|
|
| Kisiwa
cha Karafuu chageuzwa cha ulevi
Uchunguzi uliofanywa kwa muda mrefu bandarini Zanzibar umebaini kuwa Zanzibar inaingiza kreti 325 za bia kila wiki kwa wastani. Idadi hii ni sawa na wastani wa kreti 1300 kwa mwezi ambazo soko lake ni Zanzibar na wale wanaokuja kwa muda. Mbali na ulevi huo wimbi kubwa limeendelea kuikumba Zanzibar kwa upande wa pombe za kienyeji. Hivi karibuni kumekuwako na ongezeko la kukamatwa kwa galoni, madebe na matangi (mapipa) ya pombe hiyo. Sehemu ambazo zimekuwa na mafuriko ya pombe hii ni Chukusani, Kisakasaka, Kisauni, Shakani, Kiyanga, Dole n.k. Nyingi ya sehemu hizi ni zile zenye wahamiaji Wakristo kutoka Tanzania Bara. Aidha imebainika kuwa wengi wa wapikaji wa ulevi huo ni hao hao wanaotoka Bara. Uchunguzi umebainisha zaidi kuwa waingizaji wakubwa wa pombe zitokazo nje ya Zanzibar ni Shirika la Utalii, Bottom’s Up, Golf Club, Scotch Store, Shangani Everest Trade, Prakash, Kampuni moja ya Dubai inayomiliki Duty Free Shop (Uwanja wa Ndege) n.k. Watu wa kati na wanaomiliki maduka ya pombe wamebainika ni watu wenye asili ya kiasia (Mabaniani au Magoa), Wakristo kutoka Tanzania Bara na Wazanzibari wanaomiliki mahoteli na mikahawa. Watumiaji wa pombe inayoingizwa, uchunguzi umebainisha kuwa ni wageni kutoka nje ya Tanzania, wafanyazi wa Taasisi za Muungano walio Zanzibar (hususan JWTZ) ambao wengi wao ni Wakristo na Wazanzibari wachache. Pamekuwepo na wasiwasi kuwa ongezeko hili ni katika mkakati maalumu wa kuifisidi Zanzibar kwani imebainika kuwa Sheria ya Utoaji leseni za vileo (pombe) imekuwa haifuatwi. Sheria hiyo inakataza ujenzi au ugeuzaji wa nyumba kuwa mabaa sehemu wanazoishi watu. Maduka ya pombe na mabaa yote yamo ndani ya sehemu za kuishi watu na
yamekuwa yakiongezeka kila siku. Aidha wingi wa wamiliki hawa wa maduka
haya na mabaa wanaonekana ni maajenti au wanafadhiliwa na nguvu zilizofichikana.
Twalaban wadhibiti Afghanistan yote Wapiganaji wa Kiislamu wa Twalaban nchini Afghanistan wameuteka mji wa Taloqan ulioko kaskazini mashariki ya nchi hiyo. Taarifa kutoka Afghanistan zinafahamisha kwamba wapiganaji hao wameukamata mji huo baada ya kuyazidi nguvu majeshi ya upinzani. Wapiganaji hao ambao wamedhamiria kusimamisha serikali ya Kiislamu nchini humo, wameukamata mji huo ulio umbali wa kilometa 240 katoka mji wa Kabul, katikati ya wiki hii. Jeshi la Twalaban lilianza mapambano dhidi ya Serikali ya Afghanistan kufuatia viongozi wa serikali hiyo kushindwa kutekeleza ahadi walizozitoa wakati wa kushika madaraka. Kikosi cha Tawalaban kiliundwa na wahadhiri wa vyuo, wanafunzi wa vyuo, shule za sekondari na vijana wengine ambao wengi wao ni wanafunzi wa aliyekuwa mwanachuoni na mwanaharakati maarufu wa Kiislamu duniani, Sayyid Abul A’la Maududi. Kikosi hiki cha vijana wa Kiislamu awali kiliingia vitani dhidi ya majeshi ya Urusi ambayo yalivamia nchi hiyo mwaka 1980. Baada ya kuyasukuma nje ya nchi majeshi hayo ya uvamizi, kiligeuza mtutu kwa vibaraka wake wakiongozwa na dikteta Najibullah hadi kuung’oa utawala wa kikomunisti nchini humo. Hata hivyo licha ya ushindi ilioupata, Twalaban inadharamia kufanya
mazungumzo na makundi ya upinzani ili upatikane muafaka utakaopelekea amani
ya kudumu nchini humo chini ya Sheria ya Kiislamu.
Madina yachapisha kitabu cha rejea KITENGO cha uchapishaji cha Mfalme Fahd hivi karibuni kimechapisha kitabu cha rejea ya tafsiri ya Qur’an ambacho kitajulikana kwa jina la "Qur’an Interpretation made simple." Waziri wa Mambo ya Kiislamu, Tabligh na Malezi wa Saudi Arabia, Bw. Abdullah el Turki, amerioitiwa kusema kwamba kitabu hicho kitatumika kama rejea katika uandishi wa Tafsiri utakaofanywa siku za usoni. Aidha, Bwana el Turki aliongeza kusema kuwa kitabu hicho huenda kikakidhi
hitajio la kuwa na tafsiri za Qur’an ambazo zitakuwa nyepesi kueleweka
kwa wasomaji.
|
Serikali yaipongeza Africa Muslim
Agency
Wanafunzi Wakatoliki darasa la saba
1998:
Athari ya milipuko Dar, Nairobi: Waliokufa
wafikia 258
Wakuu wa mashule waache ubaguzi
ABU AMEENA: Mwana harakati aliyesilimisha wanajeshi 3000 wa Marekani -2 Kisiwa cha Karafuu chageuzwa cha ulevi Twalaban wadhibiti Afghanistan yote Madina yachapisha kitabu cha rejea MAPENDEKEZO YA KATIBA YA SHIRIKISHO LA TANZANIA Maoni: Nyerere kasema kweli Ujamaa
na Ukristo vimeshindwa
Kina Ngatara na wenzake ndio urithi
tulioachiwa na Wakoloni
HOJA BINAFSI: Suala la Mwembechai,
serikali imeumbuka
Kupigwa mabomu misikitini: Waislamu
tumejifunza nini?
MAONI: Hoja za kutofautisha Yesu
na Issa ni udhaifu na ni uzushi mtupu!
Utangazeni Uislamu kwa nguvu
zote – Sheikh Jongo
Salafiya wataka wanawake
wawe macho na vyombo vya habari
Waumini Misufini Morogoro
waazimia kujenga Msikiti
Serikali yatakiwa kuondoa
askari Mwembechai
|