NASAHA
Na. 047 Jumatano Mei 10 - 16, 2000
Ukurasa wa mwanzo
Islam Tanzania
Matoleo yaliyopita
Habari za ndani

Maelfu ya tani za matunda yanaoza Tanga 

Na Ali Shechonge 

ZAIDI ya tani 32,000 za matunda na mboga mboga zinazolimwa mkoani Tanga, zinaoza kila mwaka kwa kukosa soko na kiwanda cha kusindika mazao hayo ya kilimo.

Akinukuliwa na vyombo mbali mbali vya habari mwanzoni mwa wiki hii, Afisa wa Kilimo na Mifugo wa Wilaya ya Lushoto, Bw. Twaha Kizunguto, alisema hali ya soko la mazao ya matunda na mboga mboga katika wilaya hiyo inasikitisha sana. 

Mtaalam huyo wa wilaya aliongeza kwa kusema ubovu wa bara bara ni kikwazo kingine kinachowafanya wakulima kushindwa kupeleka mazao yao katika jiji la Dar es Salaam na mkoa wa Kilimanjaro, ambako angalau kuna soka la matunda na mboga mboga. 

Mkoa wa Tanga na hasa wilaya yake ya Lushoto inaongoza kwa uzalishaji wa matunda. 

Bw.Twaha Kizunguto ametoa wito kwa serikali kutafuta wawekezaji ili wajenge viwanda vya kusindika matunda na mboga mboga, hatua ambayo itawasaidia wakulima kuepukana na hasara wanayoipata kila mwaka. 


Uondoeni 'ukoloni' wa CCM- Mbukuzi 

UMETOLEWA wito wa kuwataka wananchi wakiondoe Chama Cha Mapinduzi (C.C.M) madarakani.katika uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.

Wito huo umetolewa hivi karibuni na Amir wa Shura ya Maimamu Sheikh Juma Mbukuzi, wakati akihutubia katika maadhimisho ya mwaka mpya wa Kiislam wa 1421 A.H. yaliyofanyika katika msikiti wa Ijumaa wa Gongo la Mboto mwisho. 

Amir Mbukuzi aliuambia umati wa waumini waliohudhuria maadhimisho hayo kuwa wakati wa kuhakikisha jamii inakombolewa kutoka katika ukoloni wa CCM hivi sasa umekwishawadia. 

Sheikh Mbukuzi aliufananisha utawala wa C.C.M na wakoloni kwa kuwabagua wananchi na kutojali maslahi yao.Akitoa mfano,Sheikh huyo alisema. 

"Wakoloni (Wazungu) waliichukia sana TANU, hadi Baba yangu Mzee Mbukuzi kwa hofu akawa anaificha kadi yake ya TANU ndani ya shimo la choo kwa kuining'iniza na uzi ili asijulikane kuwa yeye ni mwana-TANU. Hii ni sawa na leo wapinzani wanavyochukiwa. Imefikia akikamatwa Sheikh au kiongozi yeyote wa Kiislam basi huusishwa na CUF. "Sasa kwani kuwa CUF ni dhambi?", alihoji Sheikh Mbukuzi. 

Aliwataka waumini wazipuuze propaganda za kutochanganya dini na siasa, na badala yake waendelee kuelimishana popote pale walipo jinsi gani wataikomboa jamii. 

Alisema msamiati wa kutochanganya dini na siasa umetungwa maalum muda mrefu ili kuwaziba mdomo Waislamu wasipate kuyabainisha maovu yanayofanywa na CCM na serikali yake dhidi ya raia. 

Alisema inashangaza sana kuwaona watu hawa leo wanajitia kusahau kwamba jambo la kuchanganya dini na siasa ndio lililoleta uhuru wa nchi ya Tanganyika, ambapo Waislamu ndio waliokuwa mstari wa mbele na kusimama kidete katika kumwondoa mkoloni. 

"Wanajifanya hawajui kuwa Mufti wa Waislamu, Almarhuum Sheikh Hassani bin Amir, pamoja na kufundisha dini katika msikiti wa Ngazija, alikuwa pia akigawa wazi kadi za TANU msikitini hapo", alisema Amir Mbukuzi. 

Aidha, Sheikh Mbukuzi alionesha kushangazwa na ukimya wa viongozi wa serikali pale ambapo wakristo hasa kanisa katoliki linapozungumzia siasa. 

"Lakini wao hawasemwi kuwa wanachanganya dini na siasa, ila Waislamu tu. Tutambue kuwa propaganda hiyo dhidi yetu ni kuogopa tusiwaseme kwani ni sisi ndio waliotuathiri sana. Hivyo, wanachokihami hapo ni ukweli wa mambo unaowauma tunaowasema. Sasa tunasema hivi, hatutoishia tu katika kuchanganya dini na siasa bali ni kukorogwa hadi dhulma iondoke". 
 

Juu
 

YALIYOMO
 

TAHARIRI
Mazingira ya uchaguzi huru na haki yasivurugwe

Wananchi washutumu vyombo vya habari

Lipumba awaambia wananchi wasibabaishwe na walioko madarakani

Wasomi SUA walaani ‘rushwa’ ya kisiasa

Polisi kataeni kutumiwa - Lipumba 

Maelfu ya tani za matunda yanaoza Tanga

Habari za ndani
Uondoeni ‘ukoloni’ wa CCM- Mbukuzi

MPASHO NASAHA
WABONGO HAWANA NYONGO !

HABARI
Nchi wafadhili wataka upinzani,  CCM yalalama

Waislamu Musoma walalamika

Habari za Kimataifa

Ushauri Nasaha
Jukumu la wazazi, walimu kwa wanafunzi wanaomaliza masomo

Makala
Madhara ya ulevi kwa binadamu

MAKALA
Sababu ‘1000’ kwanini tunataka CCM ing’oke madarakani - 6

MAKALA
Kiini macho cha msamaha wa deni

Kalamu ya Mwandish
Kama CUF ni chama cha Waislamu 
Jee, CCM ni chama cha Wakristo?

MAKALA
Chama cha Mapinduzi na sera za maendeleo (2)

RIWAYA
Mapinduzi ya fikra

Lishe
Jinsi ya kuzuia utapiamlo kwa wanawake

BARUA

MASHAIRI

MICHEZO

  • Real Madrid yaingia fainali
  • Mapunda, Makoye hawafai timu ya Taifa - Kipingu
  • Tarimba ashinikizwa kujiuzulu Yanga

  •  

     


       Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:Bonyeza hapa
    Au
    Andika barua  kwa: nasaha1420@yahoo.com

    Ukurasa wa mwanzo
    Islam Tanzania
    Matoleo yaliyopita