|
Na. 041 Jumatano Machi 29 - Aprili 4, 2000 |
|
|
|
|
|
'Polisi hawana uwezo wa kuzuia mabadiliko' IMEELEZWA kuwa katika jamii yoyote ile uma unapoamua na kuungana pamoja katika kutaka dhulma, maonevu, kukandamizwa na aina nyingine za manyanyaso katika jamii na kupelekea mwamko wa kutaka mabadiliko, basi polisi hawana uwezo wa kuzuia mabadiliko hayo. Akizungumza na mamia ya wananchi wa Handeni katika mkutano wa hadhara wa chama cha Wananchi (CUF) Machi 23, mwaka huu, Mkurugenzi wa vijana wa chama hicho Mhe. Shaibu Akwilombe amesema kuwa kuna ushahidi wa wazi hapa nchini kwa vyombo vya usalama hasa polisi kuingilia siasa kw alengo la kudidimiza upinzani kwa maslahi ya chama tawala cha CCM na serikali yake. Alisema kuw avijana wamepata mwamko wa mabadiliko ya kisiasa kwa sababu katika Taifa lolote lile kukiwa na jambo zuri au baya basi watakao nufaika au kuathirika kwa kiwango kikubwa wanakuwa ni vijana, hivyo alisema, "sisi vijana tuna wajibu wa kutetea maisha yetu na maisha ya vizazi vyetu". Aliendelea kusema kwamba unapoibuka mfumo fulani wa utawala katika jamii kuna makundi mawili ambayo lazima yatokee. Aliyataja makundi hayo kuwa ni ya wale walionufaika na wale walioathirika na mfumo huo. Hivyo akasema, "katika hali kama hii haya ni mapambano ya kitabaka kati ya wadhulumiwa na wenye kudhulumu". Mhe. Akwilombe alisema kwa kuwa CCM imekuwepo madarakani kwa takriban miaka arobaini basi wapo walionufaika na utawala huo na kuongeza, "Hawa ndio watakaopinga mabadiliko haya kwa kupambanisha dola (polisi) na wanasiasa, kwa kuwa hawana hoja". "Tunasikitika sana tunapokuta polisi ambao tumewapeleka kozi CCM (Chuo Cha Polisi) kwa kodi zetu, wakawa wanakula ugali na maharage na nyama kutokana na mapato ambayo yamechangiwa na wazazi wetu, wanageuka na kuwa simba kuwakandamiza wanyonge wenzao", alisema. Aidha, aliwataka polisi wawe na ufahamu kuwa kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano, jukumu kubwa la jeshi hilo ni ulinzi wa raia na mali zao tu na sio kuwatumikia wale wenye kunufaika na mfumo uliopo, kuingilia siasa. Na akawataka vijana waliopo kwenye vyombo hivyo vya dola wawe makini wasijehukumiwa na historia. Katika mkutano huo ambao pia ulihutubiwa na Mwenyekiti wa Chama hicho Prof. Ibrahim Lipumba na kuhudhuriwa na matawi ya Jijini ya chama hicho ya Kossovo, Chechnya na Mashujaa, ilielezwa kuwa matawi 52 mapya yalifunguliwa siku hiyo katika majimbo mawili ya uchaguzi ya Handeni Mashariki na Magharibi.
SHEREHE ya mwaka mpya wa Kiislamu (1421 Hijiria) itafanyika rasmi katika msikiti wa Tungi Temeke Dar es Salaam Aprili 9, 2000. Kwa mujibu wa habari kutoka Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania(Baraza Kuu) ambao ndiyo waandaji wa sherehe hiyo, kamati maalum ya maandali zi imeundwa ikijumuisha wenyeji wa shughuli hiyo ambao ni viongozi wa msikiti wa Tungi itaandaa taratibu zote za sherehe hiyo. Inasemekana kuwa sherehe hiyo ambayo itaanza mara baada ya swala ya adhuhuri na kuisha baada ya swala ya magharibi siku ya Jumapili, zitahudhuriwa na waalikwa kutoka mikoa ya jirani ikiwemo Pwani, Morogoro, Lindi na Tanga. Waislamu wa jijini Dar es Salaam wamejiwekea taratibu zao za kuadhimisha matukio muhimu kwa siku maalumu ambapo hujumuisha kwa pamoja jiji zima siku moja. Mwenendo huo ambao umezaa na kuimarisha mshikamano mkubwa miongoni mwa Maimamu wa madhehebu na taasisi mbali mbali jijini, ulijitokeza katika sherehe za Baraza la Eid lililoandaliwa na Halmashauri Kuu ya Waislamu Januari 2000 katika ukumbi wa Diamond. Mshikamano huo pia ulijitokeza tena katika hitma ya kukumbuka waliouliwa Mwembechai (1998), ambayo ilifanyika kwa kushirikiana na taasisi zote ikiwemo Tanzania Islamic Centre (T.I.C.) ambako hitma hiyo ilifanyika tarehe 13/2/200 ndani ya msikiti wa (T.I.C.) uliopo Magomeni Mapipa Dar es 'salaam. Nao msikiti wa Sinza jijini(Masjid N-Nuur) uliandaa baraza la Eid l-Haj kwa mtindo huo huo wa mshikamano. Aidha Waislamu wamekuwa wakitumia hafla hizo pia kujadili masuala mbali
mbali ya jamii yao, hali ya nchi na mazingira ya kisiasa nchini.
|
YALIYOMO
Tahariri
Mkapa awatahadharisha wanawake CCM Lipumba: Wananchi wana uwezo wa kuondoa utawala mbovu Wastaafu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuishitaki Serikali Habari za ndani
Sherehe za mwaka mpya wa Kiislamu kufanyika Dar MPASHO NASAHA
Ushauri Nasaha
MAKALA
WAZO LA WIKI
MAKALA
Kalamu ya Mwandishi
MAKALA
Riwaya
Lishe
Makoye: Fedha za Simba nimetafuna mwenyewe |
Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:Bonyeza
hapa
Au
Andika barua kwa: nasaha1420@yahoo.com
|
|
|
|