|
MASHAIRI
Wasomi tuikomboeni nchi
Ndugu zangu ninyi wasomi, wakatiumeshafika,
Tushirikini wasomi, chaguzi imeshafika,
Kwani ni sisi wasomi, ndio tunalalamika,
Oktoba 29, shime tukomboe nchi.
Tusiwache MAMBUMBUMBU,waje angamiza nchi,
Watu wasokumbu kumbu, ya hali mbaya kwa nchi,
Wamejaa mambumbu, kila pembe kwenye nchi,
Oktoba 29, shime tukomboe nchi.
Wasomi nawaamini, katika upambanuzi,
Wasomi mpo makini, kuchagua kiongozi,
Mtuhawadanganyeni, kwa sera za uchochezi,
Oktoba 29, shime ktukomboe nchi.
Mwaenda mikutanoni, kusikiza viongozi,
Hamukai majumbani, mwachambua viongozi,
Kisera naElimuni, mwampata mkombozi,
Oktoba 29, shime tukomboe nchi.
Kwa uongo wa udini, mtu hawadanyanyeni,
Waseme nambari, udini kwenu wahuni,
Nyinyi mwazama seani, kwa Lipumba kikomoni,
Oktoba 29, shimetukomboe nchi.
Wasomi nguvu ya hoja, mimininawaamini,
Wao kwa kauli moja, Lipumba yuko moyoni,
Uchumi ni yao hoja, haki sawa na amani,
Oktoba 29, shimetukomboe nchi.
Kenye nani ni zaidi, kwa maraisi wanne,
Lipumba bwanazaidi, umchambue uone,
Kusoma ndio zaidi, nani ashindane nae!
Oktoba 29, shimetukomboe nchi.
Nchi kukosa wasomi, ndio manayayumbishwa,
Wawapo wengi wasomi, hapa tusingefikishwa,
Tungeshiriki wasomi, wabaya kubatilishwa,
Oktoba 29,shimetukomboe nchi.
Betitiosa kama nati, sitaki kuenda fa,
Wazomi tujizatiti, nchi sipate maafa,
Tjemweka kwenyekiti, mwenye mengi maarifa,
Oktoba 29, shime tukomboe nchi.
Almasi H.Shemdoe
(Tunda la Matumaini”.
Ngangari na neno jino
Washangaza sisiemu, kutwa wanalalamika,
Hawaishi kulaumu, na maneno kutamka,
Mnyonge siwafahamu, nini wanachokitaka,
Ngangari na neno jino, udini wake ni nini.
Ngangari na neno jino, udini wake nataka,
Nami sitatia neno, kweli ikibainika,
Sio mwazusha maneno, kwa kutaka madaraka,
Ngangari na neno jino, udini wake ni nini.
Mimi ni Mtanzania, pia ni Muafrika,
Nina haki kuchagua, chama ninachokitaka,
Na sio kunipangia, kama wewe unavyotaka,
Ngangari na neno jino, udini wake ni nini.
Huku kwetu mitaani, wenyewe hatuna shaka,
Si kabila wala dini, vyungu vyetu vyapikika,
Unaposema udini, wapi unatupeleka,
Ngangari na neno jino uwapi udini wake.
Unaposema kidumu, kukalia madaraka,
Japo kuwacha dhulumu, na raia kuteseka,
Hapo waniisha hamu, nashindwa hata kucheka,
Niambie nifahamu, udini wa neno jino.
Babu yangu alisema, adidhi kunitambia,
Masikini mpe nyama, wenzeke kuwagawia,
Walahi hagawi nyama, mkononi itaozea,
Najua kweli ya uma, sasa mnatapatapa.
Mwisho nina malizia, jibu nataka haraka,
Kama mtapuuzia, mahakamani tapeleka,
Najua mwatuzulia, matope mnatupaka,
CUF ya waislamu, CCM dini gani?
(Nyonge wa haki),
UstadhiKassimJumaa (Mbaya),
S.L.P. 100054,Mbagala, Dar
Tutasaga meno
Chonde chonde jamachonde, ndugu zangu wananchi,
Chaguzi ni chonde chonde,muwe macho wananchi,
Naomba msivulunde, mtaja iua nchi,
Tukimkosa Lipumba, tutaja kusaga meno.
Nduguchagua Lipumba, mpole mpenda haki,
Dhiki sije tukumba, tukaja kufa malaki,
Balaa litatukumba, klwa ujinga ushabiki,
Tukimkosa Lipumba, tutaja kusaga meno.
Ndugu acheni mzaha, nyaka mitano ni mingi,
Tufanyeni ufasaha, na sababu za msingi,
Tujefurahia raha, tuchague kwa msingi,
Tukimkosa Lipumba, tutaj kusaga meno.
Mitano ndugu fundisho, myaka kumi jamamingi,
Tusisikize vitisho, sera zisizo msingi,
La Benjamini fikisho, jama tumekerwa wengi,
Tukimkosa Lipumba, tutajakusaga meno.
Tutaja kusaga meno, na kukonda ka vidingi,
Mkapa ni msumeno, mmeshuhudia wengi,
Puzeni yangu maneno, mtanikumbukawengi,
Tukimkosa Lipumba, tutajakusaga meno.
Sita beti wangu mwisho, nimefikakituoni,
Tusiogope vitisho, walo navyo majanuni,
Tusije kulia mwisho, naaga kwa huzuni,
Tukimkosa Lipumba, tutaja kusaga meno.
Almasi H.Shemdoe
(Tunda la Matumaini”..
Ukumbusho
Hodi tena Mhariri, mpangaji gazetini,
Leo ninalo shauri, niwajuze kilindini,
Niwakumbushe habari, uchaguzi u njiani,
Nawakumbusha raia.
Uchaguzi u njiani, kujiandikisha adhimu,
Watanzanianchini, hakikwetu ni muhimu,
Mijini na vijijini, siachie sehemu,
Nawakumbusha raia..
Msiachie sehemu, oneni hili mapema,
Siku hiyo ya muhimu, ikumbukeni nasema,
Watuchosha udhalimu, ndio mana twalalama,
Nawakumbusha vijana.
Jama fanyeni mapema, kituoni sije kana,
Ndugu zangu hima hima, watani wangu naguna,
Tuje tung’oe dhuluma, iwe usiku mchana,
Nawakumbusha raia..
Hata usiku mchana, mvua zaunguruma,
Jua kali likichoma, mtu siache simama,
Kupiga kura vijana, amana yake Karima.
Kisha nyuma msirudi, ikitimia chaguzi,
Yabidi kujitahidi, tutaondosha majonzi,
Ili sumu isizidi, sote tuwe na mapenzi,
Naikumbusha jamii.
Tujifute na machozi, tuseme tumekomboka,
Tufurahi nasi enzi, mashoka kutuondoka,
Nasi tupate ujuzi, watoto tumeteseka.
Mwisho ninakumbshia, kura muwahi mapema,
Kisha CUF kuchagua, hapa twakaliwa dhima,
Tusije tena ugua, Mwembechai huko nyuma,
Nawakumbusha raia..
Almasi Shemdoa, nimekumbushia uma,
Lipumba tuseme nae, Mtagaluka lazima,
Kijukuu situlie, CUF tuhuma kuzima,
Nawakushia raia.
Mtoto
(Mkimbiza mashairi),
Tanzania.
Tukimkosa Lipumba basi
Mzee Juma saidi, kikongwe jirani yangu,
Wallahi Joni shahidi, naapa haki ya Mungu,
Kasema mbele ya Iddi, mpendwa rafiki yangu,
Kwamba Lipu mkombozi,tumkosapo majuto.
Lipumba ni kiongozi,tumkosapo majuto,
Lipu peke mkombozi, mwanisikia watoto,
Lipu pendo la mwenyezi, kwa yote yetu mazito,
Lipu bwana kiongozi, tumkosapo majuto.
Tukimkosa Lipumba, Wallah kasema basi,
Ni kweli sio kuimba, tena bila wasiwasi,
Kidumu wataturimba, akatupa wasiwasi,
Kwamba Lipu mkombozi,tumkosapo majuto.
Wanachagua Lipumba, sisi sote katuasa,
Yeye wake ni Lipumba, mwingine hao ni sasa,
Kwa yote yalo mkumba,mkombozi Lipu sasa,
Lipu Bwana kiongozi,tumkasapo majuto.
Mimi na ukongwe wangu, Lipu nimemuamini,
Nitampa kura yangu, naahidi kwa manani,
Mimi na busara zangu, kwa Lipu nimesaini,
Kwamba Lipu mkombozi,tumkosapo majuto.
Mimi na ukongwe wangu, Lipu nimemkubali,
Namridhia wenzangu, ashinde kwa kila hali,
Alete heshima yangu, awezavyo kila hali,
Lipu Bwana kiongozi,tumkosapo majuto.
Kadi tamani mwishoni, kalamu naweka chini,
Mzee Juma jamani,hayo ni yake maoni,
Nanyi wengine igeni, Lipumba awe kitini,
Kwamba Lipu mkombozi,tumkosapo majuto.
Almasi H. Shemdoe,
“Tunda la Matumaini”,
Dar es Salaam.
Mke huyu hanifai
Kweli imedhihiri, kwa kila mwenye akili,
Mke ni yule mahiri, kwa mume aso jahili,
Sote sisi tumekiri, mke mwema muhimili,
Mke huyu ni mke gani, hata kulea hajui!!
Yahitaji kufikiri, kuweza tambua hili
Utajuta siyo siri, ukichagua fedhuli,
Yazidi hata shubiri, uchungu wake mithili,
Mke huyu ni mke gani, wakushabihi sioni.
Usijitie kiburi ukapumbazwa na mwili,
Zingatia na mahari, isije kuwa kufuli,
Usihisi ufahari, kuona wingi wa mali.
Mke mwema ni mtaji, wa lile jambo na hili.
Arubaini imejiri, nimetunza wake mwili,
Ameshindwa kusitiri, asili yangu na hali,
Zimekuwa ni fahari, kwa wale watu wa mbali,
Mke huyu hanifai, kumuacha ni halali.
Nimekuwa ni fakiri, chini kwa kila hali,
Siuoni utajiri, alonigea Jalali,
Ni kipi nakisubiri, ili niweze kubali?!!
Mkehuyu ni hatari, kuishi naye hafai.
Kupitia washauri, na mafundi wa Injili,
Mimi nikawa tayari kungoja zake fadhili,
Mitano nikasubiri huenda angebadili,
Mke huyu ni bandari, ya kila ovu na shari.
Katu hali siyo shwari, kama nitamkubali,
Watoto wangu wazuri, watajakuwa “makuli”,
Hawatojua witiri, na hata shufwa nambali,
Ah! Mke huyu siafiki, kuilea familia.
Kijani kajisitiri, na njano yake kwa mbali,
Kumbe ndani machachari, huwezi kumkabili,
Hapani natafakari, nimpate asiye mili,
Mke huyu hatakikani, ni kheri ya kisichana!!!
Mohammedi Khamisi, S.L.P. 374,
Tabora (Masomoni Tabora).
|
YALIYOMO
TAHARIRI
Polisi ‘isiibebe’ CCM
Wapinzani
kumuimarisha Prof. Lipumba
Ngangari
kung’olewa Sokoni, Ilala
Polisi
nchini hawajui mipaka ya kazi yao -OAU
MAKALA
BBC, CCM
ndugu au tajiri na kibaraka?
HABARI
‘Walioshindwa
kutawala wasikimbilie matusi’
ATV
yatakiwa kuzingatia maadili
Wakazi
wa Tabata walalamikia athari ya maji machafu
Maalim Seif
akanusha madai ya kumwaga damu
USHAURI NASAHA
‘Mama,
hela hii inanunua nini?'
MAKALA
Demokrasia
ni kukubaliana kutokukubaliana
MIPASHO NASAHA
HEBU VUENI
MIWANI ZENU!
KALAMU YA MWANDISHI
Juha haliambiliki!Juha
haliambiliki!
MAKALA
Amani
ya Tanzania itadumishwa na haki
MWENYE MACHO…
Hoja za
uongo katika kampeni
MAKALA
Chonde
Dk. Omari na Karume wahurumieni Wazanibari wenzenu
Habari
za Kimataifa
LISHE
Kimfaacho
mtoto
BARUA
MASHAIRI
MICHEZO
Yanga kuwakosa Mahadhi, Mbuna
Idd Azzan lawamani
Kibadeni, Kayuni wanafaa Stars
- Machuppa
Said Maulidi: Sihami Simba
|