|
|
|
Na Mwandishi Wetu
Inasikitisha zaidi kuwa baadhi yao ni watumishi wa serikali. Kifungu cha 13(4) cha katiba yetu kinabainisha wazi kuwa, "Ni marufuku kwa mtu yeyote kubaguliwa na mtu au mamlaka yoyote inayotekeleza madaraka yake chini ya sheria yoyote au katika utekelezaji wa kazi au shughuli yoyote ya mamlaka ya nchi." Kifungu cha 13(5) kinatoa fasili ya neno "kubagua" na kukataza ubaguzi wa kidini miongoni mwa mambo mengine. Wakati makala hii inaandikwa, wanafunzi sita (6) wa Kiislamu wa Shule ya Sekondari ya Mkwawa wamepewa muda wa mwezi mmoja waamue ama kuvua hijab au kuhama shule yake na kutafuta shule nyingine. Yanafanywa haya bila kujali vifungu vya katiba vilivyonukuliwa hapo juu. Pia hazingatii wala kujali agizo la serikali kuhusu hijab lililotolewa na Wizara ya Elimu tarehe 28/8/1995 lenye Kumb. No. EDC/10/62/Vol.I/417 na kusainiwa na Kaimu Kamishina wa Elimu, Bwana S.P. Mkoba. Kifungu cha agizo hili kinasema, "Madhumuni ya barua hii ni kuelekeza shule zote za sekonadari na vyuo vya ualimu kuanza kutekeleza mara moja agizo hilo la Rais". Mtu anaweza kushangaa Mkuu huyu wa shule anapata wapi huo ujasiri wa kukaidi agizo la Wizara na pia kutotii sheria mama ya nchi yaani katiba? Imedaiwa kwamba Mkuu wa shule huyo ametamba kwamba hapatavaliwa hijab hapo Mwakwa muda wa kuwa yeye ni Mkuu wa shule hiyo! Ujasiri huu wa kutoa hadi maneno ya mwisho anaipata wapi mtumishi huyu wa serikali isiyo na dini? Sambamba na tukio hili la huko Iringa ambalo lipo pia katika shule nyingi tu hapa nchini, bado hata zile shule na vyuo ambako hijab imeruhusiwa juhudi za chinichini zinafanywa ili wanafunzi Waislamu wanaopenda kuvaa vazi hili wasivae. Moja ya mikakati inayotumika ni wakuu wa shule kukataa kata hata kuingiza vazi hili katika"joining instruction" wanazotumiwa wanafunzi wapya. Hatua hii ni kwenda kinyume na kifungu cha 18 (2) cha katiba ya nchi ambacho kinasema, "kila raia anayohaki ya kupewa taarifa wakati wote kuhusu matukio mbalimbali nchini....ambayo ni muhimu kwa maisha na shughuli za wananchi na pia juu ya masuala muhimu kwa jamii." Mfano wa shule hizi ni shule ya sekondari ya Jangwani iliyo Dar es Salaam. Katika barua ya kuwaita shuleni wanafunzi wa kidato cha tano kuanza muhula wa kwanza tarehe 8/7/98 iliyosaniwa na Mkuu wa shule Mama Theresia Mkamati, sehemu ya sare za shule inasomeka hivi:- 6.A: Vazi Rasmi la shule (uniform) Vazi lenyewe:- (i) Sekti 2 za rangi ya deep orange (angalia mchoro na kipande cha nguo kilichoambatanishwa) (ii) Mashati 2 meupe ya mikono mifupi yasiyo na urembo wa aina yoyote. Kwa mtu wa kawaida ambaye hajasoma atashindwa kuamini kuwa tangu tarehe 28/10/95 hadi leo Augusti 98 bado hajapata muda wa kuongeza kipengele cha kuonyesha sare za wanafunzi Waislamu ambazo tayari ameziruhusu kama agizo la Rais lilivyo; sasa sikuambii mtu mwenye japo elimu kidogo tu. Kwa kuwanyima wanafunzi hao taarifa kuhusu sare anajua wazi kuwa wengi watashindwa kupata sare hizo alizoagiza yeye halalfu tena wakashone na pea nyingine kuzingatia sare ya hijab ya Waislam. Mpango huu bila shaka unasaidia sana kupunguza idadi ya wanafunzi Waislamu wanaovaa hijab mashuleni. Si jambo la ajabu basi kwa sisi tunaoona haya kujiuliza Mkuu huyu wa shule anamtumikia nani? Kama ni Watanzanhia asingevunja kifungu cha 18(2) cha katiba yake (Tanzania) na wala asingechagua kukaidi agizo la Rais ambalo kwa madaraka yake linamlazimu kuwapatia wanafunzi Waislamu taarifa sahihi kuhusu sare zao za shule. Chuo cha Ualim Dar es Salaam hakipo mbali na haya. Ingawa tarehe 16/3/98 Mwalimu Mlezi wa Waislamu aliwatangazia wanafunzi Waislamu juu ya uamuzi wa chuo kuwaruhusu mabinti wa Kiislamu kuvaa hijab, tangazo ambalo lilikuja thibitishwa na Mkuu wa chuo tarehe 23/03/98 bado wanafunzi wapya wa diploma wa mwaka wa kwanza hawakupewa taarifa hii muhimu katika barua ya kuwaita wanafunzi hao chuoni ya tarehe 31/8/98 sehemu ya sare za chuo inasema: 3.Uniform B. Women. (i) A paire of skirts (sample enclosed) (ii) Two white short sleeve shirts N.B. A proper college uniform can also be obtained at the college at the following rates: A skirt at shiling five thousands five hundreds (5,500/-) only. Ni wazi kwamba mwanafunzi akishashona sketi na mashati kama ilivyoagizwa hapo itakuwa vigumu sana kupata fedha za kushona sketi ndefu, mashati ya mikono mirefu na ushungi mweupe: Katika mazingira kama haya ya kubaguana na kunyimana habari vitu ambavyo ni kinyume na katiba yetu, ndipo inapokuwa ni lazima kwa Waislamu kumpata mbaya wao. Huyu ni mbaya kwa sababu anaweza kuwafanya hata watumishi wa serikali kutoitii katiba wala nyaraka za serikali kwa lengo la kutuumiza sisi (Waislamu). Ni mbaya kwa sababu anasimama na kutekeleza dira ya ubaguzi. Kwa mawaziri na makamishna tunategemea watu hawa watarekebishwa ili utumishi wao serikalini uwe ni kwa maslahi ya umma badala ya dini au kabila fulani. Pia kuna taarifa kuwa baadhi ya wanafunzi wa Kiislamu katika mashule ya Wakristo (ambayo siyo seminari) wananyimwa uhuru wa kujifunza dini yao au kufanya ibada zao kama kufunga na kadhalika. Katika baadhi ya shule, wanafunzi hukatazwa kufunga mwezi wa Ramadhani kwa sababu ya ugumu eti wa kuwapatia futari na daku. Ni vyema vyombo vinavyohusika vikafanya utafiti kuona ni mashule mangapi
ambayo usajili wake si wakiseminari lakini zinavunja masharti kwa kuwanyima
wanafunzi wa dini zingine uhuru wa kuabudu.
|
Serikali yaipongeza Africa Muslim
Agency
Wanafunzi Wakatoliki darasa la saba
1998:
Athari ya milipuko Dar, Nairobi: Waliokufa
wafikia 258
Wakuu wa mashule waache ubaguzi
ABU AMEENA: Mwana harakati aliyesilimisha wanajeshi 3000 wa Marekani -2 Kisiwa cha Karafuu chageuzwa cha ulevi Twalaban wadhibiti Afghanistan yote Madina yachapisha kitabu cha rejea MAPENDEKEZO YA KATIBA YA SHIRIKISHO LA TANZANIA Maoni: Nyerere kasema kweli Ujamaa
na Ukristo vimeshindwa
Kina Ngatara na wenzake ndio urithi
tulioachiwa na Wakoloni
HOJA BINAFSI: Suala la Mwembechai,
serikali imeumbuka
Kupigwa mabomu misikitini: Waislamu
tumejifunza nini?
MAONI: Hoja za kutofautisha Yesu
na Issa ni udhaifu na ni uzushi mtupu!
Utangazeni Uislamu kwa nguvu
zote – Sheikh Jongo
Salafiya wataka wanawake
wawe macho na vyombo vya habari
Waumini Misufini Morogoro
waazimia kujenga Msikiti
Serikali yatakiwa kuondoa
askari Mwembechai
|