|
Na.163 Rabiul Thani 1419, Agosti 21 - 27, 1998 |
|
Aya ya 256 - 257 Hakuna kulazimishwa kuingia katika
dini
Sehemu ya pili ya aya inasema yule ambaye amemkanusha Twaghuut na akamuamini Allah basi huyu ameshikilia mashiko madhubuti. Abul-A’la Maududi katika uchambuzi wake wa Twaghuut anaelezea: Neno la Kiarabu Twaghuut katika lugha linamuhusu kila mtu anayechupa mipaka. Qur’an inalitumia neno hili kwa kila mtu anayemuasi Allah na akajidai yeye mwenyewe ubwana na mamlaka yasiyo na mipaka juu ya waja wa Allah na kisha akatumia nguvu kuwalazimisha kuwa watumwa wake. Uasi dhidi ya Allah una daraja tatu za uovu: (1) Yule ajulikanaye kama Fasiq iwapo anakubali kuwa ni mja wa Allah lakini matendo yake ya kila siku yanakwenda kinyume na amri zake (Allah). (2) Yule ajulikanaye kuwa ni Kafri iwapo yeye hujitenga moja kwa moja na utegemezi wa Allah au anayemtumikia kwa utii mwingine kinyume na Allah. (3) Twaghuut n i yule ambaye anafanya uasi dhidi ya Allah na kisha akajitahidi kuwafanya waja wa Allah kuwa ni waja wake yeye badala ya Allah.Twaghuut anaweza kuwa ni shetani au kiongozi wa dini au kiongozi wa kisiasa kama mfalme au serikali. Kwa sababu hiyo mtu hawezi kuwa muumini wa kweli bila ya kumkanusha au kupingana na Twaghuut. Kwa lugha nyingine Twaghuut ni daraja ya juu ya uasi kwani inakusanya mtu kuasi yeye na kisha kuwalazimisha wengine uasi. Kwa kuwa Waislamu wanaoishi katika zama zetu karibu sote tumo chini ya mifumo ya kitwaghuut; suala la kupambana na Matwaghuut ni lazima liwe ni mfumo wetu wa maisha. Vinginevyo Uislamu wetu utakuwa mashakani kama si kutokuwepo kabisa. Kuishi chini ya hali hiyo ndiyo salama yetu kwani tutakuwemo kwenye kivuli cha hadithi ya Mtume (s.a.w.) ya njia tatu za kukataza maovu - kutumia nguvu; kukaripia maovu au kuchukia maovu. Kushabikia maovu au serikali zilizopo ni kukubali kuwa mfuasi mtiifu wa Twaghuut. Aya ya 257 Mwenyezi Mungu ni Mlinzi wa wale walioamini - huwatgoa katika giza na kuwaingiza katika nuru. Lakini wale walikufuru; walinzi wao ni Matwaghuut - hjuwatoa katika nuru na kuwaingiza gizani. Hao ndio watu wa Motoni, humo watakaa milele. Aya tuliyoishia nayo inaeleza kuwa yule ambaye amemkanusha Twaghuut na akamuamini Allah basi huyo ameshika kitu madhubuti kabisa. Katika aya hii Allah anaeleza huo umadhubuti wa hicho kishiko ambacho kinahusiana na Yeye Mwenyewe akiwa Mlinzi wa wale walioamini. Kazi yake ni kuwatoa waliomuamini Yeye kutoka katika viza vya upotofu, ujinga, maovu ya kiroho na mengine n.k. na kuwaingiza katika nuru ya haki na ukweli wa maisha. Matumizi ya neno giza ndani ya Qur’an siku zote katika maana ya hapa yamekuja kwa wingi - dhulumat’; kinyume na nuru ambayo imetumika kwa uchache. Hikma ya matumizi haya inasadikiwa ni kuonyuesha kuwa viza ni vingi kwani vinaashiriwa na dini (mifumo ya maisha) zinazobuniwa na wanaadamu kuwa ni nyingi lakini hakuna hata moja inayoweza kumuongoza binaadamu kwa ufanisi. Kwa upande wa pili mfumo wa hakika (dini) unao muhakikishia binaadamu kuwa yuko salama ni mmoja tu ambao ni Uislamu. Kwa lugha nyingine, Ukristo, Uyahudi, Ubepari, Ukoministi, Uhindu, Ufursi, Ulokole, Ujamaa, Ubahai, Utalii (Tourism) n,k, ni viza wakati Uislamu pekee ndiyo nuru ambayo Allah huwaongezea huko wale waliomuaminiYeye. Kinyume na wale waliomuamini Allah na akawa Mlinzi wao; wale waliokufuru mlinzi wao ni Twaghuut ambaye kazi yake kubwa ni kuwatoa katika njia ya haki - Nurfu (Uislamu) na kuwaingiza katika viza (njia potofu za maisha). Ingawa neno lililotumika hapa ni Twaghuut kwa uchache lakini inapewa tafsiri ya wingi kwasababu mtu yoyote ambaye anamkanusha Allah na kuamua kuishi kwa kufuata mfumo wowote wa masiah usio Uislamu basi anakuwa mtumwa si wa Twaghuut mmoja bali Matwaghuut kadhaa wenye maumbile na hali tofuati. Kinara wa Matwaghuut ni Ibilisi ambaye humuandalia mtu huyu namna kwa namna za udanganyifu wenye mvuto wa aina yake. Mbali na Ibilisi, Twaghuut mwingine aliyefichika kwa wegni na nafsi yake mwenyewe binadamu. Nafsi ya binadamu humfanya kuwa mtumwa na matamanio na matashi na kumuongoza kwenye kila aina ya upotofu na njia zilizokwenda upogo. Matwaghuut wengvine ni mke au mume, watoto, jamaa zake, kabila au familia, marafiki au taifa. Aidha Matwaghuu wengine ni viongozi wa kisiasa au kidini na hata serikali yake. Wote hawa ni Matwaghuut kwa mtu mmoja huyu na kila mmoja anamvutia kwenye yale anayoyatamani yeye wakati huyu mtu anabaki kuwa mtumwa anayejidanganya kuwa ataweza kuwaridhisha wote. Ni kwasababu kama hizo Allah alisema kuwa iwapo tutawatii wengi waliomo ardhini watatupoteza aliposema: "Na kama ukwatii wengi katika hawa waliomo ulimwenguni watakupoteza na njia ya Allah. Hawafuati ila dhana tu, na hawakuwa ila ni wenye kuzua (tu basi).(6:116). Kinyume na hivyo anaeleza tena: "Sema: "Hii ndiyo njia yangu, ninaita (ninalingania) kwa Allah kwa ujuzi wa kweli - mimi na wanaonifuata......(12:108). Kwa hiyo bado tunatilia mkazo kuwa njia ya Allah (Nuru) ni moja tu ambaye
aliilingania Mtume (s.a.w.) na sasa inalinganiwa wa Waislamu wa kweli siyo
wale wafuasi wa Matwaghuut waliojivika vilemba na kujipachika madaraka
bila ya haki.
|
Milipuko ya mabomu Dar, Nairobi: Waislamu
walaani vyombo vya habari
Wanawake Waislamu Tanga waazimia kupigania
haki
Marekani yashambulia Sudan, Afghanistan Maoni: Kulipuliwa kwa Ubalozi wa Marekani:
Nguruwe kuzua tafrani Kibamba
Sheikh Mbukuzi ataka vijana
wajihadhari na utamaduni wa Magharibi
TAMPRO kuzindua Tawi Iringa
Tamasha la kusaidia wagonjwa
laanza Moro
Kambi ya matibabu ya Macho Tanga
yaanza
MAONI: Kanisa mshiriki wa ukandamizaji Porojo za Ngatara
Ubatizo kupitia TVZ?
MAPENDEKEZO YA KATIBA YA
Hoja binafsi: Uhusiano na Marekani
usituletee maafa
Wanamume toeni haki za
wanawake kuepusha ufisadi
MAKALA: Hoja za kutofautisha Yesu
na Issa ni udhaifu, ni uzushi mtupu! - 2
Mwanaadamu alipofikia
|
Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:
Bonyeza hapa
Au
Andika barua kwa: webmaster@islamtanzania.org