|
Na. 043 Jumatano Aprili 12- 18, 2000 |
|
|
|
|
|
Museveni awasaka Wakristo wauaji KAMPALA, Uganda, SERIKALI ya Rais Museven wa Uganda imetangaza kutoa donge nono la dola 1300 za Kimarekani kwa yeyote atakayesaidia kupatikana kwa viongozi wa Kikristo waliosababisha vifo kwa kuungua moto mamia ya waumini. Wiki iliyopita serikali hiyo ilitamka rasmi kuwakamata mara wakionekana wadhamini sita wa dhehebu hilo linalojiita Kuhuisha amri kumi za Mungu. Mwishoni mwa mwezi Machi mwaka huu, huko Kanungu nchini Uganda Kanisa moja liliwaka moto na wahanga mamia walipoteza maisha. Kufuatia tukio hilo, serikali ya Uganda imechukua hadhari ikiwemo kuzifanyia utafiti dini na madhehebu mbalimbali zinazosadikiwa kuwafundisha waumini wake kibubusa. Inasemekana viongozi hao wamekimbilia baadhi ya nchi jirani ikiwemo Congo Kinshansa. Uganda nchi iliyopo Afrika
ya Mashariki ina idadi kubwa ya waumini wa dini ya Kikristo na Waislamu
ni asilimia 30.
Wairaq milioni moja wafa kwa vikwazo AMMAN, Waziri wa Afya wa Iraq, Umid Medhat Mubarak Jumatatu alisema kwamba zaidi ya Wairaq milioni moja, wengi wao wakiwa watoto, walikufa kutokana na vikwazo vya Umoja wa Mataifa ambavyo vimechukua miaka kumi sasa. "Kiwango cha vifo vya watoto wachanga kimepanda nchini Iraq kufuatia vikwazo hadi kufikia vifo 108 kwa kila watoto 1000 wanaozaliwa wakati ambapo kabla ya vikwazo kulikuwepo vifo 42 kati ya 1000 wanaozaliwa", Mubarak aliwaambia waandishi. Alihitaja kwamba idadi ya vifo vilivyosababishwa na vikwazo ni 1,294,882, kati yao 523,204 walikuwa watoto wa chini ya umri wa miaka mitano. Umoja wa Mataifa uliiwekea vikwazo Iraq mwaka 1990 baada ya kuivamia Kuwait mwaka 1989, mwaka mmoja kabla Umoja wa Mataifa haujaweka vikwazo, madaktari walifanya operesheni 151,525 kwa kila mwezi kulinganisha na sasa ambapo operesheni kama hizo ni 4442 tu kwa mwezi. Pia Waziri huyo alilaumu vikwazo kwamba ndiyo chanzo cha utapiamlo ambao unasababishwa na uzazi kabla ya muda wake na kuenea kwa magonjwa ya kuambukiza kama kipindupindu, magonjwa ambayo yalishakoma katika Iraq kabla ya 1990. Waziri wa Afya wa Iraq alianzisha kampeni ya kitaifa mnamo Machi 28 ya chanjo kwa watoto milioni 3.5 walio chini ya umri wa miaka mitano dhidi ya maradhi ya polio. Hatua ya pili ya kampeni hii itaanza Aprili 25. Shirika la Afya Ulimwenguni
liligundua ongezeko kubwa la idadi ya watoto wa Iraq wanaougua pepopunda
(polio) na lilitoa kauli ya hofu kwamba ugonjwa huo ungeenea.
G77 kukuza ushirikiano HAVANA, Cuba MATAIFA yanayoinukia kimaendeleo hii leo katika mkutano wa kilele yanatarajiwa kupitisha azimio la ushirikiano wa nguvu kati yake na nchi changa. Naibu Waziri Mkuu wa Cuba akizungumza hapo jana katika matayarisho ya mkutano huo amesema kuwa nchi yake inatoa mwito wa kuunda mfumo moya wa kutukuza utu. Mfumo ambao amesema utaondoa au kupunguza pengo kubwa lililopo kati ya maskini na matajiri. Ushirikiano wa mataifa hayo utatilia mkazo kuwekeza biashara na rasilimali, kukuza uchumi, ubadilishanaji wa fedha pamoja na ujuzi, ufundi wa teknolojia mpya. Mataifa yanayoendelea yajulikanayo kama G77 yaliunda umoja huo mnamo mwaka 1967 azimio la biashara la UNCTAD mnamo 1964. Zaidi ya nchi 160 zinatarajiwa
kuwakilishwa na wakuu wa nchi zao, wajumbe 122 kutoka sehemu mbalimbali
na wasio wanachama wapatao 34 watashiriki.
Hizbullah wanusurika MSEMAJI wa kikundi cha wapiganaji wa Kiislamu Hizbullah amesema jana kuwa mabomu yaliyorushwa na ndege za Israel hayakuua wala kujeruhi. Ndege za kivita za Israel jana zilidondosha mabomu katika eneo walipo Hizbullah kusini mwa Levnan. Wapiganaji hao wanapambana na Israel kusini ili kurudisha ardhi yao ambayo ilitekwa na Israel. Israel inakalia milima ya Golan kwa mabavu, iliteka milima hiyo katika vita yake na Syria mnamo miaka ya sitini. |
YALIYOMO
Tahariri
Waislamu waapa kuinyima kura CCM Mkapa
ahutubia Taifa:
Wananchi wamuunga mkono Askofu Kakobe MPASHO NASAHA
SHERIA
Ushauri Nasaha
MAKALA
WAZO LA WIKI
MAKALA
Kalamu ya Mwandishi
MAKALA
Makala ya Mtangazaji
Riwaya
Lishe
•••Golikipa Majimaji alia na mabeki |
|
|
|
|