AN-NUUR
Na.163 Rabiul Thani 1419, Agosti 21 - 27, 1998
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
Mwanaadamu alipofikia 

Na Nineka B.N., Geita

SIKU za kutubu ni hizi, siku za kujuta ni hizi, siku za majonzi ndizo hizi, siku za maovu makubwa ndizo hizi ambazo mwanaadamu mwenyewe amezisababisha kwa sababu ya uroho tamaa ya kujikusanyia mali, fahari na sura ya dunia ameiharibu yeye na sasa anatangatanga. Na baada ya kuiharibu dunia hakutosheka sasa ameanza kujiharibu yeye mwenyewe.

Akiwa mwanadamu mwenye umbile nyoofu na zuri, umbile la kupendeza na mwenye taratibu zinazotii kanuni za maumbile, ameasi kama alivyomwasi siku ile ya awalikalipokatazwa kuukaribia ule mti.

Anasemaanaweza kuunda mwanadamu kwa kuunga ‘seli’ na ‘seli’ fulani, akawa mtu. Anao uwezo wa kumbadili mwanaume akawa mwanamke, anao uwezo wa kumbadili mwanamake akawa mwanaume. Na sasa amepandilia ngazi kuelekea anakopenda yeye.

Nilishangaa niliposikia ndoa ya mwanaume kwa wanaume na ndoa ya wanawake kwa wanawake. Usistaajabu ya Musa, kumbe ya Firauuni makubwa zaidi. Huku Geita, mama mmoja tena mke wa mtu, kapelekwa danguloni na mlopa mmoja, kaambiwa siku hizi, mapenzi ya njia ya kawaida hayana bei, ila ya kaumu. Zogo lilivyotokea humo halisimuliki.

Wengine, wakafungishwa nikahi na majibwa kwa ajili ya malipo safi. Mbwa kuzama meli , mmoja kaaga dunia. Lisemwalo lipo, kama halipo laja. Si vema wala si jambo la hekima, kueleza jambo hili zaidi. Lakini katika hisia zako, unaweza kuupokea ujumbe huo kwa fikra gani?

Utundu wa mwanadamu umemfikisha mahali hapo leo, hatujui kesho itakuwaje? Je, ipo haja ya kuoa au kuolewa? Na hasa katika karne ijayo? Yako mambo mengi mno ya kujiuliza.

Kama mwanasayansi anao uwezo wa kuunga seli na seli akawa mtu, mwanadamu anaweza akamaliza ashiki yake kwa mbwa, kondoo au mbuzi ili mradi ajisifu kuwa na hilo ameweza.

Ukimwi umebuniwa na utundu wake, hivyo kamwe asijute. Huo ni mradi wake wa kupunguza idadi ya watu kama ambavyo mataifa mengine yamekuwa yakitoa zawadi kwa yeyote anayekubali kuharibiwa sehemu zake za uzazi ili kupunguza kasi ya uzazi kutoka mataifa hayo.

Sera za mke mmoja zimepotoshwa na huwa sheria kutoka mataifa mengi na hivyo kukiuka kanuni za maumbile, na mke kuzaa nje ya ndoa ni adhabu ya kifo. Hata hivyo madangulo katika dunia ya Magharibi ni biashara safi. Umalaya, watoto kutupwa mabarabarani ni mambo ya kawaida. Pengine idadi ya kutupa watoto ingepungua kama mme angepewa nafasi ya kuwa na mke zaidi ya mmoja. Tusione aibu kuwaambia watu, sasa wanawake ni wengi mno kuliko wanaume mara nne.

Wakati miye na marafiki zangu tulipokuwa tukidodosa somo letu (Anthropology) sayansi ya maisha ya mwanadamu. Na hasa kuwepo mme na mke. Mke anataka watoto, mme anataka watoto.

Hivyo basi, je, ni bora mke aoe mme? Je, ni vema mke kuoa mke mwenzie, halafu akamtafutie dume la kuajiriwa? Je, kwa kuogopa kuwa na watoto, basi mme aoe mme mwenzie.

Basi unapofikia hayo na zaidi, ndipo unatambua kuwa maisha ya mwanadamu yote yanahitaji sheria. Na sheria hizo zitii kanuni za maumbile

Na yuko mwanamke mmoja ambaye ana watoto watano lakini baba yao ni mmoja. Na baba yule ana wake wane na wote wana watoto wake.

Pia yuko baba mmoja alikataa kuoa kwa sababu zake.

Na yuko mama mmoja alikataa kuolewa kwa sababu zake.

Sasa wamezeeka na hawana wa kuwatunza, ni kosa la nani? Na kama baba na mama zao wasingewazaa wao waingepatikana wapi? Je, ni kati ya wale wasemao siku hizi afadhali ningekuwa mbwa wa Marekani ningekula vizuri? Ona jinsi mwandamu alivyo na kufuru. Chagua na upime kati ya hayo.

Pengine watu watauliza, kwa nini huyu bwana kaamua kuongea juu ya haya. Jibu ni kwamba, hakuna mwanadamu ambaye hakuzaliwa na mwanamke. Tuache tabia za kujifanya ati hatuelewi.

Wanawake wao ni bustani ya kanuni za maumbile, na wanaume ni walinzi na vazi la heshima kwao. Mtake mstake ndivyo ilivyo.

Basi kwa kuwa mwanadamu amekataa KUTUBU, mwanadamu amejifanya mjanja, mwerevu na mweza wa kusahihisha na kubadili kanuni za maumbile.

Haya yanayojitokeza anatakiwa kuyapokea na kuyafurahia kwa sababu ni matokeo ya kazi yake. Panda mti ukikata mti ili kusitokee jangwa, mwanadamu hataki kufanya hivyo, matokeo yake, jangwa linajitokeza.

Usiendeshe gari ukiwa umelewa, mwanadamu anasema wanampotezea muda. Matokeo yake, linaua watu.

Wanawake wacheni kuiga mambo yasiyofaa kama vile madawa ya kujichubua. Matokeo yake mtu anakuwa na sura kama kinyago. Waheshimuni waume zenu kwa sababu nyie ndiyo wenye mzigo wa kulea familia. Oh! Alikwenda ngomani au kwa shangazi, kumbe yuko kwa hawala yake!

Pelekeni watoto shuleni wasome, watu hawana habari, matokeo yake anaambiwa ati dawa hii ni nzuri, ukimbaka mtoto wa miezi kumi unapata mali!

Jamani, Mwenyezi Mungu, ni mmoja, wanasema hata, mbona hata marehemu babu yangu hunisaidia.

Usiitambie zinaa, hapana, ukiwa na shamba unapashwa kuwa na bustani karibu.

Jamani, usiuwe ila kwa haki. Hata lazima mimi ni muuwe yule bibi kizee kisa alionekana siku ile tuliopasua kuku. Jamani twendeni kusali. Tazama huyu naye, tangu tusalii, tumekwisha pata nini?

Tumieni kodi ya wakulima kwa ajili ya maendeleo yao. Huyu naye, unajuaje kama mwaka ujao watakuchagua. Kalia hayo hayo wenzio wanapiga hatua.

Bange na vidonge vya kulevya, vinaharibu ubongo. Watu wanasema hakuna biashara safi kama hiyo duniani, nyepesi kutajirisha. Matokeo yake, leo hii, waokota makopo na watoto taahira wanaongezeka.

Haya ndiyo maendeleo ya mwanadamu, asiye na mwongozo.
 

Juu

YALIYOMO



TAHARIRI

Milipuko ya mabomu Dar, Nairobi: Waislamu walaani vyombo vya habari
Na Mwandishi wetu

Wanawake Waislamu Tanga waazimia kupigania haki
Na Ibn Masoud, Tanga

Marekani yashambulia Sudan, Afghanistan

Maoni: Kulipuliwa kwa Ubalozi wa Marekani:
Huu ni unazi au sehemu ya mtandao?

Nguruwe kuzua tafrani Kibamba
Na Mwandishi Wetu

Sheikh Mbukuzi ataka vijana wajihadhari  na utamaduni wa Magharibi
Na Said Shariff

TAMPRO kuzindua Tawi Iringa
Na Mwandishi Wetu

Tamasha la kusaidia wagonjwa laanza Moro
Rajab Rajab na Mussa Ally, Morogoro

Kambi ya matibabu ya Macho Tanga yaanza
Na Mwandishi Wetu

MAONI: Kanisa mshiriki wa ukandamizaji

Porojo za Ngatara
Na J. Hussein

Ubatizo kupitia TVZ?
Na Salahuddin Ahmad

Waislamu Kosovo waangamizwa

MAPENDEKEZO YA KATIBA YA 
SHIRIKISHO LA TANZANIA -2

Hoja binafsi: Uhusiano na Marekani usituletee maafa
Na Said Rajab

Darasa la Muhammad (s.a.w)

Wanamume toeni haki  za wanawake kuepusha ufisadi
Na Halima Issa Ndabi,  Mwanza

MAKALA: Hoja za kutofautisha Yesu na Issa ni udhaifu,  ni uzushi mtupu! - 2
Na Muhibu Said

Mwanaadamu alipofikia
Na Nineka B.N., Geita

Mafunzo ya Quran

Barua za wasomaji

Mashairi

Masomo ya dini ya Kiislam

Chakula na Lishe

Matangazo
 

 

 Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:
Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtanzania.org

Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita