|
Na.163 Rabiul Thani 1419, Agosti 21 - 27, 1998 |
|
Watu wengi wahofiwa kujeruhiwa, kufa
Ndege za kijeshi za Marekani zimeshambulia Sudani na Afghanistan jana (Alhamisi) saa tatu usiku wa kwa majira ya Afrika mashariki. Kwa mujibu wa matangazo ya CNN, mashambulizi hayo ya yamefanywa kufuatia tuhuma kwamba nchi hizo zinahusika na milipuko ya mabomu kwenye balozi za Marekani katika miji ya Nairobi na Dar es salaam. Ikulu ya Marekani imesema kuwa mashambulizi hayo yamefanywa ili kutoa kile ilichodai kuwa ni onyo kwa mataifa yanayojihusisha na Ugaidi. Msemaji wa Ikulu hiyo ameeleza kwamba mashambulizi hayo yaliidhinishwa na Rais Bill Clinton saa chache kabla ya kufanyika na kwamba yalielekezwa katika maeneo yaliyolengwa. Akitoa sababu za kushambulia Sudan na Afghanistan, Rais Bill Clinton amedai kwamba ana ushahidi wa kutosha kuhusika kwa mataifa hayo na mipango ya kigaidi, kwamba yalishawahi kufanya ugaidi, kwamba yanajiandaa kufanya mashambulizi mengine ya kigaidi katika balozi za Marekani na kwamba yanamiliki silaha za Sumu. Nchini Sudani ndege hizo za mashambulizi zilikiangushia mabomu kiwanda cha madawa kusini mwa jiji la Khartoum. Aidha nchini Afghanistan mabomu yaliangushwa katika vituo sita vinavyodaiwa kuwa kambi za "magaidi" hao. Alipohojiwa mashambulizi hayo yamefanyika kutokea wapi, msemaji wa Ikulu ya Mareakni alijibu kwa mkato kwamba yamefanywa na majeshi ya Marekani. Kwa upande wake, Waziri wa Mambo ya ndani wa Sudan, ameyaeleza mashambulizi hayo kuwa ni maendelezo ya hujuma zinazofanywa na Marekani dhidi ya nchi yake na kuwa yamefanywa katika kiwanda cha madawa ya binadamu ( Shifer Parmaceutical plant) kinachomilikiwa na watu binafsi kilichopo Kartoum. Msemaji mmoja wa Afghanistan Bw. Noordullah Zadran alipohojiwa jana usiku na vyombo vya habari alisema kwamba, kwanza hakuna ushahidi wa kumhusisha Bwana Usama bin Laden na milipuko ya hivi karibuni na pili hawatosalimu amri kwa yoyote. Wakati huo huo, Seneta wa Jimbo la Indiana nchini Marekani bwana Dancoats, ameshutumu mashambulizi yaliyofanywa na nchi yake katika nchi za Sudan na Afghanistan. Kwa mujibu wa taarifa za CNN, Seneta huyo amesema kwamba licha ya shambulio hilo kutokidhi haja inayokusudiwa, Rais Bill Clinton hana mamlaka ya kuidhinisha jambo zito kama hilo kutokana na kashfa inayomkabili hivi sasa. Aidha ameshangazwa na uamuzi wa nchi yake wakati uchunguzi wa kuwasaka watuhumiwa bado haujakamilika. Aidha Seneta huyo ameongeza kusema kwamba mashambulizi hayo huenda yakawaweka Wamarekani katika wakati mgumu wa kuchukiwa na dunia nzima. Seneta huyo amemtaka Rais Bill Clinton ajiuzulu mara moja kwa hatua yake hiyo ambayo ameieleza kuwa haikuwa na ridhaa ya Wananchi wa nchi hiyo. mashambulizi mengine ya kigaidi katika balozi za Marekani na kwamba yanamiliki silaha za sumu. Nchini Sudani ndege hizo za mashambulizi zilikiangushia mabomu kiwanda cha madawa kusini mwa jiji la Khartoum. Aidha nchini Afghanistan mabomu yaliangushwa katika vituo sita vinavyodaiwa kuwa kambi za "magaidi" hao. Alipohojiwa mashambulizi hayo yamefanyika kutokea wapi, msemaji wa Ikulu ya Mareakni alijibu kwa mkato kwamba yamefanywa na majeshi ya Marekani. Kwa upande wake, Waziri wa Mambo ya ndani wa Sudan, ameyaeleza mashambulizi hayo kuwa ni maendelezo ya hujuma zinazofanywa na Marekani dhidi ya nchi yake na kuwa yamefanywa katika kiwanda cha madawa ya binadamu ( Shifer Parmaceutical plant) kinachomilikiwa na watu binafsi kilichopo Kartoum. Msemaji mmoja wa Afghanistan Bw. Noordullah Zadran alipohojiwa jana usiku na vyombo vya habari alisema kwamba, kwanza hakuna ushahidi wa kumhusisha Bwana Usama bin Laden na milipuko ya hivi karibuni na pili hawatosalimu amri kwa yoyote. Wakati huo huo, Seneta wa Jimbo la Indiana nchini Marekani bwana Dancoats, ameshutumu mashambulizi yaliyofanywa na nchi yake katika nchi za Sudan na Afghanistan. Kwa mujibu wa taarifa za CNN, Seneta huyo amesema kwamba licha ya shambulio hilo kutokidhi haja inayokusudiwa, Rais Bill Clinton hana mamlaka ya kuidhinisha jambo zito kama hilo kutokana na kashfa inayomkabili hivi sasa. Aidha ameshangazwa na uamuzi wa nchi yake wakati uchunguzi wa kuwasaka watuhumiwa bado haujakamilika. Aidha Seneta huyo ameongeza kusema kwamba mashambulizi hayo huenda yakawaweka Wamarekani katika wakati mgumu wa kuchukiwa na dunia nzima. Seneta huyo amemtaka Rais Bill Clinton ajiuzulu mara
moja kwa hatua yake hiyo ambayo ameieleza kuwa haikuwa na ridhaa ya Wananchi
wa nchi hiyo.
|
Milipuko ya mabomu Dar, Nairobi: Waislamu
walaani vyombo vya habari
Wanawake Waislamu Tanga waazimia kupigania
haki
Marekani yashambulia Sudan, Afghanistan Maoni: Kulipuliwa kwa Ubalozi wa Marekani:
Nguruwe kuzua tafrani Kibamba
Sheikh Mbukuzi ataka vijana
wajihadhari na utamaduni wa Magharibi
TAMPRO kuzindua Tawi Iringa
Tamasha la kusaidia wagonjwa
laanza Moro
Kambi ya matibabu ya Macho Tanga
yaanza
MAONI: Kanisa mshiriki wa ukandamizaji Porojo za Ngatara
Ubatizo kupitia TVZ?
MAPENDEKEZO YA KATIBA YA
Hoja binafsi: Uhusiano na Marekani
usituletee maafa
Wanamume toeni haki za
wanawake kuepusha ufisadi
MAKALA: Hoja za kutofautisha Yesu
na Issa ni udhaifu, ni uzushi mtupu! - 2
Mwanaadamu alipofikia
|
Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:
Bonyeza hapa
Au
Andika barua kwa: webmaster@islamtanzania.org