|
Na. 067 Jumatano Septemba 27 - Oktoba 2, 2000 |
|
|
|
|
|
Wahutu, Watutsi acheni ukabila - Sheikh NAIROBI, Kenya. MAKUNDI yanayopigana nchini Burundi yametakiwa kuacha uhasama baina yao nabadala yake yajikite kukamilisha mwenendo wa amani. Hayo yamesemwa na Sheikh Mustafa Ramadhani ambaye ni Katibu wa Jumuiya Waislamu nchini Buruni katika mazungumzo ya amani mjini Nairobi wiki hii. Mkutano huo ulifanyika nchini Kenya ulikuwa ni muendelezo wa kuyapatanisha makundi yanayopigana nchini Burundi. Mkataba wa amani kati ya makundi hayo ulitiwa saini mwishoni mwa mwezi Agosti mwaka huu mjini Arusha Tanzania chini ya mpatanishi Rais Mstaafu wa Afrika ya Kusini Bwana Nelson Mandela. Huko Arusha makundi yapatayo 19 yalitia saini na kubaki mengine matano ambayo wiki hii huko Nairobi mengine yamejiunga. Ambayo bado yamepewa muda takribani mwezi mmoja kuja na msimamo wa mwisho. Sheikh Mustafa katika mahojiano na idhaa ya Kiswahili ya sauti ya Ujerumani amesema kuwa tatizo kubwa la Burundi ni ukabila. Ameyatolea mwito makabila ya Wahutu na Watutsi kuachamapigano hayo ya kikabila. Sheikh huyo aliongeza kuwa mnamo miaka ya tisini kulipotokea mapigano hayo jamii ya Kiislamu haikuathirika na mauaji hayo ya halaiki. "Hii ilitokana na makabila yote walio Waislamu kushikamana na mafundisho ya dini yetu ambayo yanapinga ukabila", alisema Sheikh Mustafa. Aliongeza, "Uislamu ndiyo tiba pekee dhidi ya ukabila na aina zote za ubaguzi." Alipotakiwa kueleza zaidi wajibu walionao viongozi wa dini katika mwenendo wa amani nchini humo alisema kuwa wao wataendelea kupiga kelele kwa wauaji waache kuua. Akizungumzia vikundi vinavyokataa kusaini Mkataba wa amani Sheikh amesema kuwa vinakwamisha utaratibu huo na hivyo kuongeza machungu zaidi kwa Warundi ambao licha ya kutumaini amani bado ni ndoto isiyotabirika. Juu ya makundi yaliyovunjwa, Katibu huyo amesema Waislamu na wale wa Imani zingine wamerejea makwao lakini mauaji bado yanaendelea na hivyo kufanya utekelezaji wa haki za binadamu kuwa mgumu. Nao Warundi waishio nje bado wana wasiwasi na kurejea makwao kutokana na hali hiyo, alisema kwa masikitiko Sheikh huyo. Warundi walio nchi Tanzania kwa mujibu wa Mkuu wa Wilaya ya Ngara wamekuwa wakitoroka makambini na kuelekea nchi jirani ya Uganda. Pamoja na kuendesha zoezi la kuwakamata ni wachache tu wanaokamatwa ambao mara nyingi ndio wanaokuwa na familia zao. Mkuu huyo wa wilaya amesema sababu zinazowapeleka Uganda kwanza ni kwaajili ya kupata usalama. Pili ni kutokana na uhaba wa chakula uliopo hapo Ngara na hususani makambini, kwani hutoka kutafuta vibarua kwaajili ya kuongeza riziki ndipo wengine hutoroka. Akitaja sabahu nyingine alisema kuwa vijana wafikapo Uganda hujiunga najeshi nafamilia zao hutunzwa vizuri. Alisema kiasi cha wakimbizi 60 hutoroka kwa wiki, na kuongeza kuwa ni vigumu kuwadhibiti. Hali ya chakula makambini si nzuri kutokana na shirika la kushughulikia wakimbizi (UNHCR) na lile la mpango wa chakula duniani (WFP) kutoa mgao usiotosheleza. Naye Bwana NelsonMandela anatarajiwa hivi karibuni kuzitembelea kambi za wakimbizi za Kigoma na Ngara nchini Tanzania.
MALUKU, Indonesia UISLAMU uliingia Maluku katika karne ya 13, baada ya Gapi Baguna (aliyetawala 1432-1465), Mtawala wa Kisiwa cha Ternate kuwaalika Waislamu kufanya makazi katika kisiwa chake. Baguna alivutiwa na mfumo (utaratibu) wa maisha ya Waislamu hao na akashawishika kujifunza zaidi kutoka kwao. Kuwasili kwa Waislamu kulifanya wakazi wa Ternate kufuata ustaarabu wa Kiislamu. Wengi wa Waislamu waliohamia huko walikuwa wafanyabiashara kutoka Ghuba yaUarabuni, Iran, Uchina, Java na Sumatra. Baada ya Baguna na Ikulu yake ya Ternate kurejea katika Uislamu ilitangazwa rasmi na kuanza rasmi shughuli ya kuwakumbusha raia kurudi katika dini yaasili, Uislamu, katika eneo lote la Maluku. Wimbi la Waislamu kuhamia huko kutoka katika mchi hizo kulisababisha mchanganyiko wa damu, na pia baada ya muda mfupi wakazi wote wa Maluku wakawa ni waumini wa Kiislamu. Vile vile tawala zilizokuwa jirani kusini na kusini mashariki, Sulawesi (Celebes)zilirejea katika Uislamu na punde kuwa mataifa yenye nguvu. Tawala hizo tatu (Sulawesi kusini, Sulewesi kusini mashariki na Maluku) zikaunda serikali ya shirikisho. Shrikisho hilo liliimarisha nguvu za kijamii na kisiasa katika eneo hilo, na watuwengi walivutiwa na kumiminika Maluku. Mnamo mwaka 1512 Wareno kutoka Ulaya, wakiongozwa na Antonio d’Abreu walifika katika moja ya visiwa vya Maluku. D’abreu akisaidiwa na mfanyabiashara wa Kimaleyi Ismail ambaye alikuwa chini ya Wareno hao au alitekwa walifika kisiwa cha Neira karibu na Lonthor. Wareno walikuta Maluku kuna utajiri wa karafuu jambo ambalo liliwafanya wasafiri hadi Goa, India kutoa taarifa juu ya biashara hiyo na hazina iliyopo Maluku. Alfonso d’Albuquerque mara moja aliandaa mashambulizi ya kijeshi kuvamia Maluku hatimaye kumiliki mtaji wa kisiwa hicho. Huo ukawa ndio mwanzo wa Ureno kuikalia Maluku kwa miaka 93 na ni mwanzo wa machafuko yanayoendelea hadi hivi sasa. Mashindano ya kumiliki biashara ya viungo visiwani humo miongoni mwa mataifa ya Kikoloni ya Ulaya, Upinzani kutoka kwa Waislamu wa Maluku, kusambaratika kwa utawala wao kulileta matokeao ya Ukristo kukua na kustawi katika himaya hiyo. Mnamo 1605 wakoloni wa Kijerumani waliibuka na kuwa na nguvukuu ya kumiliki Maluku. Tofauti kati ya Wajerumani na Wareno ilikuwa juu ya uendelezaji Ukristo. Wajerumani hawakutilia maanani suala la kusimamisha Ukristo, walilenga kupata faida ya biashara ya viungo zaidi na ndio maana waliweka sheria na kanuni ngumu katika biashara hiyo ili wamudu kumiliki wao tu. Pia waliwatumia wenyeji wa Maluku walioingia imani ya Kikristo kupigana na ndugu zao wa damu (Waislamu) walioonekana wapinzani dhidi ya Wajerumani. Na waliwatumia katika mapigano ya kupanua utawala wa Kijerumani maeneo mbalimbali. Wajerumani hawakuwaingiza katika Ukristo watu wengi wa Maluku.Zaidi waliimarisha tabaka kati ya Waislamu na Wakristo. Wareno lengo lao kuu ilikuwa kuwabatiza Waislamu na kuubomoa Uislamu hatimaye kuufuta huko Maluku. Hivyo walitumia kila mbinu na hila kuhakikisha Waislamu wengi wanakuwa Wakristo.
Mafia wa Algeria wajiandaa ALGIERS, Algeria KIKUNDI cha Mafia cha Algeria wako tayari kwa lolote ili kuendelea kushikilia biashara wanazofanya. Mara nyingi kikundi hicho hushambuliwa na vyombo vya habari na Rais Abdel Aziz Bouteflika, wanailinda sekta ya biashara ya uingizaji bidhaa, ambayo tayari wanamiliki kwa kiasi kikubwa. Kufuatia kuundwa kwa mfumo huru wa biashara baada ya kushindwa kwa mfumo wa Kisovieti(Ujamaa) uliotumika mara baada ya uhuru mwaka 1962 na kufikia hatima yake 1992, mabosi wa kikundi cha Mafia wamejitengenezea umiliki wa aina yake katika biashara za nje. Mafia ambao ni vigumu kuwamiliki lakini wenye nguvu nchini humo ambamo kwa muda mrefu kuna ghasia za kisiasa na mapigano wamegundua kuwa katika maendeleo ya viwanda, hasa vile vya kigeni kuna ‘uvamizi’ katika biashara ya uingizaji bidhaa ambayo wameiendesha kwa miaka mingi. Hivyo iwapo viwanda vya kigeni vitapeleka bidhaa zake kupiku biashara ya uagizaji bidhaa ya Mafia, basi huo utakuwa mwisho wa mabosi wa Mafia am ao wamejilimbikizia mali nyingi licha ya umaskini ambao umekithiri miongoni mwa wananchi wa Algeria hasa kipindi cha miaka kumi iliyopita. Hivi karibuni Mafia wanatuhumiwa kwa shambulio la bomu ambalo liliharibu ofisi moja ya makampuni machache ya serikali yanayopata faida. Kampuni hiyo ya utengenezaji vifaa vya umeme katika mji wa Tizi-Ouzou, ilioyopo kiasi cha kilomita 100 mashariki mwa mji huo, inadhaniwa kwamba kilish ambuliwa ili kuionesha serikali kwamba kuna mipaka ambayo Rais wa nchi hiyo alilaumu shambulio na kuilenga moja kwa moja Mafia ya Algeria baada ya baadhi ya watu kutoa lawama zao kwa vikundi vya Kiislamu. Shambulio hilo lilidhihirisha "Mgongano katiya wazalishaji (wa ndani) na waingizaji bidhaa katika soko la uchumi", Rais alisema. "Waingizaji bidhaa wanapoteza soko kwa kuwa uzalishaji sasa unafanywa ndani", aliongeza na kusema kuwa shambulio hilo ni "kitendo cha Mafia wa Algeria." Muda mfupi baada ya uchaguzi mwezi Aprili mwaka jana, Bouteflika alitangaza kwamba wazalishaji wa samani na vifaa vya umeme ambao wanataka kuwekeza Algeria wanashauriwa kwenda nchi za jirani za Tunisia na Morocco. Ushauri huo inadaiwa kuwa ulikusudia kuvunja umiliki
wa Mafia katika biashara ya uingizaji bidhaa ambayo ndiyo chanzo cha kipato
kizuri kwa mabosi hao wa Mafia..
|
YALIYOMO
TAHARIRI
Wapinzani kumuimarisha Prof. Lipumba Ngangari kung’olewa Sokoni, Ilala Polisi nchini hawajui mipaka ya kazi yao -OAU MAKALA
HABARI
ATV yatakiwa kuzingatia maadili Wakazi wa Tabata walalamikia athari ya maji machafu Maalim Seif akanusha madai ya kumwaga damu USHAURI NASAHA
MAKALA
MIPASHO NASAHA
KALAMU YA MWANDISHI
MAKALA
MWENYE MACHO…
MAKALA
LISHE
|
|
|
|
|