|
Na. 047 Jumatano Mei 10 - 16, 2000 |
|
|
|
|
|
Wameshindwa miaka 40 hawataweza 5 ijayo Na Mwandishi Wetu MWENYEKITI wa Taifa wa Chama cha Wananchi (CUF) Mhe. Profesa Ibrahim Lipumba amewataka wananchi kutokubabishwa na wale walioko madarakani kuwa wanaweza kuwaletea maendeleo katika kipindi cha miaka mitano ijayo wakati wameshindwa kufanya hivyo kwa kipindicha miaka 40. Mhe. Lipumba aliyasema hayo Mewi 6 na 7 mwaka huu alipokuwa akizungumza na mamia ya wananchi wa Mlandizi na Chalinze katika mikutano mwili tofauti ya chama hicho. Alisema kuwa kipindi cha miaka 40 ni kikubwa mno ambacho mtu anaweza kuzaa na kujukuu, lakini Chama Cha Mapinduzi na mzazi wake TANU vimeshindwa kufanya lolote katika kuleta maendeleo ya wananchi hadi kuitumbukiza nchi katkka umaskini uliokithiri. Alisema kuwa 1961 viongozi wa TANU waliwaahidi wananchi kuwa wangetumia muda wa miaka 10 tu kuleta maendeleo na maisha bora kwa wananchi zaidi ya maendeleo yaliyoletwa katika muda wa miaka 76 ya ukolohi wa Wajerumani na Waingereza. Baada ya miaka 40 ya uhuru, Mhe. Lipumba alisema, asilimia 50 ya Watanzania wanaishi katika maisha ya umasikini wa kutupwa, ambapo asilimia hiyo hiyo ya watoto wadogo chini ya umriwa miaka 5 wanautapiamlo. "Hali ya maradhi inatisha, malaria imeshakuwa sugu. Serikali ya Japan imetoa mabilioni ya shilingi katika kupambana na malaria, lakini fedha zimetafunwa na wenye meno", alisema Mhe.Lipumba. Alisema kuwa hali ya upatikanaji wa huduma muhimu katika nchi imekuwa ngumu, na akatolea mfano wa maji na elimu kukazia nukta hiyo. "Hivi sasa Watanzania zaidi ya milioni 2 wenye umri wa kujiunga na shule za msingi hawamo mashuleni. Katika kila vijana 100 ni vijana 70 tu ndio wako mashuleni. Na hata hao walioko mashuleni hawapati elimu yakufaa", alisema. Akizungumzia kuporomoka kwa sekta ya kilimo na biashara alisema kuwa wakati mbogamboga na matunda kama vile mabibo, embe na machungwa yana soko kubwa katika nchi za Ulaya na Marekani, hapa nchini bidhaa hizo zinaoza kwa kukosa soko na hivyo kuwakatisha tamaa wakulima. Aidha aliwataka wananchi nchini kuwa na msimamo wakupambana na udhalimu na kwamba wasiwe waoga, kwani hakuna jamii ya waoga ambayo imeweza kupambana na watawala wenye kuendeleza udhalimu juu ya raia zao. Aliwahimiza wananchi hao kuendelea kuhamasishana na kujitokeze kwa wingi kujiandikisha na hatimaye kupiga kura muda utakapofika, kwani kwa kuindoa CCM pekee ndio wanaweza kuondokana na madhila haya yanayowakabili. Mwenyekiti huyo wa CUF alimalizia kwa kusema,
"Watanzania hatujamkosea Mungu, matatizo yetu ni matokeo ya sera mbovu
na zisizotekelezeka za CCM."
|
YALIYOMO
TAHARIRI
Wananchi washutumu vyombo vya habari Lipumba awaambia wananchi wasibabaishwe na walioko madarakani Wasomi SUA walaani ‘rushwa’ ya kisiasa Polisi kataeni kutumiwa - Lipumba Maelfu ya tani za matunda yanaoza Tanga Habari za ndani
MPASHO NASAHA
HABARI
Ushauri Nasaha
Makala
MAKALA
MAKALA
Kalamu ya Mwandish
MAKALA
RIWAYA
Lishe
|
|
|
|
|