NASAHA
Na. 043 Jumatano Aprili 12- 18, 2000
Ukurasa wa mwanzo
Islam Tanzania
Matoleo yaliyopita
Wananchi wamuunga mkono Askofu Kakobe 
  • Wataka CCM, Serikali iache vitisho 
  • Wasema kila kiongozi wa dini ana haki ya kukosoa sio Wakatoliki tu 
Na Mwandishi Wetu

WANANCHI mbalimbali wameendelea kukilaumu Chama Cha Mapinduzi kutokana na kero zinazowakabili raia na wamekitaka chama hicho kuleta mabadiliko badala ya kuendelea kuwatisha raia wanaokikosoa chama hicho tawala.

Wanachi hao wamekuwa wakitoa maoni yao kufuatia kuzuka kwa vita vya maneno kati ya Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship, Bw. Zakaria Kakobe na kiongozi mmoja wa kitaifa wa CCM, Bw. Emmanuel Nchimbi. 

"Shida zote hizi ni sababu yao CCM, wao wanatanua kila siku na wala hawashituki kama sisi tupo na tunaumia", alisema Bw. Adolphonce Mikina, mfanyabiashara wa Manzese. Bw. Mikina ameilaumu CCM na kudai kuwa umri wa chama hicho haufanani na uwezo wake wa kuongoza nchi. 

"Tuliipigia kura CCM kwa vile tulijua ni chama chenye uzoefu kuongoza nchi, lakini leo hii kila unapokwenda unadaiwa rushwa... na wao wala hawatusikilizi, tunaumia peke yetu", alisema Bw. Mikina anayekadiriwa kuwa na umri wa zaidi ya miaka 40. 

Mwananchi mwingine, Bw. Abdillah, amesema wananchi wa kawaida ndio wanaotaabika kutokana na serikali kutowajali. 

"Mimi sioni kama huyu Askofu amewazulia CCM, mkitaka kero za chama hiki tuulizeni sisi watu wa kawaida", alisema Bw. Abdillah bila kufafanua "watu wa kawaida" ni watu wa aina gani. 

"Hapa nilipo akili inanizunguka, siku yoyote mwanangu atasimamishwa shule shilingi 20,000 ya kukamilisha ada imenishinda", alisema mwananchi huyo. 

"Redioni wanatangaza kutokomeza umasikini lakini hatupati msaada wowote, wanatangaza wasiyoyatenda ndio maana Kakobe anawaita wanafiki", aliongeza Bw. Abdillah. 

Mwananchi mwingine amesema CCM inaendelea kuwagawa Watanzania na kuleta matabaka kwa "tabia yake ya kuwafumbia macho viongozi wa dini moja na kuwasakama viongozi wa dini zingine." 

Mwananchi huyo ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini alisema, "Maaskofu wa Katoliki wanasema watakavyo hakuna wa kuwagusa, lakini dini zingine hawatakiwi kufurukuta." 

Akiendelea kutoa maoni yake mwananchi huyo alitahadhirisha kuwa tabia hiyo ya serikali "kuwadekeza" Maaskofu Wakatoliki kutaifikisha nchi pabaya kwa vile waumini wa dini zingine nao watachoshwa na upendeleo huo wa serikali kwa Wakatoliki. 

Mwishoni mwa mwaka jana, Askofu Shayo alipokuwa akizungumza katika sherehe za Krismas aliilaumu serikali kwa kushindwa kutoa huduma muhimu kwa wananchi hali ambayo Askofu huyo wa Kanisa Katoliki alisema inaweza kuleta machafuko nchini. 

Miezi michache baadaye Askofu wa Jimbo la Dar es Salaam na kiongozi wa Kanisa Katoliki nchini, Polycarp Kadinali Pengo alikemea CCM kuwa ni kichaka cha wahuni na akaitaka ijisafishe. 

Chakushangaza, wameeleza wananchi waliotoa maoni yao, viongozi hao wa Kanisa Katoliki hawakukemewa na serikali wala CCM yenyewe. 

Mbali na Askofu Kakobe kukemewa na Chama Cha Mapinduzi,kiongozi mwingine wa kidini aliyewahi kusakamwa na serikali baada ya kuitahadharisha CCM na Serikali yake juu ya dhuluma wanazofanyiwa wananchi ni Amir wa Shura ya Maimam, Sheikh Juma Mbukuzi ambaye alifunguliwa mashitaka. 
 

Juu
 

YALIYOMO
 

Tahariri
Wanaokemea dhuluma wasinyanyaswe

Waislamu waapa kuinyima kura CCM

Mkapa ahutubia Taifa: 
Ugumu wa maisha kuendelea

Wananchi wamuunga mkono Askofu Kakobe

MPASHO NASAHA
WAKIAMUA, HATA WAKICHAFUKA WATANAWA!!!

SHERIA
Faida ya kuwepo kwa sheria za haki kunategemea na wanaozisimamia

Ushauri Nasaha
Namna ya kumfanya mtoto wako aweze kuzungumza

MAKALA
Sababu ‘1000’ kwanini tunataka CCM ing’oke madarakani - 2

WAZO  LA  WIKI
Polisi acheni ubalakala

MAKALA
Kuporomoka kwa maadili  katika jamii yetu; Sababu na utatuzi wake - 2

Kalamu ya Mwandishi
Tatizo si jino kwa jino, bali utekelezaji muafaka!

MAKALA
Uchaguzi Mkuu Mwaka 2000 (6)
Vijana mjiandikishe kwa wingi na siku ya uchaguzi mjitokeze

Makala ya Mtangazaji
LEO NI SIKU YA ASHURA

Habari za Kimataifa

Riwaya
Kisasi cha mauti -3

Lishe
Ni kwa jinsi gani wanawake wanapata utapiamlo

MASHAIRI

MICHEZO

  • Madadi, Jamhuri acheni ‘rusha roho’ katika soka – Wapenzi
  • Yanga wakumbwa na kiwewe
  • Mapunda asema hana bahati ya kutia mabao

  • •••Golikipa Majimaji alia na mabeki 


       Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:Bonyeza hapa
    Au
    Andika barua  kwa: nasaha1420@yahoo.com

    Ukurasa wa mwanzo
    Islam Tanzania
    Matoleo yaliyopita