AN-NUUR
Na.163 Rabiul Thani 1419, Agosti 21 - 27, 1998
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
Chakula na lishe

Na Mujahiid Mwinyimvua

KATIKA miaka ya sitini na sabini, serikali mbali mbali duniani ziliwahamasisha kina mama kuacha kuwanyonyesha watoto wao maziwa ya mama. Na badala yake watumie maziwa ya kopo.

Juhudi hizo zilizaa matunda yaliyokusudiwa. Yaani kina mama wengi waliacha kuwanyonyesha watoto wao maziwa ya mama, na badala yake waliwanyonyesha maziwa ya kopo (bottle feeding).

Hata hivyo teknolojia hiyo mpya ilileta maafa ya maelfu ya watoto wadogo katika nchi mbali mbali. Hii ni kwa sababu, maziwa ya kopo hayana kinga, yanagharama kubwa, yanahitaji muda wa kuyaanda na usafi wa hali ya juu. Pia maziwa ya kopo hayana virutubisho vyote anavyovihitaji mtoto mchanga.

Baada ya maafa hayo, katika miaka ya hivi karibuni serikali kadhaa duniani zimeanza kuwahimiza kinama kuirudia teknolojia asilia. Yaani kuwanyonyesha watoto maziwa ya mama.

Hata hivyo, maisha yetu ya kila siku yanatuonyesha kwamba, kuna kinamama kadhaa hasa katika mji ambao hawajawa tayari kuirejea teknolojia hiyo ya asili, licha ya faida zake nyingi kama zinavyowekwa wazi sasa na elimu ya sayansi.

Baadhi ya kina mama hao wasiotaka kuwanyonyesha watoto wao maziwa ya mama wanaona jambo hilo ni kero na lina wanyima muda na uhuru wa ‘kustarehe’ (kwenda Bar, ufukweni, kwenye kumbi za muziki, kwenye makasino, kwenye pati, n.k.

Pia wapo wale wanaoona kwamba ‘kero’ ya kunyonyesha maziwa ya mama itawazesha mapema na pia wataonekana kuwa hawaendi na wakati!

Kwa kuzingatia kasoro hiyo, iko haja kwa vyombo vya habari kuongeza juhudi za kuwahamasisha kina mama na jamii kwa jumla ili kuirejea teknolojia ya kuwanyonyesha watoto maziwa ya mama. Makala hii inalenga katika azma hiyo. Kwa kuielimisha jamii faida zinazopatikana katika maziwa ya mama yanapotumika kwa unyonyeshaji watoto wadogo.

Awali ya yote maziwa ya mama ni mlo kamili wenye mchanganyiko wa virutubisho vyote inavyoweza kumpa mtoto afya kwa kipindi cha miezi minne ya kwanza bila ya kuihitaji nyongeza ya chakula kingine.

Maziwa ya mama pia ni chakula na kinywaji kilicho safi na salama. Vilevile maziwa ya mama yanakinga kwa mtoto na vilevile tayari muda wote.

Pamoja na faida hizo, maziwa ya mama yana gharama nafuu yakilinganishwa na yale ya kopo. Vilevile maziwa ya mama hayachafui mazingira. Kwa maneneo mengine maziwa ya kopo (makopo na mifuko iliyowekwa maziwa) yanachafua mazingira.

Zaidi ya hayo, teknolojia ya kumnyonyesha mtoto maizwa ya mama inaongeza mapenzi baina ya mtoto na mama. Pia utafiti wa kisayansi ulioripotiwa hivi karibuni na jarida la American Academy of Pediatrics", umeonyesha kwamba unyonyeshaji wa maziwa ya mama hasa kwa muda mrefu unaongeza uwezo wa utambuzi kwa mtoto.

MIONGONI mwa magonjwa mabaya kabisa ambayo ni aghalabu kutibika wayapatayo wala nguruwe ni kuhara damu. (Rejea Animal Parasibes and Human Diseases, page 7, By Dr. Chandler).

Ugonjwa mwingine wa hatari unaowapata "wateja" wa kharamu hiyo ni "Trichinosis" unaoambukiza halaiki kwa wakati mmoja!

Ugonjwa huo unatokana na minyoo hatari iitwayo "trichina" ambayo hupatikana katika mwili wa nguruwe.

Mwaka 1968 mwezi wa tano huko Berlin Wisconis Ujerumani, watu wanne wote kutoka familia moja waligundulika kuwa na trichinosi, baada ya kupata ugonjwa ufananao na mafua. 

Uchunguzi umeonyesha kuwa Wajerumani hao "waliichapa" mikate mitamu ya hambaga yenye "utajiri mkubwa" wa nyama ya nguruwe ndani yake.

"Kutokea ghafla kwa trichinosis bado ni jambo la kawaida katika Amerika". Anaeleza Dk. Glen Shapherd katika "Washington Post" la Mei 31, 1952 akielezea gonjwa hilo ambalo mamia kadhaa ya wala nguruwe umewaacha na kilema cha maisha.

"Mtu mmoja kati ya watu sita huko Amerika (USA) na Canada amekumbwa na Trichinosi (Trichinelly )… watu wote hawa walikuwa wakiitafuna minofu ya nguruwe bila kujali… Hauna matibabu si dawa zenye uwezo wa kuwaua bakteria wala sindano zinazoweza kuangamiza minyoo hii hatari na midogo mno. Njia pekee ya kuepukana nayo ni kuzuia kutoambukizwa (yaani kuacha kula nguruwe)". 

Kwa mujibu wa bingwa huyo, minyoo hiyo ina kawaida ya kuishi katika kapsuli ndogo mno zisizoonekana machoni zikiwa na umbo la limao kwa zaidi miaka 40.

Kapsuli hizi ziko katikati ya msuli. Hivyo basi uroho wako wa nyama hiyo hukusababishia kula minyoo hiyo yenye ukubwa wa 1/8 ya inchi na unene wa 1/400 ya inchi!

Wadudu hawa huzaliana mwilini mwako huku kila mmoja ukiacha watoto 1,500 ambao hupenya kwenye damu kwa muda wa wiki kati ya moja hadi tatu tangu ulipokula nyama hiyo ya nguruwe.

Wataalamu wanathibitisha kuwa dalili za gonjwa hilo zinapatikana sana na dalili za magonjwa mengine zaidi ya 50 hivyo kuwaacha katika wakati mgumu mabingwa wa matibabu.

"Kwa kawaida inasemekana kwamba, kuwepo Trichina kwenye nguruwe ndiyo hasa msingi halisi wa Mayahudi kuharamishiwa nguruwe kuwa chakula" (Rejea Dk. WD. Foster katika "Historia of Parasitology – 1965).

Kwa kifupi tu minyoo hiyo ya trichina ni hatari na imeshaua wengi na kuwaacha wengine katika hali ngumu. Rejea CDC Veterinary Public Health Notes, 1969, February) pia pitia (Morbidty and Mortality weekly report Vol. No. 23 and Vol. 18 No. 9).

Aidha, nyama ya nguruwe ina "utajiri" mwingine wa minyoo hatari aina ya tegu (tape worms) au "Taenia solium" kwa lugha ya kitaalamu.

Imethibitishwa kuwa moja ya nji mushuhuri kama si maarufu mno ya kuambikiza minyoo hiyo ni kula nyama ya nguruwe.

Takwimu zinaonyesha kuwa hadi mwishoni mwa miaka ya 40, karibu watu milioni mbili waliikwaa minyoo hiyo. Rejea "This wormy word 1947 By MD. Stoll.

Miongoni mwa magonjwa mabaya kabisa ya ini, saratani na kifua yanayowasumbua mamia ya watu hivi leo ulimwenguni hutokana na minyoo hatari ya Clonorchis sinesis ambayo maskani yake ni katika maini ya nguruwe. Rejea utafiti na ugunduzi wa mabingwa Looss -–1907 na mtangulizi wake Cabbold – 1875.

Aidha, utaratibu wa ugunduzi wa Bw. Odliver – 1902 bila kusahau aliyemtangulia Linkaster – 1857, unaonyesha kuwa katika utumbo mdogo wa nguruwe kumejaa vijidudu vidogo vyenye athari mbaya kiafya kwa mla nguruwe ambavyo hufahamika kama Faciolopsis buski kwa lugha ya kitaalamu.

Pia ugonjwa wa mapafu (Pneumonia) ambao husababisha matatizo ya kuvuta pumzi kutokana na pafu kuwa zito ni zao la Paragonimus kimelea kilichopiga kambi yake ya kudumu katika mapafu ya nguruwe.

Kimelea hiki aidha hupelekea homa ya nyongo (Jaudice) ambayo huathiri vibaya ngozi ya mwili na rangi ya njano kutawala machoni pa mgonjwa. Rejea ripoti ya utafiti ya mgunduzi wa kijidudu hicho hatari Dk. Mason – 1880.

Ugonjwa mwingine usio na matibabu ya kueleweka hadi hivi leo, ambalo hutokana na ulaji nyama ya nguruwe ni "Erysipelas" unaosababishwa na kimelea kiitwacho "Erysipelothrix rhusiopathiae" kwa lugha ya kitaalamu. Rejea Chambers Encyclopaedia – 1968 Vol. 10 na American Peoples Encyclopaedia – 1960 Vol. 15.

Ukiacha utitiri wa magonjwa katika mnyama huyo, aidha ulaji wa nyama hiyo hupelekea upotofu uliopea wa kimaadili kama nilivyoeleza kwa kifupi mwanzoni mwa makala hii.

Mwandishi mashuhuri wa vitabu Saeed Akhtar anafafanua zaidi jambo hilo katika maandikio yake kadhaa juu ya nguruwe, "… Binadamu ameumbwa katika hali ya mwili, akili na roho, ubongo (maskani ya akili) ni sehemu ya mwili na hupata malisho kama zilivyo sehemu nyingine za mwili.

Mara zote utitiri wa chembe hai (cells) kwenye miili yetu hutumika kuendeshea sehemu kadhaa wa kadhaa za mwili", anasema Akhtar.

Aidha, anaendelea kusema kwamba, chembe hai nyingine zinazochukua nafasi ya zile zilizotumika kutokanana chakula tunachokula.

Chembe hizo za vyakula tulavyo huwa sehemu za mwili na baadhi yake huenda katika ubongo.

"Inajulikana sana kuwa chakula huathiri afya ya mwili. Lakini ni watu wachache sana watambuao athari za chakula katika ubongo… chakula safi, halali na kiliwacho kwa amani, hupelekea athari nzuri kiafya kwenye mwili na akili ya mlaji. Lakini kinyume chake, chakula hicho huwa na madhara makubwa mwilini". Anabaiisha mshika kalamu huyo wa Kiasia.

Akifafanua zaidi, Akhtar anasema kwamba nguruwe ni alama ya uchafu, ukosefu wa adabu, ulafi na uasherati popote pale ulimwenguni.

"Nguruwe ni chanzo cha upotoshaji wa uharibifu wa tabia za watu. Yote haja ni sababu nguruwe au mwasherati aso haya." Anatoboa Saeed Akhtar katika wimo wa maandishi yake "The pig".

"Watu walao nyama ya nguruwe…" Anaendelea kupasha mchanga maandiko huyu, "huathiriwa kidogo kidogo na uasherati wake wa asili, na tabia hiyo inapoathiri akili zao, utovu wa haya huwa desturi ya kila siku. Haya ni unyofu huwa mawazo ya kizamani ambayo hutupiliwa mbali na badala yake uasherati na upotovu huchukuliwa".

Tukiyatafakari maandiko ya Akhtar kwa kina, tunaiona picha halisi ya jamii yetu ya Kitanzania jinsi ilivyo hivi leo.

Kadri mabucha na mazizi ya nguruwe yanavyozidi kuongezeka, vitendo duni kabisa kimaadili ndivyo vinazidi kushamiri.
 
Madhara ya nyama ya nguruwe

WAISLAMU na wote wanaomtii Mola wao hawali nyama ya nguruwe kwa sababu moja muhimu. Ni kharamu. Mwenyezi Mungu Muumba aliye mjuzi wa yote; amekataza nyama hiyo kuliwa na watu. Hiyo ndiyo sababu ya msingi. Pamoja na hayo, juhudi za utafiti wa kisayansi zinaonyesha kwamba nyama ya nguruwe ina madhara mengi sana kwa afya ya watu. Hii ni pamoja na kuambukiza magonjwa mabaya.

Juu

YALIYOMO

TAHARIRI

Milipuko ya mabomu Dar, Nairobi: Waislamu walaani vyombo vya habari
Na Mwandishi wetu

Wanawake Waislamu Tanga waazimia kupigania haki
Na Ibn Masoud, Tanga

Marekani yashambulia Sudan, Afghanistan

Maoni: Kulipuliwa kwa Ubalozi wa Marekani:
Huu ni unazi au sehemu ya mtandao?

Nguruwe kuzua tafrani Kibamba
Na Mwandishi Wetu

Sheikh Mbukuzi ataka vijana wajihadhari  na utamaduni wa Magharibi
Na Said Shariff

TAMPRO kuzindua Tawi Iringa
Na Mwandishi Wetu

Tamasha la kusaidia wagonjwa laanza Moro
Rajab Rajab na Mussa Ally, Morogoro

Kambi ya matibabu ya Macho Tanga yaanza
Na Mwandishi Wetu

MAONI: Kanisa mshiriki wa ukandamizaji

Porojo za Ngatara
Na J. Hussein

Ubatizo kupitia TVZ?
Na Salahuddin Ahmad

Waislamu Kosovo waangamizwa

MAPENDEKEZO YA KATIBA YA 
SHIRIKISHO LA TANZANIA -2

Hoja binafsi: Uhusiano na Marekani usituletee maafa
Na Said Rajab

Darasa la Muhammad (s.a.w)

Wanamume toeni haki  za wanawake kuepusha ufisadi
Na Halima Issa Ndabi,  Mwanza

MAKALA: Hoja za kutofautisha Yesu na Issa ni udhaifu,  ni uzushi mtupu! - 2
Na Muhibu Said

Mwanaadamu alipofikia
Na Nineka B.N., Geita

Mafunzo ya Quran

Barua za wasomaji

Mashairi

Masomo ya dini ya Kiislam

Chakula na Lishe

Matangazo
 
 Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:
Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtanzania.org