|
Na. 047 Jumatano Mei 10 - 16, 2000 |
|
|
|
|
|
Jinsi ya kuzuia utapiamlo kwa wanawake CHAMOS, H.J UTAPIAMLO husababisha maradhi mengi, na kuwa hatari zaidi na kwa haraka na magonjwa mbalimbali kuliko watu wenye (fya) lishe nzuri, nayo maradhi huwadhoofisha sana watu hata wakashindwa kufanya kazi kwa bidii kukabiliana na hali ngumu ya maisha. Hivyo umasikini kuongezaka. Kwa upande wa mwananke, mambo huwa mabaya zaidi kwani yeye hupelekea kuzaliwa watoto kudhoofu na hatimaye jamii dhoofu isiweze kufanya kazi kisawawa. Tufanyeje basi ili kuzima utapiamlo kwa wanawake? Kwa kuwa tatizo ni utapiamlo, basi bila shaka suluhisho la awali ni upatikanani wa chakula cha kutosha. Hili litawezekana iwapo sera madhubuti za kilimo bora zitakapopewa kipaumbele. Familia zisaidiwe utaalam na pembejeo ili ziweze kujizalishia chakula cha kutosha na cha ziada kuepuka baa la njaa. Kilimo ambacho ni uti wa mgongo wa Taifa letu kimesahauliwa kabisa, serikali imekuwa zimamoto ikisubiri njaa iombe msaada, badala ya kuzuia kwa kuwa serikali hii imezeeka hatujachelewa (40) tuipe mgongo Oktoba ili tuwaone vijana watakavyofanya kazi, upepo unaweza kupasika. Familia nyingi vipato vyao ni duni kuweza kuzitosheleza kwa mahitaji muhimu ya kimaisha. Gharama ya maisha ni juu, hali uchumi unazama matopeni. Miradi midogo midogo ya kimaendeleo inaweza kuongeza pato la familia. Kina baba wawaruhusu wake zao kujishughulika ili kuweza kuingizia familia fedha, hivyo kujitosheleza kwa chakula. Serikali inayo jukumu la kutoa misaada au mikopo bila riba na upendeleo kwa wanawake. Ni jambo la ajabu kuona wanawake wenye uwezo kifedha ndio wanaopata mikopo. Na wengine ni wale wenye uhusiano wa karibu na "WENYE OFISI", hali ya kuwa wanawake wa hali ya chini wakizidi kunyanyaswa na utapiamlo. Wahusika tuyaone haya na kuyaoondoa mapema, kwani hata watu wakiisha wote, hatufurahi kubaki na kuishi peke yetu duniani! Tupendane na kusaidiana. Sayansi na teknolojia itumike pia katika kumpunguzia mama majukumu yake, hivyo kupunguza upotevu wa nguvu nyingi. Badala ya kusaga kwa jiwe, vijiji vipatiwe mikopo ya mashine za kusaga; na wala isiwe mikopo jela inayodai riba trilioni! Upatikanaji wa visima vya maji karibu na makazi utapunguza muda na nguvu anazotumia mama kutafuta maji. Halikadhalika familia zitapata maji salama. Ubunifu wa majiko yanayotumia kuni chache yatampunguzia mwanamke kazi ya kutafuta kuni na hata kutunza mazingira. Kupunguza bei za umeme na mafuta ya taa kutaziwezesha familia kubana matumuzi zaidi na kuweza kununua chakula cha kutosha. Vituo vya kulelea watoto vitaweza kuwasaidia wanawake kazi ya kwenda na watoto shambani; vilevile vinaweza kuwapa nafasi wanawake kujiaajiri wenyewe au kuajiriwa badala ya kukaa nyumbani kulea watoto na utapiamlo. Lengo hasa ni kupunguza mzigo wa kazi za wanawake. Mtaala wa elimu kuanzia shule za msingi ni vyema kuwa na michepu ya lishe katika madarasa mbalimbali. Wanafunzi tangu awali waelimishwe kuhusu lishe bora, miili yao na ulazima wa kula chakula cha kutosha. Elimu ya lishe na afya bora ni vyema ikafundishwa kwa jamii yote kwa ujumla. Jamii inapaswa kusoma vijarida, magazeti, kusikiliza redio na kuangalia tv. Ni vizuri kusoma ratiba za redio na TV ili uchague vipindi vyenye manufaa. Jamii inapaswa kufahamu kuwa wanawake wanahitajika kula vyakula vya kutosha na vya aina mbalimbali, kabla na wakati wa ujauzito; kipindi cha unyonyeshaji kwa afya zao binafsi na afya za watoto wao. Kinababa wafahamu kuwa mke mwenye nguvu na afya bora ni faida na si mzigo kwa mumewe, anaweza kufanya shughuli zake kwa ufanisi, hukuza uwezo wake kiakili na vilevile huzaa watoto wenye afya bora. Mume anaweza kumsaidia mkewe kubakia na afya bora kwa kumpa chakula cha kutosha na kumpunguzia kazi . Wanafamilia pia wanapaswa kumsaidia mama ili aweze kunyonyesha mtoto zaidi ya miaka miwili. Yaani asibebe mimba mapema. Iwapo watoto watazaliwa karibu karibu, mama na watoto wanaweza kudhoofu daima. Mwanamke ni tegemeo letu katika malezi ya jamii, mwanamke ni jicho letu katika kuendeleza uzao (kizazi), mwanamke ni mama wa kila kilicho hai na mama ni kipenzi cha kila kiumbe. Yaani hiyo haitoshitu kuwaenzi wanawake?!!!! |
YALIYOMO
TAHARIRI
Wananchi washutumu vyombo vya habari Lipumba awaambia wananchi wasibabaishwe na walioko madarakani Wasomi SUA walaani ‘rushwa’ ya kisiasa Polisi kataeni kutumiwa - Lipumba Maelfu ya tani za matunda yanaoza Tanga Habari za ndani
MPASHO NASAHA
HABARI
Ushauri Nasaha
Makala
MAKALA
MAKALA
Kalamu ya Mwandish
MAKALA
RIWAYA
Lishe
|
|
|
|
|