|
Na. 043 Jumatano Aprili 12- 18, 2000 |
|
|
|
|
|
Ni kwa jinsi gani wanawake wanapata utapiamlo CHAMOS, H.J MAKALA iliyopita tuliona jinsi mume alivyo na wajibu wa kulea ujauzito, katika nyanja mbalimbali.Katika makala hii, kwa kuzingatia umuhimu wa afya ya mama, nimeona ni bora tukafahamu ni sababu zinazopelekea wanawake kuwa na lishe duni (Utapiamlo). Hii itasaidia kuwaweka wanawake katika hali ya ubora unaofaa zaidi, ndani ya jamii zetu. Awali ya yote, wanawake wanaweza kuwa wamepata utapiamlo tangu wangali wadogo na pengine kuendelea na utapiamlo kwa muda wote wa maisha yao. Mtoto wa kike aliyezaliwa na uzito mdogo, au ambaye hakupata lishe bora (utapiamlo) katika miaka mitatu ya mwanzo, hudumaa na baadae huwa mwanamke mfupi. Wakati mwingine wanawake hawali chakula cha kutosha kufikia mahitaji yao,ikwa ni sababu itokanayo na umasikini wa familia, jamii au nchi kwa ujumla mfano Tanzania. Lakini pia lipo tatizo lingine ambalo linaweza kuungwa kwenye sababu niliyoitaja hapo juu japo si moja kwa moja. Nalo ni kwa baadhi ya jamii kuwapa kuwapa wanaume chakula kingi zaidi kuliko wanawake kutokana na sababu mbalimbali katika mila zao. Kazi ngumu pia huwasababishia wanawake utapiamlo. Katika jamii zetu za kiafrika wanawake hutumia masaa mengi zaidi wakiwa kazini kuliko wanaume, sababu inayowafanya wahitaji nguvu zaidi. Sasa endapo wanatumia nguvu nyingi zaidi kuliko zile wazipatazo toka kwenye chakula, basi wanapoteza uzito na hatimaye kudhoofika(utapiamlo). Kwa upande wanawake walioko vijijini hali huwa ni mbaya zaidi, kwani wao hufanya kazi zaidi hasa katika kipindi cha kilimo ambacho mara nyingi huambatana na upungufu mkubwa wa ziada ya chakula ha hivyo wanawake huzidi kudhoofu. Mbaya zaidi ni kwamba wajawazito pia hushirikishwa katika shughuli zote hizi kama wanafamilia wengine? bila kujali kuwa wajawazito huhitaji kuwa na mapumziko. Sababu nyingine ni kutokula vyakula vya aina mbalimbali vya kutosha hata kama vinapatikana, jambo ambalo lnawafanya wakose virutubisho muhimu. Mfano, iwapo mwanamke atakosa madini ya chuma au folate, ambayo humkinga na ukosefu wa damu (anaemia), huishia kwenye kupungukiwa damu mwilini na kudhoofu. Tukumbuke kuwa wanawake hupoteza damu kila mwezi; kuliko watu wengine, hivyo wanahitajika kuitunza na kuiongeza wakati wote. Kwa upande mwingine, wanawake wanapokuwa wajawazito, hawapati lishe ya ziada ili kufidia ile sehemu itumikayo kujenga mwili wa mtoto. Na iwapo hapati chakula cha ziada, sehemu za mwili wake hutumiwa katika matumizi ya mtoto! Hivyo mama hudhoofu zaidi.Wanawake masikini ndio huathiriwa zaidi, kwani hushindwa kuongeza manunuzi ya chakula anapokuwa mjamzito na hatimaye kuzidi kudhoofu. Kipindi cha unyonyeshaji pia huchangia utapiamlo kwa wanawake. Wanawake wanaonyonyesha huhitaji virutubisho na nguvu zaidi ili kuweza kutengeneza maziwa. Na iwapo kipindi hiki cha unyonyeshaji, mama hatapata vyakula vya kutosha na vya ziada, hulazimika kutumia sehemu za mwili wake (stored nutrients) kwa ajili ya kutengenezea maziwa. Hii huwakondesha na kuwadhoofisha kabisa wanawake. Mara nyingine wanawake huzaa wakiwa wangali wadogo. Hutokea baada ya kubalekhe tu anabeba mimba hali ya kuwa bado yeye mwenyewe anakua. Matokeo yake, yeye na mtoto hugombea chakula. Hii huishia kwenye makuzi duni ya mama na mtoto atakayezaliwa. Hivyo ndivyo wanawake hupata utapiamlo katika jamii. Na kwa kuwa lengo letu ni kupata jamii yenye afya bora, ni vyema kuwaandaa zaidi wanawake ambao ndio wazazi na walezi wa jamii hiyo. Kwa upande wa wazaz, ni jambo la muihimu kumlea mtoto wa kike katika misingi bora zaidi ya afya ukizingatia athari ya lishe duni, anapokuwa mkubwa. Bila kuwasahau watoto wa kiume,ambao baadhi jamii yetu huwapa kipaumbele watoto wa kiume na kuwapenda zaidi kulikowa kike. Tuitambue nafasi ya mwanamke ili tumtunze inavyostahiki. Kwa upande wa waume, ni
wajibu kwao kuwatunza wake zao kwa kuzingiatia umuhimu wao. Wapewe lishe
inavyostahiki kadri ya uwezo uliopo. Na sio kumaliza pesa kwenye mambo
ya kipuuzi huku nyumba(familia) inaangamia. Wanawake wapunguziwe uzito
wa majukumu, hasa kulingana na afya na uwezo. Hakika wanawake si zana za
kufanyia kazi, bali ni viumbe maalum, kwa kazi maalum!!
|
YALIYOMO
Tahariri
Waislamu waapa kuinyima kura CCM Mkapa
ahutubia Taifa:
Wananchi wamuunga mkono Askofu Kakobe MPASHO NASAHA
SHERIA
Ushauri Nasaha
MAKALA
WAZO LA WIKI
MAKALA
Kalamu ya Mwandishi
MAKALA
Makala ya Mtangazaji
Riwaya
Lishe
•••Golikipa Majimaji alia na mabeki |
|
|
|
|