|
Na. 067 Jumatano Septemba 27 - Oktoba 2, 2000 |
|
|
|
|
|
Kimfaacho mtoto Mariam Mbwambo Kwa mara nyingine tena, wapendwa wasomaji tunawaletea mfululizo wa makala za lishe. Leo tutaangalia uboreshaji wa afya ya mtoto. Mtoto anahitaji uangalifu wa hali ya juu ili kumwezesha kukua vizuri. Mtoto huyu atahitaji virutubisho muhimu kama proteni, wanga (starch),vitamin, maji yaliyo safi na salama, madini mbalimbali, kwa ajili ya kuimarisha mifupa yake na meno. Pia kumwepusha na magonjwa yasababishwayo na ukosefu wa madini hayo kama goita (tezi la shingo) n.k. Hivyo, mtoto kama kiumbe mwingine ana vipimo maalum. Katika kukamilisha mahitaji hayo, maziwa ya mama ni muhimu sana tangu mtoto anapozaliwa hadi anapofikia umri wa miezi minne hadi atakapohitajia vyakula vya ziada ambavyo vitatayarishwa katika hali ya usafi na utaalam wa hali ya juu. Maziwa ya mama ni chakula tosha cha mtoto awapo mdogo kwa sababu yamekamilika katika virutubisho vyote muhimu vihitajikavyo mwilini. Kutoka umri wa miezi 4-6 maziwa peke yake humtosheleza mtoto. Maziwa ni muhimu kwa mtoto kwani huzidisha upendo kati ya mama na mtoto. Hayana vimelea vya magonjwa, humuepusha mtoto na magonjwa kama kuhara, na mengine mengi, humuongezea uzito na afya nzuri. Iwapo akaanza kupatiwa maziwa ya chupa kutokana na kufa kwa mama yake, chupa hizo lazima visafishwe vizuri kwa maji ya mtoto na vikaushwe vizuri. Vyombo vya mtoto visichanganywe na vya watu wazima. Ili visipate shombo, ikasababisha maziwa kuchacha au harufu mbaya katika chakula cha mtoto. Unashauriwa kuzingatia muda wa kulisha mtoto wako kila baada ya masaa 3 au 4. Ama kwa masaa 3, saa 12 asubuhi, saa 3 asubuhi, saa sita mchana, saa tisa na saaa 12 jioni. Mlo wake kwa ujumla waweza kuwa uji, wali bokoboko (ubwabwa) na mchuzi usio na chumvi wala ndimu nyingi, supu ya nyanya. Juisi ya matunda na maziwa, bila kusahau maji. Baada ya kuacha maziwa ya mama lazima apewe vyakula vya kujenga na kulinda mwili zaidi ili kujenga mwili wake na kumwepusha na utapiamlo au P.E.M. (protein energy malnutrition). Vyakula hivyo vyaweza kuwa juisi ya machungwa, papai, mboga mboga kama nyanya za kusaga, karoti, juisi, mchicha n.k. Mayai, hasa kiini cha yai kilichopikwa na maziwa. Kwa watoto wanaoanza kutembea, wapewe vyakula vya kuvutia kwani huwa wabishi kula. Hivyo lazima wabadilishiwe vyakula ili kuwapa hamu ya kula vyakula hivyo. Wakati huu maziwa yanahitajika kwa wingi, mayai, samaki wa kuchemsha, nyama ya kusaga,viazi vya kusaga, ndizi, uji. Supu ya mbogamboga na matunda aina mbalimbali. Vyakula kama dagaa, maharage, supu ya maharage apewe kwa wingi zaidi. Vyakula vya sukari nyingi, vya kukaanga, samaki ambao itawawia vigumu kutafunwa wasipewe pamoja na pastries wasipewe. Hivyo basi tunashauriwa kufuata maelekezo na mawaidha
mazuri kutoka kwa wataalm wa lishe ili kuweza kuwapatia lishe bora, watoto
ambao ni taifa la kesho.
|
YALIYOMO
TAHARIRI
Wapinzani kumuimarisha Prof. Lipumba Ngangari kung’olewa Sokoni, Ilala Polisi nchini hawajui mipaka ya kazi yao -OAU MAKALA
HABARI
ATV yatakiwa kuzingatia maadili Wakazi wa Tabata walalamikia athari ya maji machafu Maalim Seif akanusha madai ya kumwaga damu USHAURI NASAHA
MAKALA
MIPASHO NASAHA
KALAMU YA MWANDISHI
MAKALA
MWENYE MACHO…
MAKALA
LISHE
|
|
|
|
|