|
Na. 041 Jumatano Machi 29 - Aprili 4, 2000 |
|
|
|
|
|
Mkapa awatahadharisha wanawake CCM
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Benjamin Mkapa amewatahadharisha wanachama wa chama hicho tawala kutoipuuza nguvu ya upinzani kwa kile alichokieleza kuwa wapinzani wamejiandaa kwa uchaguzi mkuu ujao na wamedhamiria kushika hatamu za uongozi wa serikali. Mwenyekiti huyo wa CCM alitoa tahadhari hiyo Jumatatu wiki hii alipokuwa alifungua kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) kinachofanyika Dodoma. UWT ni moja ya Jumuiya za CCM. Rais Mkapa alikiambia kikao hicho kinachofanyika katika ukumbi wa mikutano wa CCM Makao Makuu kuwa wanawake wanao wajibu wa kuanzisha vikundi vya uhamasishaji kukisemea Chama Cha Mapinduzi na kuwaelimisha wanawake wenzao ili wajue haki zao za kupiga kura na haki zao za msingi kwa kuwapa elimu ya uraia. "Tunataka wanawake wajiamini ili wasibabaishwe na utapeli wa wapinzani...." alisema Mwenyekiti huyo wa chama tawala. Rais Mkapa aliihimiza UWT kutoa elimu ya Uraia na ile ya uchaguzi kwa wanawake kwa vile elimu hiyo inapotolewa na taasisi nyingine huwapotosha wanawake na kujenga chuki dhidi ya CCM. Rais Mkapa alisema zipo baadhi ya taasisi zisizo ya kiserikali (NGOs) hapa nchini ambazo hutoa elimu ya uraia, hususan wakati wa uchaguzi mkuu, ambazo Rais alidai huwapotosha wananchi dhidi ya CCM. Rais Mkapa alisema, "kivuli kimojawapo kinachotumika kuwaghilibu wanawake na (pia) kuwachonganisha na chama tawala ni (utoaji) elimu ya uraia na elimu ya uchaguzi." Alisema tayari hapa nchini "yamezuka" mashirika yasiyo ya kiserikali kwa lengo la kutoa elimu ya uraia kwa njia za semina warsha na makongamano. Akiwaeleza wanawake hao namna ya kukabiliana na kitisho hicho kinachokikabili chama tawala, Rais Mkapa alisema, "...... kwanza tuwe macho nazo; pili, tushiriki semina, warsha na kongamano zao ili inapopasa (pasiwe na budi) kuvisahihisha, kuviumbua na kufichua njama zao". Hata hivyo Mwenyekiti huyo wa CCM hakutaja taasisi yoyote anayoituhumu kuhusika na elimu hizo zinazodaiwa 'kuipiga vita CCM'. Aidha, Rais Mkapa aliwataka wanawake wa CCM kujiweka tayari kugombea nafasi mbalimbali za uongozi ili kuiwezesha CCM kuendelea kutekeleza sera zake. Katika nchi nyingi ambako wanawake wanaruhusiwa kupiga kura kuwachagua viongozi wa serikali, takwimu zinaonesha kuwa wanawake huunda sehemu kubwa ya wapiga kura. Wachunguziwa masuala ya kisiasa na kijamii wamekuwa wakieleza kuwa,
kufuatia kupitishwa kwa sheria ya kumtangaza mgombea urais kwa wingi wa
kura, chama kitakacho jihakikishia 'sapoti' ya wanawake kitakuwa "kimejisafishia
njia ya kwenda Ikulu."
|
YALIYOMO
Tahariri
Mkapa awatahadharisha wanawake CCM Lipumba: Wananchi wana uwezo wa kuondoa utawala mbovu Wastaafu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuishitaki Serikali Habari za ndani
Sherehe za mwaka mpya wa Kiislamu kufanyika Dar MPASHO NASAHA
Ushauri Nasaha
MAKALA
WAZO LA WIKI
MAKALA
Kalamu ya Mwandishi
MAKALA
Riwaya
Lishe
Makoye: Fedha za Simba nimetafuna mwenyewe |
Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:Bonyeza
hapa
Au
Andika barua kwa: nasaha1420@yahoo.com
|
|
|
|