|
Na. 067 Jumatano Septemba 27 - Oktoba 2, 2000 |
|
|
|
|
|
LIGI KUU TANZANIA 2000:
WAKATI Ligi Kuu ya Muungano Tanzania inaanza leo, kuna uwezekano kwa timu za Yanga na Kajumulo kushindwa kuwatumia wachezaji wapya katika ligi hiyo baada ya kushindwa kuwasilisha majina ya wachezaji hao FAT kwa wakati. Majina hayo yalitakiwa yawe yamewasilishwa juzi jioni katika ofisi za Chama cha Soka nchini (FAT) kitu ambacho hakikufanyika. Kwa mujibu wa kaimu Katibu Mkuu wa FAT, Amin Bakhroon ni timu ya Mtibwa pekee ndiyo iliyowasilisha majina ya wanandinga wake. Amewataja wachezaji hao kuwa ni Patrick Betwel, Charles Wilson Chacha, Hussein Hamis Swedi na Aldina Hashim Swedi ambao hata hivyo hawajaidhinishwa rasmi na FAT. Kulingana na kanuni zinazoongoza michuano hiyo, timu zinaruhusiwa kuongeza wachezaji wasiozidi watano ili kuongeza nguvu kwa timu zao, ligi hiyo pia inazishirikisha timu za Kipanga, Polisi na Mafunzo za Zanzibar. Awali, Yanga ilitarajiwa kuwaongeza Waziri Mahadhi, Fred Mbuna, Aziz Hunter, Abdulqadir Tash na Chibi Chibinda. Nayo Kajumulo ilipanga kuwatumia Gwakisa Mwandambo, Mengi Matunda, William Fahnbuller, Peter Nkwera na Edward Kayoza. Kufuatia hali hiyo, Mwenyekiti wa FAT, Kanali Idd Kipingu ameongeza muda mpaka leo mchana Kajumulo na Yanga kuwasilisha majina ya wachezaji hao. Ameongeza kwamba wachezaji hao hawataruhusiwa kuvichezea vilabu hivyo endapo timu hizo zitashindwa kufuata maelekezo. Katika michezo ya fungua dimba leo Mtibwa itamenyana na Kajumulo (Morogoro), Yanga na Mafunzo (Dar) na Kipanga itakwaana na Polisi huko Zanzibar.
Na Mwandishi Wetu CHAMA cha soka ya Kinondoni (KIFA) ambacho Iddi Azzani ni Mwenyekiti wake kimelaumiwa kwa kudharau mualiko wa timu ya Msoka F.C yenye masikani wilayani humo. Kwa mujibu wa Juma Digama Madenge, KIFA kilitakiwa kutuma muwakilishi katika sherehe za kukabidhi kombe Jumapili iliyopita katika mashindano yaliyoandaliwa na Msako F.C ya Kigogo jijini. "Licha ya kuthibitisha kwamba wangetuma mwakilishi lakini hawakufanya hivyo kitu ambacho kimetusikitisha sana", amesema Madenge ambaye ni Mwenyekiti wa Msako F.C Mkuu wa wilaya kinondoni Hawa Ngulume alikuwa mgeni rasmi ambaye alikabidhi kombe kwa timu ya Boca Junior ya Kigogo iliyoishinda Baruti ya Magomeni kwa penati 5-4 Katika mashindano hayo bingwa ilizawadiwa jezi
14, mshindi wa pili alipata katoni moja ya sabuni ya taifa na mpira,wakati
Fadhili Ally ambaye alikuwa mfungaji bora wa mashindano hayo alipewa jezi
Na Mwandishi Wetu CHAMA cha Makocha nchini (TAFCA) kimepinga madai kwamba makocha Abdallah 'King' Kibadeni na Sunday Kayuni hawafai kufundisha timu ya Taifa, Taifa Stars. Akizungumza mjini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa chama hicho Idd Omar Machuppa amesema, makocha hao wana kila sifa zinazowafanya wastahili kuifundisha timu hiyo. "Kibadeni na Kayuni ni makocha wazuri na sina wasiwasi nao hata kidogo juu ya uwezo wao", amesema Machuppa. Juzi Katibu Mkuu wa Kajumulo World Soccer, Juma Simba alisema, Kibadeni na Kayuni hawafai kufundisha timu ya Taifa kwa kuwa uwezo wao ni mdogo. "Mimi naamini kama makocha hawa (Kibadeni na Kayuni) watapata vitendea kazi madhubuti basi timu lazima itafanye vizuri", ameongeza. Amevitaja vitendea kazi hivyo kuwa ni vifaa vya mazoezi, posho nzuri kwa wachezaji na makocha na muda wa kutosha wa kambi. Lakini akaonya kama vitu hivyo havitapakana kulingana na mahitaji basi kuna uwezekano mkubwa wa Taifa Stars kufanya vibaya. Taifa Stars inakabiliwa na mashindano ya Global yatakayozishirikisha nchi nne ambazo ni Kenya, Uganda, Ghana na Tanzania yenyewe yatakayofanyika hivi karibuni nchini Kenya. Kadhalika, Kibadeni na Kayuni walioteuliwa na FAT hivi karibuni watakuwa na kibarua cha kuiandaa Kilimanjaro Stars kwa ajili ya michuano ya kombe la Chalenji itakayofanyika nchini Uganda Novemba mwaka huu. Aidha, Machuppa amewataka watu wasio na taaluma ya ukocha kukoma kabisa kuzungumzia juu ya ubora wa makocha wazalendo nchini akiwemo Kibadeni na Kayuni.
Hamis Kasabe na Said Mwenda MSHAMBULIAJI wa Kimataifa wa Simba na timu ya Taifa , Taifa Stars, Said Maulid 'SMG' amekanusha habari kwamba amesajiliwa na timu pinzani na Simba, Yanga kwa ajili ya msimu ujao wa ligi. Amesema, hajawahi hata kuzungumza na kiongozi yeyote wa Yanga kuhusu suala hilo zaidi ya yeye kusoma tu kwenye magazeti. "Kwa kweli suala hilo hata mimi nimelisoma tu magazetini lakini sijawahi kuzungumza lolote na watu wa Yanga kuhusu usajili", amedai Maulid katika mazungumzo na NASAHA jana jijini. "Kwanza hata hivyo suala lenyewe haliwezekani kwa sababu tayari vilabu hivi (Simba na Yanga) vina mkataba wa kutokuchuliana wachezaji", ameongeza. Naye mshambuliaji tegemeo wa timu ya Ashanti ya Ilala, Yasin Abuheri Hussein (23) ametajwa kuwa ni miongoni mwa wachezaji wanaowindwa na Coastal Union ya Tanga. Habari hizi zimethibitishwa na Hussein mwenyewe
ambaye hata hivyo hakutaka kuingia kwa undani kwa madai kuwa suala hilo
liko mikononi mwa kocha Nzoyisaba Tauzany wa Coastal Union ya Tanga.
|
YALIYOMO
TAHARIRI
Wapinzani kumuimarisha Prof. Lipumba Ngangari kung’olewa Sokoni, Ilala Polisi nchini hawajui mipaka ya kazi yao -OAU MAKALA
HABARI
ATV yatakiwa kuzingatia maadili Wakazi wa Tabata walalamikia athari ya maji machafu Maalim Seif akanusha madai ya kumwaga damu USHAURI NASAHA
MAKALA
MIPASHO NASAHA
KALAMU YA MWANDISHI
MAKALA
MWENYE MACHO…
MAKALA
LISHE
|
|
|
|
|