|
Na. 047 Jumatano Mei 10 - 16, 2000 |
|
|
|
|
|
Na Mwandishi Wetu MWENYEKITI wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba amelaani kitendo cha Polisi kutumika kuvuruga mikutano ya chama cha chake. Hayo aliyasema alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara mjini Chalinze mkoa wa Pwani Jumapili iliyopita, kufuatia kilichodaiwa Polisi kuzuia msafara wa wanachama wa CUF waliokuwa wakifuatana na mwenyekiti huyo katika ziara ya Mlandizi na Chalinze zilizofanyika Mei 6 na 7. Imeelezwa kwamba katika msafara wa Mei 6, magari yaliyo wabeba wanachama na wapenzi wa CUF yalisimamishwa Kibaha Maili Moja, kwa madai mbali mbali ikiwemo magari kuchubuka rangi. Aidha katika msafara wa Mei 7 magari ya CUF yalizuiliwa katika eneo la Pingu, kilometa chache kabla ya kufika Chalinze takriban kwa zaidi ya masaa 7. Katika msafara huo ilidaiwa kwamba Polisi waliyasimamisha magari ya CUF kwa sababu kadhaa ikiwemo ya kukosa kibali cha kusafiri katika njia hiyo. Juhudi za viongozi wa CUF kutaka msafara huo uruhusiwe kuendelea na safari hazikufanikiwa na badala yake watu watano akiwemo kiongozi wa chama hicho, Bw. Akwilombe ambaye ni Mkurugenzi wa Vijana, walifunguliwa mashitaka, katika mahakama ya Wilaya, mjini Bagamoyo. Hata hivyo baadhi ya wanachama wa CUF walifanikiwa kufika katika mkutano huo baada ya kukodisha magari yaliyokuwa na kibali cha kwenda Chalinze. Pamoja na hali hiyo, Polisi wengi walipelekwa katika mkutano huo na imedaiwa kuwa wananchi walitishwa ili wasihudhurie mkutano huo wa chama cha upinzani. Mwenyekiti wa CUF, Profesa Lipumba aliwataka polisi wakatae kutumiwa na CCM kuvuruga demokrasia nchini bali wafanye kazi kwa kuzingatia sheria. Aliwafahamisha polisi kuwa katika mfumo wa kidemokrasia wenye kuthamini haki za binadamu polisi hawana haki ya kumzuia raia kutembea au kusafiri kutoka sehemu moja kwenda nyingine.Hivyo kitendo cha kuwazuia wananchi na wanachama wa CUF kuhudhuria mikutano ya Mlandizi na Chalinze ni kwenda kinyume haki hiyo. Aliwakumbusha polisi hao juu ya kisa cha aliyekuwa Rais wa Chile, Generali Agusto Pinochet ambaye alijitengenezea na kuweka mazingira ya utawala, ambao haukujali demokrasia, leo anatapatapa kwa ubaya alioufanya. Aidha Mwenyekiti huyo wa CUF alieleza katika mkutano huo kuwa mikutano yao mara kwa mara inavurugwa na vyombo vya dola, na kila walipolalamika baadhi ya watu wakiwemo mabalozi wa nchi za nje, walikuwa wakidai vielelezo vya ushahidi. Hivyo aksema kuwa matukio hayo ni ushahidi wa kutosha. |
YALIYOMO
TAHARIRI
Wananchi washutumu vyombo vya habari Lipumba awaambia wananchi wasibabaishwe na walioko madarakani Wasomi SUA walaani ‘rushwa’ ya kisiasa Polisi kataeni kutumiwa - Lipumba Maelfu ya tani za matunda yanaoza Tanga Habari za ndani
MPASHO NASAHA
HABARI
Ushauri Nasaha
Makala
MAKALA
MAKALA
Kalamu ya Mwandish
MAKALA
RIWAYA
Lishe
|
|
|
|
|