AN-NUUR
Na.163 Rabiul Thani 1419, Agosti 21 - 27, 1998
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
Milipuko ya mabomu Dar, Nairobi:
  • Waislamu walaani vyombo vya habari
  • Ugaidi hauna dini - SUPKEM
  • Isiwe kuna agenda ya siri - Dk. Badawi
  • Mabomu ya Waislamu ni Qur’an - Sheikh Mwilima


Na Mwandishi Wetu

WAISLAMU wamevilaumu vyombo vya habari kwa kuihusisha dini yao na ulipuaji wa mabomu ya kigaidi mjini Nairobi.

Baraza Kuu la Waislamu Kenya (SUPKEM) limesema kwamba Waislamu hawakubaliani na vitendo vyovyote vya kinyama na hivyo hawawezi kuhusika kwa namna yoyote na ulipuaji wa mabomu.

Katika taarifa yake iliyosainiwa na Katibu Mkuu wake, Sheikh Ahmad Khalifa, SUPKEM limesema kwamba Uislamu kama dini nyingine yoyote haiwezi kuunga mkono mauaji ya watu wasio na hatia.

Na hivyo, akasema kwamba kuhusisha Uislamu na tukio hilo kulikofanywa na vyombo vya habari ni kuupaka Uislamu matope. 

SUPKEM imeongeza kusema kwamba ugaidi ni sumu hatari na uovu kwa dunia nzima ambao hauwezi kuhusishwa na dini yoyote.

Taarifa ya SUPKEM imesisitiza kwamba ni jambo la kusikitisha kwamba hata kabla ya uchunguzi kukamilika zimekuwepo juhudi za baadhi ya vyombo vya habari kuonyesha kwamba wa kulaumiwa katika vitendo hivi vya ugaidi ni Waislamu.

Imevitaka vyombo vya habari viwaache wachunguzi wafanye kazi yao kwa sheria, kanuni na taratibu zao.

Wakati huo huo, Waislamu sehemu mbali mbali duniani, wamekuwa wakielezea wasi wasi wao kufuatia shutuma zinazotolewa kupitia vyombo vya habari kwamba waliohusika na milipuko ya Dar na Nairobi ni Waislamu au makundi ya kiislamu yanayodaiwa kuwa na msimamo mkali.

Akionyesha kushangazwa na shutuma hizo, Msomi maarufu duniani Dk. Jamal Badawi, amehoji ni kwa vipi Waislamu watajwe kuhusika na milipuko hiyo wakati uchunguzi bado haujakamilika.

Dk. Badawi amesema kwamba kuwahusisha Waislamu na matukio hayo kwa haraka kiasi hicho kunaweza kudhaniwa kwamba huo ulikuwa ni mpango uliopangwa muda mrefu wa kutafuta visingizio ili kuwadhuru.

Dk. Badawi aliyasema hayo wakati akihojiwa na shirika la utangazaji la Uingereza BBC, havi karibuni.

Mwanachuoni huyo wa kiislamu wa masuala ya Utawala, amesema kwamba inawezekana kuhusishwa huko kwa Waislamu kunatokana na uadui mkubwa uliopo kati ya Marekani na baadhi ya nchi na makundi ya Waislamu. Hata hivyo Dk. Badawi amesema kuwa kuwatuhumu na kuwaandama Waislamu kiasi hicho huenda kukawa na ajenda ya hatari.

Dk. Badawi amefafanua kwamba kama itakuwa ni uadui, Marekani ina maadui sehemu mbali mbali duniani ikiwa ni pamoja na Ukanda Mzima wa Maziwa Makuu barani Afrika.

Aidha, Dk. Badawi ameelezea kuchukizwa kwake na jinsi vyombo vya habari vinavyowaripoti Waislamu kwa kuwahusisha na mambo mabaya ulimwengu mzima.

Naye Sheikh Abubakar Mwilima akihojiwa na Michael Sikawa wa BBC juu ya tuhuma za kuhusika kwa Waislamu, alisema kwamba mabomu ya Waislamu ni Qur’an na kwamba Uislamu ni dini ya amani na salama.

Nchini Afghanistan ambako inadaiwa kuwa ndiko alikojificha "mfadhili" wa makundi ya kiislamu yenye msimamo mkali, Wanaharakati wa nchi hiyo wameripotiwa kutoa tamko la kukanusha uzushi unaoenezwa dhidi yao.

Wanaharakati hao wametoa onyo la kuwa tayari kupambana na yeyote yule atakayejaribu kuvamia nchi hiyo kijeshi.

Wamemtaja Usama bin Laden kwamba hahusiki na milipuko iliyotokea Dar na Nairobi na kwamba hawako tayari kumkabidhi kwa Marekani na wameahidi kumlinda hata kwa kumwaga damu yao.

Juu

YALIYOMO



TAHARIRI

Milipuko ya mabomu Dar, Nairobi: Waislamu walaani vyombo vya habari
Na Mwandishi wetu

Wanawake Waislamu Tanga waazimia kupigania haki
Na Ibn Masoud, Tanga

Marekani yashambulia Sudan, Afghanistan

Maoni: Kulipuliwa kwa Ubalozi wa Marekani:
Huu ni unazi au sehemu ya mtandao?

Nguruwe kuzua tafrani Kibamba
Na Mwandishi Wetu

Sheikh Mbukuzi ataka vijana wajihadhari  na utamaduni wa Magharibi
Na Said Shariff

TAMPRO kuzindua Tawi Iringa
Na Mwandishi Wetu

Tamasha la kusaidia wagonjwa laanza Moro
Rajab Rajab na Mussa Ally, Morogoro

Kambi ya matibabu ya Macho Tanga yaanza
Na Mwandishi Wetu

MAONI: Kanisa mshiriki wa ukandamizaji

Porojo za Ngatara
Na J. Hussein

Ubatizo kupitia TVZ?
Na Salahuddin Ahmad

Waislamu Kosovo waangamizwa

MAPENDEKEZO YA KATIBA YA 
SHIRIKISHO LA TANZANIA -2

Hoja binafsi: Uhusiano na Marekani usituletee maafa
Na Said Rajab

Darasa la Muhammad (s.a.w)

Wanamume toeni haki  za wanawake kuepusha ufisadi
Na Halima Issa Ndabi,  Mwanza

MAKALA: Hoja za kutofautisha Yesu na Issa ni udhaifu,  ni uzushi mtupu! - 2
Na Muhibu Said

Mwanaadamu alipofikia
Na Nineka B.N., Geita

Mafunzo ya Quran

Barua za wasomaji

Mashairi

Masomo ya dini ya Kiislam

Chakula na Lishe

Matangazo

 

 Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:
Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtanzania.org

Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita