|
Na.163 Rabiul Thani 1419, Agosti 21 - 27, 1998 |
|
Na Mwandishi Wetu UUZAJI wa nyama ya nguruwe huenda ukazua mtafaruku miongoni mwa wakazi wa Kata ya Kibamba Jijini Dar es Salaam, ANU-NUUR imedokezwa. Kwa mujibu wa taarifa zilizofikishwa katika gazeti hili, mfanyabiashara mmoja ambaye anadaiwa kuuza nyama hiyo, amekuwa kero kwa baadhi ya wakazi wa eneo hilo. Kutokana na tabia yake ya kupuuza malalamiko yaliyokwishafikishwa kuhusiana na uuzaji huo wa nyama ya nguruwe. Mfanyabiashara huyo ambaye imeelezwa hajali kanuni za afya wala mahusiano na wengine, huuza nyama hiyo dukani kwa kutumia mizani ambayo pia huitumia kwa kupimia bidhaa nyingine. Katibu wa Waislamu wa Kata hiyo Bwana A. Mfinanga, amewaomba wahusika walishughulikie mapema suala hilo kwa kuchukua hatua zifaazo ili kuepusha mgongano unaoashiria kujitokeza baina ya Waislamu na mwenye biashara hiyo. "Tunaowaomba wale wanaohusika kufanya jitihada za makusudi kabisa kukomesha kero hii kwa Waislamu wa maeneo haya", amesema katibu hiyo. Imedaiwa kuwa biashara hiyo inafanyika bila ya leseni ya Jiji na minofu ya nyama hiyo huning’inizwa juu ya bidhaa kama unga, mchele na nyinginezo. Suala la ufugaji na uuzaji holela wa nyama ya nguruwe limekuwa likipigiwa kelele na Waislamu sehemu mbali mbali nchini. Licha ya kuwepo sheria inayokataza uuzaji au ufugaji
wa nguruwe katika maeneo mchanganyiko, malalamiko ya Waislamu yamekuwa
yakiambulia patupu au wao kuchukuliwa hatua kufuatia kulalamika huko, kama
ilivyojitokeza mwaka 1993.
Sheikh Mbukuzi ataka vijana wajihadhari na utamaduni wa Magharibi
Na Said Shariff IMAM Masjid Mujahiduun na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo Mburahati Barafu (CBO), Sheikh Juma Salim Mbukuzi amewataka vijana wajihadhari na utamaduni unaopingana na maadili mema unaoingizwa nchini ukiwa na nembo ya maendeleo. Amesema vijana hawana budi kufahamu kwamba ulevi wa aina yoyote, uzinifu, mavazi yasiyositiri mwili na mengineyo, hayo sio maendeleo bali ni maovu yanayopelekea katika maangamizi ingawa serikali inahalalisha na kutumia vyombo vya habari kutangaza na kueneza maovu hayo. Sheikh Mbukuzi amesema vijana wajihadhari sana na wimbi hilo la maovu linalopewa nembo ya maendeleo. "Kusema kweli, haya yanayodhaniwa ni maendeleo si maendeleo bali ni maovu yanayoingizwa nchini kutoka nchi za Magharibi na Serikali inasaidia kuimarisha maovu hayo kwa kuyajengea mazingira mazuri", amesema Sheikh huyo. Aidha ameongeza kusema kuwa mwanaadamu ana roho na mwili, vyote viwili vinahitaji maendeleo. Maendeleo ya roho ni maadili mema katika jamii, sasa vyombo vya habari kutumika kikamilifu kutangaza na kueneza maovu kwa gharama nyingi hiyo ni hatua ya kupiga vita maadili mema katika jamii. Kutokana na hali hiyo Sheikh Mbukuzi amesema hata hayo maendeleo ya Sayansi na Teknolojia yatakuwa hayana maana yoyote muda ambao maadili mema katika jamii yanapigwa vita kiasi hicho. Aidha Sheikh Mbukuzi amesema wazazi wana jukumu la
kuwaongoza vijana wao katika mwelekeo sahihi wa maisha ili kujinusuru na
naqama ya Mwenyezi Mungu pale watakapoulizwa, "mliziongoza vipi familia
zenu."
Na Mwandishi Wetu JUMUIYA ya Wanataaluma wa Kiislamu nchini (TAMPRO) yenye makao yake makuu Jijini Dar es Salaam, itazindua Tawi lake Mkoani Iringa siku ya Jumapili Agosti 23, 1998. Akitoa taarifa ya uzinduzi huo, Katibu wa Jumuiya hiyo Bwana Musa Mziya amesema kwamba shughuli hiyo ya uzinduzi itatafanyika katika Ukumbi wa VETA. Aidha Bwana Mziya amesema kuwa ratiba ya shughuli hiyo itahusisha pamoja na mambo mengine, uwasilishaji wa mada mbali mbali zitakazo lenga kuwahamasisha Waislamu hususan wanataaluma kujihusisha kikamilifu katika harakati za maendeleo ya Uislamu. Siku ya Jumamosi ameongeza Bwana Mziya, wawakilishi
wa TAMPRO Makao Makuu watazungumza na wanafunzi Waislamu wa shule za sekondari
na vyuo katika ukumbi wa shule ya sekondari ya Mkwawa.
Wajitolea chakula, dawa na damu Rajab Rajab na Mussa Ally, Morogoro WAISLAMU mjini Morogoro wameanzisha tamasha la kuwafariji na kuwasaidia wagonja, wafungwa na wasiojiweza mara mbili kwa mwezi. Akizungumza na AN-NUUR katika hospitali kuu ya mkoa mapema wiki hii, mratibu mkuu wa tamasha hilo, Daruwesh Kazimoto alisema kwamba nia yao ni kuitafsiri Qur’an katika matendo. Kwa kuanzia, alisema Daruwesh huyo kuwa wameamua kwenda pamoja hospitalini hapo ili kutoa athari za kisaikolojia kwa wagonjwa na jamii iliyowazunguka, ambapo pamoja na mambo mengine walitoa misaada ya chakula na dawa kwa wagonjwa 230 waliolazwa hospitalini hapo, kuwaombea duwa na kusafisha mazingira kama sehemu ya tiba kwa wagonjwa hao. "Aidha, tumeazimia kutoa dawa zenye thamani ya shilingi 39,350 kwa wagonjwa 28 wasio na ndugu wa kuwasaidia. Kwa leo tumetoa dawa kwa wagonjwa 15 na damu chupa tatu", alisema Mratibu huyo. Kiongozi mwingine wa tamasha hilo, Ustadh Ligaya
Shaaban alisema kuwa utaratibu huo utakuwa ni wa kudumu na utaenezwa katika
maeneo
Na Mwandishi Wetu, TangaWAKAZI wa Manispaa ya tanga na miji ya jirani wenye matatizo mbalimbali ya macho wanatazamiwa kupatiwa matibabu ya bure yatakayotolewa na wataalamu wa kutoka Kenya, Uingereza na wa hapa nchini. Hayo yameelezwa na kiongozi Mkuu wa Jumuiya ya Ansar Muslim Youth Tanga, Sheikh Salim Abdulrahim katika taarifa yake aliyoifikishia gazeti hili mapema wiki iliyopita. Tawfiq Muslim Youth ya Kenya, Muslim Aid ya Uingereza wakishirikiana na Ansar-Tanga ambao ndio wenyeji na waratibu wa kambi hiyo inayotarajiwa kuanza Agosti 20 hadi 30 1998, watatoa huduma ya upimaji wa macho na matibabu ikiwa ni pamoja na kutoa dawa, miwani na upasuaji kwa wale itakaolazimu. Wenye matatizo ya macho kiasi cha 200 hadi 350 watafaidika na huduma hiyo ya bure ambayo kwa hapa nchini itakuwa ni ya aina yake kutokana na hali ya wale watakaolazimika kufanyiwa upasuaji kutohitajia kuvaa miwani baada ya upasuaji kukamilika. Taarifa imeendelea kusema kuwa ili kufikia ufanisi. kiasi cha shilingi milioni tatu zimetengwa kuikarabati zahanati ya Manispaa (Makorora Dispensary) ambayo ndiyo itakuwa kambi kuu ya upasuaji. Wito umetolewa kwa wale ambao wanatoka nje ya Wilaya ya Tanga kuwasiliana na uongozi wa Ansar Muslim Youth ili kupata uhakika wa kufanyiwa matibabu. Mawasiliano yafanywe kwa simu namba 46620 au Fax 47074.
|
Milipuko ya mabomu Dar, Nairobi: Waislamu
walaani vyombo vya habari
Wanawake Waislamu Tanga waazimia kupigania
haki
Marekani yashambulia Sudan, Afghanistan Maoni: Kulipuliwa kwa Ubalozi wa Marekani:
Nguruwe kuzua tafrani Kibamba
Sheikh Mbukuzi ataka vijana
wajihadhari na utamaduni wa Magharibi
TAMPRO kuzindua Tawi Iringa
Tamasha la kusaidia wagonjwa
laanza Moro
Kambi ya matibabu ya Macho Tanga
yaanza
MAONI: Kanisa mshiriki wa ukandamizaji Porojo za Ngatara
Ubatizo kupitia TVZ?
MAPENDEKEZO YA KATIBA YA
Hoja binafsi: Uhusiano na Marekani
usituletee maafa
Wanamume toeni haki za
wanawake kuepusha ufisadi
MAKALA: Hoja za kutofautisha Yesu
na Issa ni udhaifu, ni uzushi mtupu! - 2
Mwanaadamu alipofikia
|
Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:
Bonyeza hapa
Au
Andika barua kwa: webmaster@islamtanzania.org