|
Na.163 Rabiul Thani 1419, Agosti 21 - 27, 1998 |
|
DARASA alilohudhuria Abi Hureira anatuambia, Mtume (saw) alifundisha katika darasa hilo kwamba, "watu aina saba Mwenyezi Mungu atawafunika kwa kivuli chake, siku ambayo hakutakuwa na kivuli isipokuwa kivuli chake: Wa kwanza ni kiongozi mwadilifu, wa pili ni kijana aliyekulia kumcha Mwenyezi Mungu Mtukufu, wa tatu ni mtu aliyeshikamana na Msikiti, wa nne wawili wanaopendana kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na wakatengana kwa ajili yake, wa tano ni mwanaume aliyeitwa au mwanamke mwenye hadhi na uzuri kufanya mambo machafu na akasema, "hakika mimi ninamwogopa Mwenyezi Mungu Mtukufu, wa sita ni mtu anayetoa sadaka kwa mkono wa kulia na mkono wa kushoto usijuwe kinachotolewa na mkono wa kushoto, wa saba ni mtu anayemtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu akiwa peke yake akalia kwa ajili ya kumwogopa Allah (sw). Hiyo siku ya hofu kuu, siku ambayo vijana wadogo wataota mvi, siku ya malipo ambayo mtu siku hiyo atamkimbia mamaye, kakaye, babaye, mkewe, rafikiye na mwanaye ili kuokoa nafsi yake tu. Siku hiyo udugu au ujamaa hautasaidia. Siku hiyo litateremshwa jua na joto lake halisi kwenye mahakama ya Allah (sw) Mtukufu. Litawekwa karibu sana na viumbe wanaosubiri hukumu ya Allah (sw). Lo! Ni siku ngumu iliyoje. Siku moja ni sawa na miaka hamsini elfu. Macho ya viumbe yatanyenyekea kwa woga. Ni siku hii ngumu Allah (sw) atakapowasamehe na kuwakirimu kwa rehema zake walioteuliwa katika waja wake. Nao ni hao waliotajwa katika darasa la Mtume (saw) hapo juu. Atawaepusha na khofu, msongamano, joto kali na kiu. Hao watakuwa katika kivuli cha Arshi yake iliyo katika himaya ya Rehema zake. Watu hao wanastahili rehema hiyo kutokana na juhudi zao hapa duniani. Ili na sisi tuwe pamoja na wenye kusamehewa na kukirimiwa na Allah (sw) tunapaswa kujihesabu kabla ya kuhesabiwa. Mizani ya kujihesabu ni hii ifuatayo: Kila anayepata uongozi wa kuwaongoza wenzake anapaswa kuwatendea haki, usawa, uadilifu, na kuepukana na tamaa za kidunia. Uongozi wake uambatane na sheria za Allah (sw) Mtukufu. Vijana walelewe kumpwekesha, kumpenda, kumwogopa kwa yakini Allah (sw) na waambatanishe imani hiyo na matendo mema. Matendo ambayo ni pamoja na kupambana na matamanio ya ujana na mapenzi ya starehe za dunia zisizodumu muda mrefu. Kisha wawe ni wenye kujiepusha na michezo ya upuuzi (laghawi). Wakatumia muda wao wote kusukuma gurudumu la kusimamia haki katika jamii. Wakajiepusha na yote yale yanayomghadhibisha Allah (sw). Mtu mwenye mapenzi makubwa na Allah (sw) ambaye lau Mwenyezi Mungu angalimwamrisha kujichinja angejichinja huku akiwa amefurahia kutekeleza amri hiyo iliyotoka kwa Mola wake, Bwana wake, Mfalme wake mtakatifu. Adhana ikipigwa kuita watu kwa sala yeye anakuwa wa kwanza kufunga shughuli zake zote kuwahi msikitini kusali sala ya jamaa. Watu wanaopendana kwa ajili ya Allah (sw). Wanapendana kwa msingi wa mapenzi yao ya kumpenda Allah (sw) na dini yake, tabia njema wema na utii kwa Allah (sw) na Mtume wake (saw). Wanatenganishwa na tamaa za dunia na ubinafsi. Mwanaume Rijaali mwenye nguvu aliyeshinda tamaa za matamanio yake akakataa kuingia katika mtego wa mwanamke fasiki anayejipisha pitisha mitaani kutamanisha wanaume kutokana na uzuri, hadhi na mali yake. Akaacha kumkurubia mwanamke huyo kwa kumwogopa Allah (sw) pake yake. Mtu anayetumia utajiri wake katika njia ya Allah (sw). Akatoa sadaka na zaka kwa wanaohusika bila ya riya (kujionyesha kwa wanadamu kwakuwataka wamtukuze, waonekanae maarufu n.k.. Mtu aliyekaa peke yake machozi yakamtoka kwa ajili
ya kutafakari malipo ya wema na wabaya siku hiyo ya malipo. Na akwa hajuwi
atakavyoishi. Akatafakari ni jinsi gani atakavyoweza kupambana ili kusimamisha
dini ya Allah (sw) katika ardhi.
Wanamume toeni haki za wanawake kuepusha ufisadi Na Halima Issa Ndabi, Mwanza NAPENDA kumuunga mkoni Bi Zuhra Tajiri kwa makala yake iliyotoka katika gazeti letu tukufu AN-NUUR ambayo itasaidia kuwa changamoto kubwa kwa wale waliokuwa ma mawazo finyu ya kijima. Kwanza napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwake kwa kuonyesha ujasiri wa hali ya juu ambao watuwezesha nasi kuwa na moyo kama huo. Iwapo tutayaunga mkono maneno yake kwa kuyageuzia katika vitendo basi hautatokea ufisadi katika Ardhi hii wala ndani ya umma wa Kiislamu. Kwa hakika karibu asilimia 99.9 ya wanaume hudhani kuwa mwanamke kujichagulia mchumba ambaye atakuwa ni mshirika wake katika maisha ya ndoa basi wao huona ni tadhlil na husema wazi na kuwaona wafanyao hivi ni wakosa. Tumeshuhudia baadhi ya wazazi wakiwalazimisha wana wao wakike kuolewa na wale wasio wataka kwa kisingizio kuwa mtoto wa kike haulizwi katika suala hili. Huu kwa kweli ni udhalilishaji wa haki za mwanamke wa hali ya juu sana. Ikitokea binti kampenda kijana wa kiume na kulitamka hilo wazi huonekana amekosa haya na aibu. Je? Ninyi wanaume mnafahamu maana ya haya au aibu?! Na bila kufikiria kuwa mwanamke au msichana ana haki ya kujichagulia mchumba, kama inavyothibitisha historia (ameshasema bi Zuhra) Mambo haya yametokea toka karne 14 zilizopita hakuna asiyeyajua. Je? Sio hawa wanaume wanaojiita wa kisasa wamekosa haya kuyakataa hata yale aliyoyafanya Mtume (s.a.w.). Tunatakiwa wanawake zama hizi tufahamiane na Bi. Zuhra aliposema. "Asione vibaya mwanamke kumuanza mwanaume" maana yake si kwenda wewe binafsi, au moja kwa moja, utatakiwa kuwa makini na kutumia njia za kimantiq. Lakini dada zangu kwa upande mwingine hivi sasa sidhani kama tutawapata wanaume wakakuelewa na kukubaliana na wito huu. Imeshawatokezea vijana wengi wenye heshima zao na elimu (kwa maana ya elimu). Walionekana kwamba watawafaa mabinti ambao nao walikuwa ni wenye elimu kama wao na tabia na mitazamo ikawa ni yenye kulingana basi mabinti hao wakatumia njia mbalimbali za kuwabainishia kuwa ‘sisi ndio tuwafaao’ kama alivyosema Allah katika Surat Nnoor aya No.26. na bila shaka waliwafahamu vizuri tabia zao. Lakini kitu cha kushangaza ni kuwa pamoja na kwamba mabinti walitaka haki zao kwa hao vijana na vivyo hivyo vijana hao kwa mabinti hao na pamoja na kufahamu malengo ya mabinti hao ni wema wa kiume watawapata wema wa kike (Qur’an) na kuwa muungano huo ungefanikiwa kukijenga kizazi chao na kuwa chema kwa uwezo wa Allah (s.w.) na kuiongoza jamii ijayo kwa kauli ya Allah. Kwa kweli ingawa vijana hao walionyesha taathiri nzuri lakini matokeo yalionekana kama wanawake hawa wamejidhalilisha, maana yake sio mwanamke apelekae posa na hivyo hili ni igizo la kibaniani "walidai". Je? ni wapi unapoelekea ummah huu ambao mojawapo ya sifa zake ni kuja kumkomboa mwanamke. Pamoja na kuikomboa dunia kutoka katika ujinga, mmojawapo ukiwa huu wa kumdhalilisha mwanamke. Watu hawa wamejifanya kusahau bi Khadija (r.a.) alifanya nini kwa Mtume (s.a.w.)!! Wamesahau alichofunya Umar (r.a.) alichofanya kwa binti yake!! Wamesahau na wakasahau!!....Eee ninyi makaka wa kisasa mnaridhika mabinti hawa wakazini? Je, mmeisahau fitra? (maumbile) (rejea Islamic psychology). Na Sheikh. Feisal Abdullah. Uk.). Jaribuni kufikiria ummah huu ulivyojaa watoto wa nje ya ndoa, je na hawa mabinti mngependa waongeze?!...Hasha lilah Mwenyezi Mungu awaepushe na hayo bali ni juu yenu vijana kuwapa haki zao na lazima mfahamu enyi Waislamu wa kiume siku hizi wanawake asilimia 80 wako katika mwongozo (mfumo kinamama Mwanza) hivyo hawatoridhika na mwanaume aliye kinyume cha sheria ya Allah. Hatujali mali ya familia. Mmesahau Rasul (s.a.w) amesema kwenye hija ya wadaa. "Nakuusieni kwa wanawake kheri". Kwani kheri ni kuwapa urithi tu?! au kuwapa haki zao kisheria? Kumbukeni kasema wanawake na sio wake hivyo hamana pa kukwepea. Kaka zetu mnatakiwa kuwafikiana na fikra zetu, kwa sababu ninyi ndio nguzo zetu; kumbukeni kuwa sisi tumetoka katika mbavu zenu. Kumbukeni kuwa ninyi mnachukua urithi mara mbili (2) kwetu. Nanyi ndio wasimamizi wetu.(Qur-an) Je.tutaishi hivi hadi lini?!...a je mnaridhika tuongeze haram juu ya haram?!! Tunanaomba Eee ninyi vijana mziwahi haraka nafsi hizo bila kupoteza muda. Hakuna haja ya nyinyi au sisi kuwekana vimada na akina Esta au Joni na vizazi vinatoka humo vibovu. La haviko duniani wala Akhera. Tunataka haki zetu kwenu kabla hamjaulizwa na Allah. Uwapi? Usimamizi uliokabidhiwa na Allah? Ya wapi mavazi aliyosema Mtume (s.a.w.)? Tunahitahji mavazi kwani Mtume kasema: "Mwanamke ana stara mbili mume na kaburi." Tunataka stara zetu?!’ Ianzishwe kamati ya nusra.
NUSRA!
Hakuna kipingamizi chochote katika Uislamu kwa msichana au mwanamke kumtamkia mwanaume aliyempenda kwa kuzingatia sifa alizozitaja Mtume (s.a.w.) kwamba angependa aolewe naye. Ukiwaacha wachache waliojitosa kwa ajili ya Allah (s.w.)kufanya hivyo, wasichana au wanawake wengi wamekuwa na haya nzito kutekeleza sunna hii. Wengi hao hubakia mabubu wenye umiyo la moyo na mwisho kuangukia katika "ili mradi kuolewa". Kwa kuzingatia kwa makini hali hiyo na suala zima la ndoa, AN-NUUR imeanzisha kitengo cha NUSRA ambacho pamoja na kuwatangaza wanaume wanaotafuta wake wema, pia kitatoa fursa ya aina yake kwa wasichana au wanawake ambao baada ya kuwatafiti wenza watarajiwa kwa vigezo vile vilivyotajwa na Mtume (.s.a.w.), wangependa watamke kuolewa nao kupitia kitengo hiki. Muhimu Madada hao wajitahidi kupata anuani za vijana hao na za kwao binafsi kisha waziwasilishe Kitengo hiki kitajitahidi kwa siri kuwasiliana na vijana hao bila ya kutanguliza kutaja jina la mhusika aliyependekeza. Kabla ya kuunganisha pande hizo mbili kitengo kinaahidi kufanya utafiti wa kina kuhusu tabia ya mienendo ya wote wawili. Madada wa Kiislamu wacha-Mungu, hii ni fursa muhimu kuwapata wenza watokanao na ridhaa zenu - Insha Allah. Kwa hiyo kuweni huru kuliingia zoezi hili la ucha Mungu Tumuige Bibi Khadija (r.a) ili tupate wenza tuwapendao tujenge familia zenye mapenzi na maadili ya Kiislamu hatimaye kupata vizazi vitakavyousimamisha Uislamu wa kweli Insha Allah. Tunaahidi mbele ya Allah kuwa mawasiliano haya yatakuwa ya siri kabla ya jambo lenyewe kuwa - Insha Allah. Kitengo cha NUSRA, AN-NUUR
|
Milipuko ya mabomu Dar, Nairobi: Waislamu
walaani vyombo vya habari
Wanawake Waislamu Tanga waazimia kupigania
haki
Marekani yashambulia Sudan, Afghanistan Maoni: Kulipuliwa kwa Ubalozi wa Marekani:
Nguruwe kuzua tafrani Kibamba
Sheikh Mbukuzi ataka vijana
wajihadhari na utamaduni wa Magharibi
TAMPRO kuzindua Tawi Iringa
Tamasha la kusaidia wagonjwa
laanza Moro
Kambi ya matibabu ya Macho Tanga
yaanza
MAONI: Kanisa mshiriki wa ukandamizaji Porojo za Ngatara
Ubatizo kupitia TVZ?
MAPENDEKEZO YA KATIBA YA
Hoja binafsi: Uhusiano na Marekani
usituletee maafa
Wanamume toeni haki za
wanawake kuepusha ufisadi
MAKALA: Hoja za kutofautisha Yesu
na Issa ni udhaifu, ni uzushi mtupu! - 2
Mwanaadamu alipofikia
|
Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:
Bonyeza hapa
Au
Andika barua kwa: webmaster@islamtanzania.org