|
Na. 067 Jumatano Septemba 27 - Oktoba 2, 2000 |
|
|
|
|
|
CCM haitakiwi, sasa yakimbilia Polisi Ndugu Mhariri, Nimesikilishwa sana na jinsi ambavyo Chama cha Mapinduzi na serikali yake wanavyokazana kuupinda ukweli wa mambo. Viongozi wa CUF wamekuwa wakitangaza kwamba safari hii hawatakubali wapokonywe ushindi wao. Wakigundua kuwa wameshindwa kwa kuibiwa kura zao, hawatakaa kimya mpaka haki yao waipate. Lakini wamesema wakishindwa kihalali watakubali matokeo na watampongeza mshindi na chama chake. Cha ajabu CCM inazusha mambo ya uongo mtupu. Eti CUF wakishindwa watamwaga damu. Eti CUF inatoa kauli za vitisho kuwafanya wananchi wasijitokeza kupiga kura. Hebu ndugu zangu tazameni kichekesho hiki cha chama tawala: Kama CUF inawatisha wananchi wasijitokeze kupiga kura siku ya29/10/2000, sasa itawezaje kushinda uchaguzi ili iongoze nchi? Mbona CCM inakwepa kusema lolote juu ya hofu ya wapinzani kuibiwa kura zao? Kamati kuu ya CCM imefanya kikao chake na kukimbilia kuagiza Polisi iwashughulikie CUF badala ya kuiagiza Tume ya Uchaguzi isimamie uchaguzi kwa uwazi zaidi ili kuondoa hofu ya vyama vya upinzani kwamba kura zao zinaibiwa. Watanzania tujiulize: ikiwa kweli CCM hawana mpango kuiba kura za wapinzani kwa nini walikataa kuunda Tume ya Uchaguzi inayovishirikisha vyama vya upinzani? Watanzania msitetereke. CCM sasa maji yapo shingoni, hivyo kutapatapa kwao si ajabu. Sasa hivi CCM kila mtu anaongea kivyake. Katibu Mkuu wao, Bw. Philipo Mangula, alisema, taarifa ya Kamati Kuu ya CCM na kusema CUF inaigopa CCM kwa vile CCM inazidi kuimarika na kukubalika. Lakini Mwenyekiti wao, Rais Benjamin Mkapa anasema ndani ya chama chao kuna makundi ya upinzani ambayo yanatishia kuisambaratisha CCM kwa ilivyotokea kwa NCCR. Na wananchi wa huko Tabora wamempa RaisMkapa "laivu' kwamba hawataipigia kura CCM, badala yake watampa kura zao zote mgombea wa CUF Prof. Ibrahim Lipumba. Wakainua juu picha ya Prof. Lipumba (soma gazeti Mtanzania la 25/9/2000. Sasa kama CCM inazidi kuimarika, hayo makundi aliyayasema Mkapa yametoka wapi? Na kama CCM inakubalika inazidi kukubalika, huko Tabora wamemwambia nini Mkapa? Ninatamani Oktoba 29, ifike haraka, Mkapa kumpisha Profesa Lipumba Ikulu. Damian Magare,
Ndugu Mhariri, Naomba nafasi katika gazeti lako ili nitoe dukuduku langu kwa Wakurugenzi wa vyombo vya habari vya umma. Kwanza napenda kuwapongeza kwa kazi zao nzuri za kulihudumia taifa letu katika sekta ya habari. Kiini chabarua hii ni vipindi viwili vinacyorushwa navyombo hgivi yaani "Zama za Uwazi (TVT) pamoja na "maneno hayo" (Redio Tanzania). Katika wakati huu tunapoelekea katika uchaguzi, vyombo vya habari vina nafasi kubwa sana katika kushawishi watu juu ya ni serikali ya chama gani waikubali na kuikabidhi madaraka ya nchi. Kwa maoni yangu kwa vipindi hivyo viwili itakuwa ni jambo la busara kama vitasitishwa mara moja. Kwani kama itafuatiliwa kwa kina baadhi ya vipindi hivyo mathalani kipindi cha zama za uwazi kilichorushwa Jumapili ya tarehe tatu Septemba ni sawa kabisa na kampeni. Ni vizuri nikaeleweka kwamba, sisemi kama vyombo hivyo vya umma visitumike kwa kampeni, la hasha; bali vitumike kwa kutoa haki sawa kwa wagombea na vyama vyote vinavyoshiriki uchaguzi. Kwa kuviacha vipindi hivyo viendelee ni sawa na kukipa chama tawala nafasi zaidi katika vyombo vya umma kuliko vyama vingine. Ni lazima ikumbukwe kwamba vyombo hivyo vimeanzishwa na vinaendeshwa kwa kodi za Watanzania wote bila kujali wa chama gani. Hivyo jaribio lolote la vyombo hivyo vya umma la kukipa chama kimoja fursa zaidi ya kingine ni sawa na kumkamua kodi Mtanzania kisha kutumia kodi hiyo kuua msimamo na itikadi ya chama chake. Bi Z. Said,
Ndugu Mhariri, Ninaomba japo nafasi ya upenuni nieleze kilio changu kuhusu chama changu nikipendacho cha CCM. Kwa kweli imefikia mahali tunaona aibu kujitambulisha kuwa sisi ni CCM. Mwenyekiti wetu Mhe. Benjamin Mkapa alitutangazia kwamba Kamati Kuu ya CCM imetengua matokeo ya kura za maoni na kuwapiga marufuku baadhi ya wagombea wasigombee tena kwa sababu walihusika na vitendo vya rushwa na wengine ni wakwepa kodi. Lakini ajabu kabisa siku hizi Mhe. Mkapa akienda huko mikoani anawasifu watu walioenguliwa kwa tuhuma za kuleta mambo ya rushwa katika kura za maoni na tuhuma za kukwepa kodi kuawambia ni wana-CCM wazuri. Alipokwenda Morogoro alimsifu Aziz Abood, na alipokwenda Singida kusoma magazetini kwamba alimsifu Bw. Mdogo Mohamed Dewji. Lakini wote hawa walienguliwa, sasa leo uzuri wao unatoka wapi? Je wapinzani wataulewa vipi msimamo wa chama chetu? Hivi sasa hata mikutano yetu ya kampeni haipati wasikilizaji. Watu wametuchoka na pengine wanatudharau. Inawezekanaje wapinzani ambao hata hawajatimu umri wa miaka 10 katika siasa wapate wasikilizaji lukuki? Chama chetu kimekuwepo tangu uhuru lakini watu wanaohudhuria mikutano yetu ni wa kuokoteza. Hata hivyo kwa vile uchaguzi bado, hatujachelewa. Ninawaomba wakongwe wa siasa katika CCM, akina Mzee John Malecela, Mzee Kingunge na Mzee Ali Hassan Mwinyi wakutane na Mhe. Mkapa na Mhe.Mangula waangalie jinsi ya kukinusuru chama. Kidumu Chama Cha Mapinduzi,
Ndugu Mhariri, Naomba unipe fursa katika gazeti lako niweze kutoa nasaha zangu kwa mkuu wa Jeshi la Polisi nchini na viongozi wengine wa jeshi hilo. Kazi kubwa ya polisi ni kulinda usalama wa raia wote bila kujali rangi, dini, kabila au vyama vyao vya siasa. Tunategemea viongozi wa jeshi la polisi wazingatie wajibu huu wa makini hasa wakati huu wa kampeni na wakati wa uchaguzi. Matendo ya jeshila polisi katika baadhi ya maeneo huko Visiwani na hapa Bara yanaonesha kuwa polisi wamekuwa wakitumika kwa maslahi ya CCM. Kwa mfano polisi Dar waliwashambulia kwa mabomu wananchi waliokuwa wanaenda kwenye mkutano wa uzinduzi wa kampeni wa cuf wakati katika mkutano huo ccm Jangwani Polisi walikuwa wakitoa ulinzi na magari yaliyokuwa yanapita barabara ya Morogoro ili mkutano huo wa CCM uendelee bila bughudha. Mifano ya aina hii ni mingi. Bw. Mahita hivi ndivyo jeshi lako linatakiwa kufanya kazi yake? Majuzi KamatiKuu ya CCM imekutana na kuiagiza dola ikae chonjo na ijiandae kuwadhibiti wapinzani hasa chama cha wananchi (CUF). Napenda kumshauriBw. Mahita na viongozi wengine wa jeshi la polisi wawe makini wasijiingize katika mtego wa kutumiwa na chama chochote cha siasa. Hakuna jeshi lolote duniani linaloweza kuwazidi nguvu wananchi, ambao ndio wengi. Wako wananchi waliyoyashinda majeshi yenye nguvu navifaa vya kisasa, mfano majeshi ya Shah waIran. Sembuse askari wetu ambao wana hali duni kutokana na mishahara midogo na hawana vitendea kazi vya kutosha! Viongozi wa polisi pia wasisahau kuwa hao nambari wani watakaposhindwa vibarua vyao na hali zao zitakuwaje? Ikiwa wao hawatendi haki. Tumeshuhudia viongozi wa jeshi wa nchi nyingine wakishitakiwa kwa kunyanyasa raia baada ya viongozi wa kisiasa kutolewa madarakani. Utetezi kuwa tuliamrishwa na viongozi hautasaidia. Napenda kumshauri Bw. Mahita na jeshi la polisi kuwa liwe makini katika kutekeleza majukumu yake, lisipendelee chama chochote wala kuwatisha wananchi, kwani zama hizo zimepitwa na wakati. Abdallah Rashid,
Ndugu Mhariri, Naomba nafasi katika gazeti lako, ili niweze kuwahamasisha Watanzania wenzangu, kwa kuwakumbusha kwamba hiki ni kipindi cha kila chama kutangaza sera zake za maendeleo. Cha kushangaza ni kwamba badala ya kutangaza sera, CCM inaingia na gia ya kukusanya lundo la bendi za muziki kila katika mkutano wake wa kampeni. Hii inaonyesha ni jinsi gani, Chama Cha Mapinduzi kilivyofilisika kifikra. Wananchi tunajiuliza huku kukusanya mabendi ya muziki kutatusaidi nini sisi? Na kama gharama za kukusanya mabendi yote haya ya muziki, ni kutoka katika kodi zetu basi huo ni ufujaji wa hali ya juu kabisa wa pato la taifa. CCM hawana jipya, madai yao kwamba uchumi umekuwa, hamna lolote. Tukifikiri Mwenyekiti wa CCM atatueleza sababu ya kuuzwa kwa Benki ya NBC kwa bei poa, maana tunakumbuka kuwa mwaka 1995, aliahidi na kutilia mkazo kwamba Benki hiyo haitabinafsishwa. Ninapenda kutoa wito kwa vijana na wazee kwamba tuikomboe nchi hii Oktoba mwaka huu wa 2000 kabla haijauzwa yote. Kura zetu tuwape wapinzani walioungana CUF na CHADEMA. Wapinzani waliobaki akina Mrema na akina Cheyo si wa kuaminika, kwa kukataa muungano na wenzao, wameonyesha kuwa wanaipigia debe CCM, tuwaepuke. L. Jonas,
|
YALIYOMO
TAHARIRI
Wapinzani kumuimarisha Prof. Lipumba Ngangari kung’olewa Sokoni, Ilala Polisi nchini hawajui mipaka ya kazi yao -OAU MAKALA
HABARI
ATV yatakiwa kuzingatia maadili Wakazi wa Tabata walalamikia athari ya maji machafu Maalim Seif akanusha madai ya kumwaga damu USHAURI NASAHA
MAKALA
MIPASHO NASAHA
KALAMU YA MWANDISHI
MAKALA
MWENYE MACHO…
MAKALA
LISHE
|
|
|
|
|