NASAHA
Na. 041 Jumatano Machi 29 - Aprili 4, 2000
Ukurasa wa mwanzo
Islam Tanzania
Matoleo yaliyopita
Wastaafu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuishitaki Serikali 

Mwandishi wetu 

WASTAAFU wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wameipelekea serikali ya Jamhuri ya Muungano taarifa ya kusudio la kuichukulia hatua za kisheria endapo haitatekeleza madai yao.

Kusudio hilo lililowakilishwa kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Kampuni ya Uwakili ya Bishota Dienike chini ya kifungu cha 6 cha sheria za taratibu za serikali, cha mwako 1967 inasema kwamba: 

(a) Serikali imevunja taratibu za kisheria na uaminifu kwa watumishi hao. 

(b) Serikali ilipe malipo kamili kwa wastaafu hao chini ya Sheria za iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki(EAC). 

(c) Serikali itoe karatasi maalum (work sheets) zilizotumika kufanya mahesabu ya malipo kwa watumishi hao. 

(d) Serikali iwalipe wastaafu hao mafao yao kwa kutumia viwango vya fedha vya wakati huu. 

(e) Serikali ilipe fidia kwa kuchelewesha malipo na usumbufu waliopata wastaafu hao katika kipindi chote walichokuwa wanafuatilia mafao yao. 

"Tarehe 2/6/99 serikali ilitangaza kukubali kuwalipa wastaafu hao mafao yao yote kutokana na kutumikia Jumuiya ya Afrika ya Mashariki. Tarehe 30/11/99 serikali ilianza kutoa hundi kwa wastaafu hao. Kilichoshangaza ni kuona kiasi walichopewa wastaafu hao ni kidogo mno, shilingi 10/- na shilingi 170/- Mteja wetu anapinga vikali malipo hayo", imesema sehemu ya waraka huo. 

Kusudio hilo la kuishitaki serikali limendelea kueleza kuwa katika kipindi chote ambacho wastaafu wa EAC walikuwa wanafuatilia mafao yao, walionesha kama kielelezo takwimu zinazoonesha jinsi Serikali ya Uganda ilivyowalipa wastaafu wake wa Jumuiya hiyo, na waliitaka serikali kufuata utaratibu huo. Pia walinukuu Taarifa ya ripoti ya kamati iliyoundwa na serikali kushughulikia mafao ya waliokuwa waajiriwa wa EAC ukarasa wa 38 ambayo ilipendekeza mafao hayo yalipwe kwa kutumia fomula iliyotumiwa na serikali ya Uganda. 

Fomula hiyo iliyotumia na serikali ya Uganda ilikuwa na hatua zifuatazo: kwanza kuweka mafao hayo kama ambavyo yangelipwa tarehe 30/6/1977, pili kukitafsiri kiwango hicho kwa kuangalia vigezo vya makubaliano ya mkataba wa upatanishi wa EAC, tatu kulipa asilimia 7 ya riba kila mwaka toka mwaka ambapo mafao hayo yalitakiwa yalipwe na mwisho kuyatathmini malipo hayo ya mwaka 1977 kwa thamani ya shilingi ya leo. 

Kusudio hilo limemalizia kwa kutaka serikali kutekeleza yote yaliyotajwa humo kinyume na hapo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya serikali. 

Makala ya kusudio hilo ambalo NASAHA imeiipata toka kwa mmoja wa watumishi wa iliyokuwa Jumuiya hiyo zimepelekwa kwa mwanasharia mkuu wa serikali, Wizara ya Sheria na mambo ya katiba, katibu mkuu wa ofisi ya Rais na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi. 

Jumuia ya Afrika Mashariki kabla ya kuvunjika mwaka 1977 ilikuwa na mashirika ya General Fund Services, East African Airways Corporation, East African Cargo Handling Services Company, East African Harbours Corporation, East African Posts and Telecommunications Corporation na East African Railways Corporation. 

Juu
 

YALIYOMO
 

Tahariri
Tume ya Uchaguzi ipigwe msasa, sio wananchi

Mkapa awatahadharisha wanawake  CCM

Lipumba: Wananchi wana uwezo wa kuondoa utawala mbovu 

Wastaafu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuishitaki Serikali

Habari za ndani
Polisi hawana uwezo wa kuzuia mabadiliko’

Sherehe za mwaka mpya wa Kiislamu kufanyika Dar

MPASHO NASAHA
Hawavumi lakini...

Ushauri Nasaha
Urafiki na makuzi ya mtoto

MAKALA
Toba ya ‘Pope' liwe somo kwa utawala wa Mkapa

WAZO  LA  WIKI
Viva Senegal

MAKALA
Tatizo la ubakaji katika jamii yetu:
Mazingira katika shule zetu

Kalamu ya Mwandishi
Tahadhari isipochukuliwa huenda damu ikamwagika Zanzibar

MAKALA
Uchaguzi Mkuu Mwaka 2000 (4)

Habari za Kimataifa

Barua

Riwaya
Kisasi cha mauti

Lishe
Baba kulea ujauzito

MICHEZO

  • Ndoa ya Mobitel na Yanga mashakani
  • Homa ya pambano la Ghana na Stars yapanda

  • Makoye: Fedha za Simba nimetafuna mwenyewe


       Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:Bonyeza hapa
    Au
    Andika barua  kwa: nasaha1420@yahoo.com


    Ukurasa wa mwanzo
    Islam Tanzania
    Matoleo yaliyopita