NASAHA
Na. 047 Jumatano Mei 10 - 16, 2000
Ukurasa wa mwanzo
Islam Tanzania
Matoleo yaliyopita
Tahariri

NASAHA
S.L.P. 72045, Simu: 0811 - 600145, Dar es Salaam

Mazingira ya uchaguzi huru na haki yasivurugwe



Watanzania tayari tupo katika kipindi cha vuguvugu la kuelekea kwenye Uchaguzi Mkuu.

Shamrashamra zilizotanda katika safari na hata 'sherehe' ya Mhe. Mkapa wakati wa kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni ushahidi tosha kwamba tayari joto la uchaguzi mkuu ujao limeanza kupanda kwa kila mshiriki, yaani mpiga kura na mgombea mtarajiwa.

Kwa kuwa tupo katika mfumo wa vyama vingi vya siasa, hatuna budi kuelewa kuwa kila chama, kama vile ilivyo kwa wananchi wote wanahaki sawa ya kushiriki katika uchaguzi huo.

Inawezekana kwa baadhi ya watu kutokana na uzoefu wa kuwa chini ya uongozi wa chama kimoja tangu tupate uhuru mwaka 1961, ambapo vyombo na taasisi zote ziliandaliwa kukitumikia chama hicho; na kwakuwa chama hicho bado kipo madarakani; wakadhani kuwa hicho chama kina haki pekee iliyokubwa zaidi kuliko vyama vingine.

Lakini ukweli ni kwamba vyama vyote vina haki sawa mbele ya katiba ambayo pia inawapa wananchi haki na uwezo wa kuchagua chama chochote kati ya hivyo vilivyopo na kukiweka madarakani.

Ni kutokana na ukweli huo, sheria na kanuni za uchaguzi zinahitaji kuwepo na mazingira sawa kwa vyama vyote vitakavyo shiriki uchaguzi.

Mazingira hayo ni muhimu ili kutoa fursa ya mshindi kupatikana katika misingi ya kidemokrasia ambayo hustawi katika uchaguzi ulio huru na wa haki.

Na ili kuwepo hali ya kidemokrasia iliyo huru na ya haki, hapana budi mazingira yake kujengwa mapema.

Matukio yanayodaiwa kuwaathiri wanachama na wapenzi wa chama cha upinzani cha CUF kuzuiliwa katika msafara wa kuelekea kwenye mikutano ya chama hicho hivi karibuni huko Mlandizi na Chalinze mkoani Pwani, hayasaidii kujenga mazingira bora ya kidemokrasia kama inavyo tarajiwa. Kwa sababu matukio hayo yametokea baada ya baadhi ya viongozi wanachama na hata wapenzi wa chama tawala toka Dar es Salaam kuhudhuria mkutano wa Mei Mosi na hafla Mhe. Mkapa kuchukua fomu ya uchaguzi Dodoma.

Inawezekana kuwa baadhi ya taratibu hazikutimia katika kuwawezesha wanachama wa CUF kusafiri kutoka Dar es Salaam hadi mkoa wa Pwani. Lakini, ni vyema wahusika wangewaelimisha wanachama na viongozi wa chama hicho cha upinzani pasipo kujenga mazingira ya chama hicho kuona kinaonewa kwa kuwa ni chama cha upinzani.

Kwani hali hiyo inaweza kuwa chanzo cha wananchi kuanza kutilia mashaka hali ya uchaguzi mkuu utakavyo kuwa mwaka huu.

Inaweza kujengwa fikra ya kuwa uchaguzi huo hautokuwa huru na wa haki. 
 

Juu
 

YALIYOMO
 

TAHARIRI
Mazingira ya uchaguzi huru na haki yasivurugwe

Wananchi washutumu vyombo vya habari

Lipumba awaambia wananchi wasibabaishwe na walioko madarakani

Wasomi SUA walaani ‘rushwa’ ya kisiasa

Polisi kataeni kutumiwa - Lipumba 

Maelfu ya tani za matunda yanaoza Tanga

Habari za ndani
Uondoeni ‘ukoloni’ wa CCM- Mbukuzi

MPASHO NASAHA
WABONGO HAWANA NYONGO !

HABARI
Nchi wafadhili wataka upinzani,  CCM yalalama

Waislamu Musoma walalamika

Habari za Kimataifa

Ushauri Nasaha
Jukumu la wazazi, walimu kwa wanafunzi wanaomaliza masomo

Makala
Madhara ya ulevi kwa binadamu

MAKALA
Sababu ‘1000’ kwanini tunataka CCM ing’oke madarakani - 6

MAKALA
Kiini macho cha msamaha wa deni

Kalamu ya Mwandish
Kama CUF ni chama cha Waislamu 
Jee, CCM ni chama cha Wakristo?

MAKALA
Chama cha Mapinduzi na sera za maendeleo (2)

RIWAYA
Mapinduzi ya fikra

Lishe
Jinsi ya kuzuia utapiamlo kwa wanawake

BARUA

MASHAIRI

MICHEZO

  • Real Madrid yaingia fainali
  • Mapunda, Makoye hawafai timu ya Taifa - Kipingu
  • Tarimba ashinikizwa kujiuzulu Yanga

  •  

     


       Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:Bonyeza hapa
    Au
    Andika barua  kwa: nasaha1420@yahoo.com

    Ukurasa wa mwanzo
    Islam Tanzania
    Matoleo yaliyopita