|
Na. 047 Jumatano Mei 10 - 16, 2000 |
|
|
|
|
|
Nchi wafadhili wataka upinzani, CCM yalalama NJIA pekee itakayoweza kuifanya Serikali iwajibike kwa wananchi wake ni kuwepo kwa upinzani wenye nguvu. Kauli hiyo imetolewa na Profesa Palle Svensson wa chuo kikuu cha Arhus kilichoko nchini Denmark, wakati wa mazungumzo na Katibu Mkuu wa CCM, Bw. Philip Mangula yaliyofanyika Mei 8, jijini Dar es Salaam. Mtaalamu huyo yupo nchini kufuatilia maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, akiziwakilisha nchi wafadhili. Nchi hizo ni Sweden, Canada, Uingereza, Finland, Ireland, Norway, Uholanzi na Switzerland. Mwakilishi huyo wa nchi wafadhili pia alikutana na maafisa wa tume ya uchaguzi. Kwa kawaida katika nchi zenye vyama vya kisiasa vyenye nguvu, wananchi wanajulishwa udhaifu wa serikali iliyoko madarakani na hatimaye wanaiondoa serikali hiyo madarakani kwa njia ya uchaguzi, na kukiweka madarakani chama kingine. Kutokana na hali hiyo, baadhi ya serikali hasa katika nchi ambazo hazijali utawala wa kidemokrasia, zinavibana na kuvihujumu vyama vya upinzani ili visiwe na nguvu, na hatimae kudharauliwa na wananchi. Baadhi ya njia zinazotumika kuvihujumu na hatimaye kuvidhoofisha vyama vya upinzani ni pamoja na kuzuia mikutano ya wazi ya vyama vya upinzani, kuwakamata na kuwafungulia mashitaka viongozi wa upinzani, kuwatisha matajiri ili wasivisaidie vyama vya upinzani na mara nyingine hufikia hata kuwatisha na kuwanunua viongozi na wananchi. Naye Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Bw. Philip Mangula, akizungumza katika kikao hicho na Profesa Palle Svensson, alisema nchi wafadhili kuacha fikra alizoziita potofu kwamba uchaguzi wowote hapa nchini utakubaliwa tu kuwa umekuwa huru na wa haki ikiwa CCM itaondolewa madarakani. Bw.Mangula pia aliwaomba wafadhili waisaidie Tume
ya Taifa ya Uchaguzi. "Ni vyema wafadhili waisaidie Tume ya Taifa ya Uchaguzi
kujenga uwezo wa kutoa elimu ya uchaguzi kwa umma na kujenga uwezo wa kuendesha
na kusimamia uchaguzi kwa ufanisi mkubwa zaidi ili uchaguzi uwe huru na
haki", alisema katibu huyo wa CCM.
Mwandishi Wetu, Musoma WAUMINI wa dini ya Kiislamu wilayani Musoma mjini wamemtumia barua Waziri wa Sheria na Mambo ya Katiba, kulalamikia kitendo cha mahakimu wa wilayani hapa kuwataka wavue kofia mahakamani wakati wa kutoa ushahidi au kuwachukulia dhamana watuhumiwa. Katika barua hiyo ya tarehe Mosi Mei mwaka huu,
yenye kumbukumbu Na. Vol.Bak/MB/16/3/292 iliyosainiwa na Bwana Nyamrasa
Said, Waislamu wa mjini hapa wamedai kuwa hatua hii ya mahakama ni ya kuwadhalilisha
wao na dini yao.
|
YALIYOMO
TAHARIRI
Wananchi washutumu vyombo vya habari Lipumba awaambia wananchi wasibabaishwe na walioko madarakani Wasomi SUA walaani ‘rushwa’ ya kisiasa Polisi kataeni kutumiwa - Lipumba Maelfu ya tani za matunda yanaoza Tanga Habari za ndani
MPASHO NASAHA
HABARI
Ushauri Nasaha
Makala
MAKALA
MAKALA
Kalamu ya Mwandish
MAKALA
RIWAYA
Lishe
|
|
|
|
|