|
Na. 041 Jumatano Machi 29 - Aprili 4, 2000 |
|
|
|
|
|
Urafiki na makuzi ya mtoto NA KHADIJA IDD MAKUZI ya mtoto yanaweza kugawanywa katika nyanja kadhaa mfano makuzi
ya kimiwili, kiakili, kimaono, kimaadilin.k. Katika makala hii tutajaribu
kuona jinzi marafiki wanavyoweza kuathri ukuaji wa mtoto kimaadili. Upo
msemo kuwa tabia ya mtu inaweza kueleweka vyema kwa kuzingatia tabia ya
rafiki yake au marafiki zake. Msemo huu unatilia mkazo dhana nzima ya kuchagua
marafiki wema ili kujenga tabia njema.
MALEZI ya mtoto huanzia nyumbani kwa wazazi wake. Kipindi cha awalicha maisha ya mtoto (miaka 0-2) mtoto huishi zaidi katika mazingira ya nyumbani natabia zake zote hutegemea tabia za watu wa nyumba husika. Baada ya hapo mtoto huanza kutokana kuchanganyika na watoto wa nyumba jirani pamoja na watu wa vimo tofauti na yake. Piakwa hali ilivyo sasa watotohuanza kwenda shule za awaliau madrasa (miaka 3-6). Baadaye hujiunga na shule za msingi kuanzia miaka 7 - 14 na hatimaye kuingia sekondariakiwa naumriwa mika 15-19. Tutaona kuwa umahiri wa stadi mbalimbali kama lugha, michezo,hobi na mengineyo hupatikana katika kipindi ambacho mtoto ameshaanza kuwa na maingiliano na watu wa nje ya familia yake. Tutakubaliana kuwa wazazi kama waalimu wa mwanzo kabisa wa mtoto watahusika sana na mustakabali mzima wa tabia za mtoto wao. Hawa ndiyo wenye jukumu la kumjengea msingi mzuri wa maadili ya jamii ambapo chimbuko la tabia njema hupimwa kutokanana jinsi mtu anavyoweza kutenda mambo yake kwa kuzingatia maadili ya jamiihusika. Katika nyumba ambaye maadili huchungwa watoto hujifunza pia kuchunga maadili. Marafiki katika familia hizi hulingana kabisa na familia husika katika suala zima la kuzingatia maadili. Utakapofika wakati wa mtoto kutoka nyumbani na kuingia mitaani tayari kuwa amejengewa msingi ambao utamsaidia kupata marafiki wema. Awali wazazi humsaidia mtoto kuchagua marafiki ambao huwa ni wale wanaotoka katika familia zenye maadili mema. Msingi huu pia humsaidia mtoto kuchagua hobi nzuri ambazo haziendi kinyume
na maadili yajamii. Izingatiwe kuwa tabia za wizi, uvutaji wa bangi, madawa
ya kulevya, utoro shuleni n.k. huigwa na watoto wakiwa katika vikundi.
Kama wazazi watawaacha watoto wao bila kuwapa muongozo bora wa namna ya
kupata marafikiwema basi wasishangae watoto wao kukosa kabisa makuzi mwema
katika hii nyanja ya maadilina hivyo kuishia kuwa watu mizigo "liability"
katika jamii.
|
YALIYOMO
Tahariri
Mkapa awatahadharisha wanawake CCM Lipumba: Wananchi wana uwezo wa kuondoa utawala mbovu Wastaafu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuishitaki Serikali Habari za ndani
Sherehe za mwaka mpya wa Kiislamu kufanyika Dar MPASHO NASAHA
Ushauri Nasaha
MAKALA
WAZO LA WIKI
MAKALA
Kalamu ya Mwandishi
MAKALA
Riwaya
Lishe
Makoye: Fedha za Simba nimetafuna mwenyewe |
Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:Bonyeza
hapa
Au
Andika barua kwa: nasaha1420@yahoo.com
|
|
|
|