|
Na. 043 Jumatano Aprili 12- 18, 2000 |
|
|
|
|
|
NASAHA
Wanaokemea dhuluma wasinyanyaswe DHULUMa ni kitu cha hatari sana katika jamii, kuiepusha hatari ya dhuluma isije itumbukiza jamii katika maafa hapana budi katika jamii hiyo watokee watu watakaowakabili madhalimu kuwataka waache dhuluma dhidi ya wenzao, na hao madhalimu waache mara moja kudhulumu. Hapa kwetu nchini kuna dhuluma: Serikali inawatendea visivyo baadhi ya raia wake. Tunashukuru kwamba wamekuwa wakijitokeza watu kuikabili serikali na kuitaka iache dhuluma. Hili ni jambo zuri sana. Lakini wametokea watu ambao wanajiona kuwa wao wanahaki zaidi na wana uchungu zaidi na nchi hii kuliko Watanzania wengine. Hawa hawachelewi kuyaelekeza mambo kule wanapopataka wao hata kama ni kinyume na hali halisi. Watu hawa ama wanayo madaraka ya kisiasa au ya kidini na wanasaidiwa na wale wenye kumiki vyombo vya habari. Wao wakisema chochote, hicho ndio huwa 'sadakta', lakini akisema mwingine asiye 'mwenzao', huyo hupewa majina ya kumkosanisha na jamii, hutangazwa kuwa yeye "mchochezi",, "anataka kuvuruga amani", "anachanganya dini na siasa", n.k. Ni vema wale wote walio madarakani na wale wanaowaunga mkono kwa kila wanalosema watambue kuwa waliowaingiza madarakani ni sehemu ndogo tu ya Watanzania wanaowaongoza. Tunasema hivi kwa sababu siku zote si wananchi wote wanaostahiki kupiga kura hujiandikisha kupiga kura, na katika hao wanaojiandikisha si wote wanaojitokeza siku ya kupiga kura; na hata hao wanaojitokeza huwa wapo wasiompa kura zao mgombea anayetokea kushinda. Hivyo aliye madarakani kwa kura za wananchi akae akijua kwamba kauli za wale wasio madarakani kama yeye au wale wasio upande wa chama chake ni muhimu sana kutiliwa maanani katika uendeshaji salama wa nchi. Wamesimama Watanzania wenzetu, wameiambia serikali ya chama tawala juu ya dhuluma inazowafanyia raia wa nchi hii kutokana na utendaji wake mbovu. Amir wa Shura ya Maimam, Sheikh Juma Mbukuzi, amekuwa akiitanabaisha serikali juu ya madai ya Waislamu kwa serikali. Serikali haikukawia, Sheikh huyo akatangazwa kwa majina mabaya na akafunguliwa kesi mahakamani. Yupo Prof. Ibrahim Lipumba Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF). Naye amekuwa akiitahadharisha Serikali kutokana na uendeshaji mbaya: Wakati wananchi wanakosa 'aspirin' hospitalini, serikali inadiriki kutenga Shilingi bilioni tatu kupaka rangi Ikulu. Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Bible Fellowship, Zacharia Kakobe juzi juzi kachambua udhaifu uliomo ndani ya CCM. Lakini badala ya tahadhari zilizotolewa na wenzetu hao kutiwa maanani na wale walio madarakani, tumeshuhudia wakishambuliwa kwa maneno. Hatari zaidi ni pale vyombo vya habari, badala ya kuripoti yaliyosemwa na watu hao, vikajipa kazi ya "ujaji" na pia kucheza (kuitika) wimbo wa serikali kwamba waonyaji hao wanataka kuvuruga amani nchini. Lakini tunaamini kwamba wanaendeshaji wa vyombo hivyo vya habari wanafahamu vizuri athari za kuilea (kuitetea) dhuluma katika jamii. Mabeberu wa nchi za Ulaya walimpandikiza Mobutu huko Zaire na kumdhulumu uhai Hayati Bw. Patrice Lumumba. Alichokijua Mobutu ni dhuluma juu ya dhuluma hali iliyopelekea Wakongamani kuhiyari kumwaga damu ili kujikomboa! Rwanda na Burundi mambo ni hayo hayo. Kundi lililo madarakani halikuwa likitenda haki sawa kwa wote. Hapakuwa na misho mwingine katika nchi hizo bali ni damu ya wananchi katika kila upande kumwagika. Zanzibar ilipata uhuru wake 1962. Hata hivyo walioshika madaraka wakati huo walikuwa wakifanya dhuluma. Hapakuwa na jinsi bali damu ya ndugu zetu ilibidi imwagike kukomesha utawala wa dhuluma 1964. Afrika ya Kusini ilipata uhuru wake 1925. Lakini Wazungu wachache wakaiweka serikali mikononi mwao na hawakuwa wakitenda haki. Waafrika kadhaa wakapoteza maisha yao katika harakati za kukomesha udhalimu wa Wazungu hao. Tunaamini kuwa haya yote wanahabari hao wanayajua na mafunzo yaliyomo ndani yake wanayajua, bali tu wameamua kuyapeleka mambo katika 'staili' yao. Tunasema hatutamani siku moja ulimwengu ulazimike kuanzisha mahakama ya kimataifa kushughulikia 'watuhumiwa' wa vita na dhuluma (mauaji) ya Watanzania kama ilivyo mahakama iliyopo Arusha kwa ajili ya Burundi. Pia hatutamani siku moja, Rais atakayechukua madaraka hapo baadaye alazimike kuanzisha Tume ya Ukweli na Maridhiano kama ile aliyoianzisha Mzee Nelson Mandela kutoa nafasi kwa wale waliofanya dhuluma wakati wa utawala wa kibaguzi na mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi warudishe imani kwa wale wote waliowadhulumu. Hivyo basi tahadhari zilizotolewa na akina Sheikh Mbukizi, Profesa Lipumba na Askofu Kakobe kuhusu utawala mbovu usiojali raia, zizingatiwe. Aidha tunapenda serikali iyakumbuke yale yaliyosemwa na Askofu Shayo mjini Zanzibar wakati wa Sherehe za Krismas na yaliyoongezewa na kadinali Pengo siku chache baadaye jijini Dar es Salaam, ingawa kauli zao tunadhani zimezingatiwa na zinaheshimiwa. |
YALIYOMO
Tahariri
Waislamu waapa kuinyima kura CCM Mkapa
ahutubia Taifa:
Wananchi wamuunga mkono Askofu Kakobe MPASHO NASAHA
SHERIA
Ushauri Nasaha
MAKALA
WAZO LA WIKI
MAKALA
Kalamu ya Mwandishi
MAKALA
Makala ya Mtangazaji
Riwaya
Lishe
•••Golikipa Majimaji alia na mabeki |
|
|
|
|