|
|
|
Na Mujahiid Mwinyimvua Watu wengi hupendelea kunywa maji ya baridi (cold water) hasa majira ya joto. Hata hivyo baadhi wa watu wanaandaa maji hayo kwa njia zilizo kinyume na kanuni za afya bora. Makala hii inalenga kuielimisha jamii kuhusu njia iliyo kinyume na kanuni za afya bora. Pia makala hii itawaelimisha wananchi njia bora (zinazokubalika na kanuni za afya) za kuandaa maji ya baridi. Njia mojawapo inayotumika na baadhi ya watu ya kuandaa maji ya baridi, ambayo ni kinyume cha kanuni za afya, ni ile ambayo mtu anachemsha maji ya kunywa, lakini katika kuyafanya maji hayo yawe baridi mtu anachanganya maji yaliyochemshwa na kipande cha barafu (maji yaliyoganda). Barafu hizo hutengenezwa kwa kutumia maji yasiyochemshwa au yasiyokuwa salama. Njia hii ni kinyume na kanuni za afya bora na ni ya hatari kwa sababu, barafu iliyotengenezwa kwa maji yasiyokuwa salama (yenye vijidudu) inaweza kusambaza vijidudu kwenye maji yaliyochemshwa. Kama tulivyoona katika makala zilizopita, kuwepo kwa vijidudu kwenye maji ni chanzo kikubwa cha magonjwa kama vile kipindupindu, kuharisha na homa ya matumbo. Njia tuliyoiona hapo juu ya waandaaji wa maji ya baridi inatokana na ufahamu mbaya kwa watu wanaotumia njia hiyo. Ufahamu waliokuwa nao ni kuwa maji yakiwekwa kwemye friza na kuganda huwa hayana tena vijidudu. Kwa maneno mengine, watu wanaotumia njia tuliyoiona hapo juu wanaamini kuwa friza au friji inaua vijidudu vilivyomo kwenye maji. Imani hiyo si sahihi. Usahihi ni kuwa, friji au friza hasa hizi za majumbani hazina ubaridi wa kuviua vijidudu vyote vilivyomo katika maji. Kinachotokea ni kwamba, vijidudu hivyo huwa haviwezi kuzaliana (kwa kasi kubwa). Lakini vikipata mazingira mazuri kama vile hali ya joto lililoko katika tumbo la mwanaadamu, vinaweza kuzaliana na hatimae kusababisha maradhi kwa binadamu aliyekuwa na vijidudu hivyo. Njia bora na ambayo inakubalika na kanuni za afya bora, ya kuandaa maji ya baridi ni kuwa, mtu achemshe maji ya kunywa na ayaache yapoe. Halafu ayatie katika chombo safi na chenye mfuniko. Baada ya kuyatia maji hayo katika chombo safi na kuyafunika, ayaweke maji hayo katika friji au friza kwa muda anaoutaka. Wakati wa kuyatumia maji hayo kama yamekuwa barafu (yameganda) au yamekuwa baridi zaidi, ayachanganye maji hayo kwa kutumia maji mengine yaliyochemshwa (ambayo hayajawekwa kwenye friza au friji). Napenda kuimalizia makala hii kwa kuwaomba wananchi wanaofanya biashara ya barafu au maji baridi, wafanye biashara hiyo kwa kutumia maji yaliyochemshwa. Vile vile serikali iwekeze zaidi katika sekta ya majisafi ili wananchi waweze kupata maji safi na salama kwa urahisi zaidi. |
Serikali yaipongeza Africa Muslim
Agency
Wanafunzi Wakatoliki darasa la saba
1998:
Athari ya milipuko Dar, Nairobi: Waliokufa
wafikia 258
Wakuu wa mashule waache ubaguzi
ABU AMEENA: Mwana harakati aliyesilimisha wanajeshi 3000 wa Marekani -2 Kisiwa cha Karafuu chageuzwa cha ulevi Twalaban wadhibiti Afghanistan yote Madina yachapisha kitabu cha rejea MAPENDEKEZO YA KATIBA YA SHIRIKISHO LA TANZANIA Maoni: Nyerere kasema kweli Ujamaa
na Ukristo vimeshindwa
Kina Ngatara na wenzake ndio urithi
tulioachiwa na Wakoloni
HOJA BINAFSI: Suala la Mwembechai,
serikali imeumbuka
Kupigwa mabomu misikitini: Waislamu
tumejifunza nini?
MAONI: Hoja za kutofautisha Yesu
na Issa ni udhaifu na ni uzushi mtupu!
Utangazeni Uislamu kwa nguvu
zote – Sheikh Jongo
Salafiya wataka wanawake
wawe macho na vyombo vya habari
Waumini Misufini Morogoro
waazimia kujenga Msikiti
Serikali yatakiwa kuondoa
askari Mwembechai
|