|
Na. 041 Jumatano Machi 29 - Aprili 4, 2000 |
|
|
|
|
|
Sharia Nigeria zatekelezwa: mwizi akatwa mkono UAMUZI wa Waislamu kuongozwa na sheria za dini yao (Sharia) katika majimbo ya Kaskazini mwa Nigeria bado upo pale pale licha ya taarifa za serikali kuu ya nchi hiyo kutaka zisitishwe, kufuatia ghasia zilizozushwa na Wakristo wanaopinga kuwepo kwa sheria hizo. Kwa mujibu wa taarifa zilizotangazwa na vyombo mbalimbali vya habari ikiwemo BBC, zimeeleza kwambajimbo la Zamfara ambalo ndilo la kwanza kupitisha sheria za Kiislamu, hivi karibuni lilitekeleza adhabu ya kukatwa mkono mtu aliyepatikana na kosa lawizi. Habari hizo zilieleza kuwa mtu huyo aliyetajwa kwa jina moja la Njengembe alipewa adhabu hiyo baada ya kupatikana na kosa la kuiba ng'ombe. Kabla ya kutekelezwa kwa adhabu, alipewa muda wa siku 30 kukata rufaa. Siku ya adhabu, mwizi huyo alipewa fursa ya kutoa ombi lolote. Aliomba uji wa ngano na maziwa. Baada ya kunywa uji wake, alipigwa sindano ya ganzi kisha akakatwa mkono.
Maaskofu wazuia somo la Kiislamu
Jakarta, INDONESIA. Baraza la Maaskofu wa Katoliki nchini Indonesia wameikataa sheria ya serikali ya kuingiza mitaala ya somo la maarifa ya Uislamu katika shule mbalimbali nchini humo. Katika kusisitiza dai lao hilo wamesema kuwa si haki kwa serikali kuingiza mitaala hiyo ijapokuwa kuna zaidi ya asilimia 40 ya wanafunzi wa Kiislamu wanaosoma katika shule zinazomilikiwa na Wakatoliki. Serikali ya Indonesia imeweka sheria kuhakikisha kuwa somo la maarifa ya Uislamu linafundishwa katika mashule kuanzia shule za awali hadi vyuo vikuu. Imeelezwa kuwa lengo la kufundisha elimu ya maarifa ya Kiislamu ni kuwafanya wasomaji waufahamu Uislamu, wautekeleze kivitendo katika maisha yao na kuwaandaa kufanya mitihani ya taifa. Wakristo wa madhehebu ya Kiprotestanti nao waumeunga mkono msimamo huo wa madhehebu ya kikaktoliki. Katika taarifa yao wameeleza kuwa huo ni unyanyasaji wa kiimani kuingiza mitaala ya somo hilo. Kihistoria madhehebu ya Wakristo wa Kiprotestanti ni Wapinzani wa misimamo na mitazamo ya madhehebu ya Wakristo Wakatoliki. Mwaka jana nchini Indonesia kulitokea mapigano kati ya Waislamu na Wakristo katika miji ya Maluku na Tokajawa. Katika mapigano hayo watu 11 walifariki na wengine 24 kujeruhiwa katika mji wa Maluku, ambapo katika mji wa Kotajawa watu watano waliuawa na kumi walijeruhiwa. Miji kadhaa ilikumbwa na kadhaia hiyo hali iliyopelekea watu zaidi ya 700 kuuawa. Nchi hiyo iliyowahi kutawaliwa na Wadachi ina idadi kubwa ya Waislamu
kuliko dini nyingine zilizomo nchini humo.
Sakata la Wakristo kujichoma moto Uganda:
MAITI wengine wa waumini wa Kikristo wanaodaiwa kuwa awali walikuwa wa dhehebu la Roman Catholic, wamegunduliwa katika maeneo mbali mbali nje ya kanisa la Kanungu ambamo awali walikutwa zaidi ya maiti 400 waliodhaniwa kuwa walijifungia humo na kujichoma moto. Maiti hao wengine wapatao 153 waligunduliwa katika mashimo wakiwa na alama ya kunyongwa, kuchinjwa na kupigwa mapanga. Miongoni mwa maiti hao, zaidi ya 60 walikuwa ni watoto wadogo. Katika kufuatilia uchugunzi wa sakata ya mauaji, polisi wa Uganda waligundua maiti wengine 70 wakiwa katika shimo moja katika eneo la Rugavi, Wilaya ya Bushenyi, ambako walienda kumtafuta kiongozi wa kanisa hilo, Kasisi Dominic Ntaribaho. Kiongozi huyo ambaye zamani alikuwa wa kanisa Katoliki, hakupatikana. Inadhaniwa ni miongoni mwa waliokufa. Hata hivyo viongozi wengine wa Kanisa hilo Joseph Kabwetere na mwanamke aitwae Credonia Mwelinda inadhaniwa wapo hai na wanatafutwa. Habari zaidi kuhusu Kanisa hilo liitwalo Movement for the Restoration
of Ten Commandments, zinadai kuwa waumini wa kanisa hilo wapo karibuni
katika nchi zote za maziwa makuu na idadi yao ni kubwa.
Polisi kufikishwa kizimbani kwa kuwapiga risasi wandamanaji
Kaduna, NIGERIA. Polisi katika jimbo la Kaduna nchini Nigeria watawafikisha katika mahakama yakipolisi askari kadhaa kutokana na kukiuka taratibu za jeshi hilo kwa kuwapiga risasi na kuwaua waandamanaji wanne. Msemaji wa Polisi toka jimbo la Kaduna amenukuliwa akisema kuwa ilikuwa sio sahihi kwa askari polisi kuwapiga risasi waandamanaji badala ya kutumia njia nyingine kuwatwawanga waandamanaji hao. Aliendelea kwa kusema kuwa kwa kitendohicho askari wahusika ni lazima wafikishwe kwenye sheria. Habari zaidi zimesema kuwa kupigwa risasi kwa waandamanaji hao wanne kumepelekea magavana na maafisa upelelezi kukutana na kuamua kupunguza muda wa kutembea kuwa masaa sita tu toka saa 7 usiku mpaka 12 asubuhi. Hatua hiyo inategemewa kupunguza hali ya uhasama iliyokuwapo kati ya
polisi na raia wa jimbo hilo.
Arusha, TANZANIA. Msuluhishi wa mgogoro wa Burundi Bwana Nelson Mandela amesema kuwa licha ya kuongea na vyama na vikundi 19, pia atakwenda Burundi kuonana na maofisa wa jeshi na vikudni vingine vya upinzani. Katika mazungumzo hayo ya jana yaliyohudhuriwa na Marias sita, ambao ni Pierre Buyoya wa Burundi, Sam Nujoma wa Namibia, Olusegun Obasanjo wa Nigeria, Daniel Arap Moi wa Kenya, Yoweri Mseveni wa Uganda na Benjamin Mkapa wa Tanzania. Muamar Gadhafi wa Libya aliwakilishwa na Waziri Mwandamizi. Mandela amevipa wiki tatu vyama na vikundi 19 hivyo kupitia na kufanya uchambuzi wa mkataba wa Amani. Amevialika vitoe maoni na mapendekezo. Hata hivyo katika hotuba yake iliyojaa hekima, ushauri NASAHA na maelekezo amesema kuwa si maoni na mapendekezo yote yatakayokubaliwa. Ameongeza kuwa usuluhishi lazima ulenge kwenye maslahi ya Taifa.
|
YALIYOMO
Tahariri
Mkapa awatahadharisha wanawake CCM Lipumba: Wananchi wana uwezo wa kuondoa utawala mbovu Wastaafu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuishitaki Serikali Habari za ndani
Sherehe za mwaka mpya wa Kiislamu kufanyika Dar MPASHO NASAHA
Ushauri Nasaha
MAKALA
WAZO LA WIKI
MAKALA
Kalamu ya Mwandishi
MAKALA
Riwaya
Lishe
Makoye: Fedha za Simba nimetafuna mwenyewe |
Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:Bonyeza
hapa
Au
Andika barua kwa: nasaha1420@yahoo.com
|
|
|
|