|
Na. 067 Jumatano Septemba 27 - Oktoba 2, 2000 |
|
|
|
|
|
Maalim Seif akanusha madai ya kumwaga damu
Chama cha Wananchi (CUF) kimekanusha habari zinazoenezwa na CCM, kuwa CUF endapo itashindwa katika uchaguzi wa mwaka huu kitamwaga damu. Katibu Mkuu wa chama hicho Bwana Seif Sharif Hamadi, amesema chama chake hakijawahi kutoa kauli kama hiyo na kwamba maneno hayo ni uzushi mtupu unaoenezwa na CCM. Katibu Mkuu huyo ambaye pia ndiye mgombea Urais wa Zanzibar ameyasema hayo alipokuwa akihutubia wananchi wa Jimbo la Mlandege katika viwanja vya Lumumba. Bwana Hamadi amesema kila mara chama chake kimekuwa kikisisitiza kuwa endapo kitashindwa katika uchaguzi ulio halali basi kitaridhia matokeo kwa lengo la kuheshimu maamuzi ya wananchi walio wengi. Amesema anashangazwa na viongozi wa CCM ambao wamekuwa hawatamki hadharani kama watayakubali matokeo pindi chama chao kitashindwa. Amedai kukaa kimya kwa CCM bila kueleza msimamo wake ni dalili kuwa chama hicho hakina nia nzuri na ndio maana wamekuwa wakifanya hila ili kuvuruga uchaguzi kwa vile tayari CCM imeshapoteza matumaini ya kushinda. "Nawataka viongozi wa CCM , Mkapa, Dr. Omar na mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM Bwana Amani waseme ni wapi na lini chama chetu kimetamka kuwa endapo tutasindwa tutamwaga damu", amehoji Bw.Hamad Amesema mbali na kumwaga damu ya mtu hata ya inzi haitomwagika, lakini wakishinda kisha kudhulumiwa ushindi wao hawatakubali, alisisitiza Bw. Hamad. Aidha Bw. aliwaambia wananchi wa Jimbo la Mlandege kuwa endapo watamchagua kuwa rais wa Zanzibar atahakikisha anatatua kero zote zinazowakabili . Pia Bw.Hamad amewahidi wafanyabiashara wadogo
wadogo maarufu kama Jula Kali kuwa atawajengea vibanda vya kufanyia biashara
zao na kwamba tayari ameshajitokeza mfadhili atakayefanya hivyo na kinachosubiriwa
ni serikali ya CUF kuingia madarakani.
|
YALIYOMO
TAHARIRI
Wapinzani kumuimarisha Prof. Lipumba Ngangari kung’olewa Sokoni, Ilala Polisi nchini hawajui mipaka ya kazi yao -OAU MAKALA
HABARI
ATV yatakiwa kuzingatia maadili Wakazi wa Tabata walalamikia athari ya maji machafu Maalim Seif akanusha madai ya kumwaga damu USHAURI NASAHA
MAKALA
MIPASHO NASAHA
KALAMU YA MWANDISHI
MAKALA
MWENYE MACHO…
MAKALA
LISHE
|
|
|
|
|