanafunzi husika, wakati mwingine pia mzazi atakuwa ana kumbusha mwalimu juu yasuala hili pale wanaposahau kufanya hivyo. Pamoja na jukumu hili la wazazi, walimu wana nafasi kubwa sana juu ya kumshauri mwanafunzi juu ya masomo yake ya baadaye. Ukubwa wa nafasi hii umetokana hasa na hali halisi kwamba, walimu wako pamoja na wanafunzi kwa muda mrefu na pia kwa sababu wanawafahamu wanafunzi wao na uwezo wao katika masomo wanayochukua. Pamoja na hayo, wana uwezo na ujuzi wa kutoa ushauri kama walimu na kama washauri na vile vile wanazo taarifa za kozishule navyuo mbalimbali vinavyowafaa wanafunzi wao. Kutokana na uwezo na nafasi zao, walimu wanaweza kuwasidia wanafunzi wao kwa kuwapatia taarifa juu ya kozi na vyuo mbalimbali hata kabla ya kuanza mwaka wao wa mwisho shuleni. Mwalimu anaweza kuwabandikia taarifa hizi katika mbao za matangazo au kuziwasilisha kwao ana kwa ana. Hata hivyo hili ni jambo ambalo walimu wote wanalifahamu na wanafahamu pia majukumu yanayowakabili katika suala hili. Ila ni walimu wachache sana ambao wanatekeleza hili. Ni wakati muafaka basi kwao kutekeleza ualimu wao hasa katika wakati huu ambao una matatizo ya ajira, utitiri wa vyuo na hali ngumu ya maisha. Walimu wana deni la kulipa, nalo ni hili la kuwasaidia wanafunzi wao kuelewa watakwenda wapi na watafanya nini mara watakapomaliza masomo yao. Vyuo viko vingi sana siku hizi ni jukumu la walimu kuwasaidia wanafunzi wao kuchagua wanavyovihitaji na vinavyowafaa. Vyombo vya habari vitumiwe na walimu kuwapatia wanafunzi taarifa zinazofaa. Walimu wawasaidie pia katika kuwatafutia wataalam kutoka sehemu mbalimbali ambao watawafahamisha wanafunzi juu ya taaluma zao, kama vile kutoka sekta ya utalii, kitivo cha sheria, vyuo vya ualimu, uhandisi, udaktari n.k. Mzazi na mwalimu aone jukumu la kumshauri mwanafunzi/mtoto
wake ni lake. Kila mmoja achukue jukumu lake na amsaidie kijana husika
tusingoje mpaka muda umekwisha, bali tumsaidie mapema ili awe na malengo
na mwelekeo.
|
YALIYOMO
TAHARIRI
Wananchi washutumu vyombo vya habari Lipumba awaambia wananchi wasibabaishwe na walioko madarakani Wasomi SUA walaani ‘rushwa’ ya kisiasa Polisi kataeni kutumiwa - Lipumba Maelfu ya tani za matunda yanaoza Tanga Habari za ndani
MPASHO NASAHA
HABARI
Ushauri Nasaha
Makala
MAKALA
MAKALA
Kalamu ya Mwandish
MAKALA
RIWAYA
Lishe
|
|
|
|
|